Makamu wa Rais asisitiza mambo mbalimbali ya kuzingatia kukuza uwekezaji na kuendeleza sekta ya utalii

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Makamu wa Rais, Philip Mipango, akiwa katika hafla ya kukabidhi magari ya kukuza Utalii, Mikumi, mkoani Morogoro amesema kutokana na wingi wa utalii unaoongezeka ni muhimu kwa wawekezaji wa ndani kuwekeza katika kujenga hoteli ili watalii wasiwe wanalala kwenye mahema mbugani

Aidha amezitaka mamlaka kushughulikia malalamiko ya urasimu kwenye mamlaka zinazosimamia sekta ya utalii katika utoaji wa vibali na huduma mbalimbali. Na amezitaka kila mamlaka za mikoa kuwa na jitihada za kuendeleza vivutio vya utalii vilivyopo.

Ametoa wito kwa watanzania kujenga mazoea ya kufanya utalii wa ndani ili kuifahamu nchi vizuri. TANAPA na wizara ya Elimu wametakiwa kutengeneza sera zitakazoongeza ushiriki wa wanafunzi kwenye kutembelea hifadhi.

Makamu wa Rais amekemea uharibifu wa mazingira unaondelee kwenye hifadhi unaotokana na kukata miti, kuchoma moto, kutupa takataka, kilimo cha kuhamahama na ufugaji usiozingatia tija. Lakini pia wananchi kuacha tabia ya kuvamia maeneo ya hifadhi kiholela.

Amesema kutakuwa na Royal Tour sehemu ya pili ili kuendelea kukuza utalii nchini na amezitaka hifadhi ziwe na viingilio rafiki kwa watanzania kumudu kutembelea hifadhi zilizopo. Lakini pia watanzania kufanya kazi kwa bidii na kuendelee kuwa wakarimu kwa wageni wanaotembelea nchini ili kufaidika na ujio wao.

Lakini pia Makamu wa Raisi ameagiza Wizara ya Ardhi, Maliasiri na Utalii pamoja na TAMISEMI kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha maeneo yanapimwa kwaajili ya mashamba, miradi au makazi yasiwe kwenye njia za wanyama pori.
 
Back
Top Bottom