Makamu wa Rais ana kazi gani?

Makamu wa Rais ana kazi gani?

Jibu lake ni rahisi tu. Hizi ndizo kazi zake kwa mujibu wa kifungu cha 47 katiba ya JMT. Kama kuna kazi nyingine atakuwa anafanya zaidi ya hizi hapa basi hasitahili kulipwa kwani hakuajiriwa kwa zaidi ya hizi hapa.
47.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na hususan-
(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hata siku za Mambo ya Muungano;
(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.


(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 37(5), Makamu wa Rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwa pamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chake wakati ule ule anapopendekezwa mgombea kiti cha Rais na watapigiwa kura kwa pamoja. Mgombea kiti cha Rais akichaguliwa basi na Mahakmu wa Rais atakuwa amechaguliwa.


(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa Rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka sehemu moja ya Muungano, basi Makamu wa Rais atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.


Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania




(4) Mtu hatateuliwa kugombea au kushika kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa sheria ya Uraia;
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi;
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.


(5) Chama chochote hakitazuiwa kumpendekeza mtu yeyote kuwa mgombea kiti cha Makamu wa Rais kwa sababu tu kwamba mtu huyo kwa wakati huo ameshika kiti cha Rais wa Zanzibar au kiti cha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.


(6) Makamu wa Rais hatakuwa kwa wakati huo huo Mbunge, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, wala Rais wa Zanzibar.


(7) Endapo mtu ambaye ni Waziri Mkuu, au Rais wa Zanzibar anateuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais ataacha kiti cha Waziri Mkuu, au cha Rais wa Zanzibar, kadri itakavyokuwa.


(8) Makamu wa Rais atatekeleza madaraka yake chini ya uongozi na usimamizi wa Rais, na ataongoza na kuwajibika kwa Rais kuhusu mambo au shughuli zozote atakazokabidhiwa na Rais.
 
Yupo pale kulinda maslahi ya tanganyika zidi ya zanzb,ukimsachi mfukoni hukosi mkasi.
 
Huyu alikuwa na msimamo mkali dhidi ya muungano na hakuna mtu yeyote angemshinda kwa urais wa zanzibar, kwa hiyo kinachofanyika ni kumpumbaza kwa kumzurulisha mitaani kila siku kufanya uzinduzi na kusoma(ni nadra sana kutoa) hotuba, nadhani na vidole vyake vishakuwa sugu kwa kugombana na mikasi kila siku akikata utepe eti uzinduzi(sio kazi yake ya msingi kikatiba) huyu mzee anakula tu kodi yetu bure, majukumu yake kikatiba anayo fanya kwa sasa haya exceed 10% hence when it comes to rating>>absolute failure.
 
Jibu lake ni rahisi tu. Hizi ndizo kazi zake kwa mujibu wa kifungu cha 47 katiba ya JMT. Kama kuna kazi nyingine atakuwa anafanya zaidi ya hizi hapa basi hasitahili kulipwa kwani hakuajiriwa kwa zaidi ya hizi hapa.
47.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na hususan-
(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hata siku za Mambo ya Muungano;
(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.


(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 37(5), Makamu wa Rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwa pamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chake wakati ule ule anapopendekezwa mgombea kiti cha Rais na watapigiwa kura kwa pamoja. Mgombea kiti cha Rais akichaguliwa basi na Mahakmu wa Rais atakuwa amechaguliwa.


(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa Rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka sehemu moja ya Muungano, basi Makamu wa Rais atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.


Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania




(4) Mtu hatateuliwa kugombea au kushika kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa sheria ya Uraia;
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi;
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.


(5) Chama chochote hakitazuiwa kumpendekeza mtu yeyote kuwa mgombea kiti cha Makamu wa Rais kwa sababu tu kwamba mtu huyo kwa wakati huo ameshika kiti cha Rais wa Zanzibar au kiti cha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.


(6) Makamu wa Rais hatakuwa kwa wakati huo huo Mbunge, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, wala Rais wa Zanzibar.


(7) Endapo mtu ambaye ni Waziri Mkuu, au Rais wa Zanzibar anateuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais ataacha kiti cha Waziri Mkuu, au cha Rais wa Zanzibar, kadri itakavyokuwa.


(8) Makamu wa Rais atatekeleza madaraka yake chini ya uongozi na usimamizi wa Rais, na ataongoza na kuwajibika kwa Rais kuhusu mambo au shughuli zozote atakazokabidhiwa na Rais.


Mbona kazi ya kukagua madampo ya taka ya Jiji la Dar hakuitaja ina maana hii iliingizwa kimakosa katika ziara ya Makamu wa Rais au ndo alikuwa anawasaidia na Bwana Afya wa Mikoa na Wilaya?
 
sa mbona yupo off duty? au anatangaza biashara ya kiwanda cha mikasi?
 
sikumbuki bhana, ngoja nitunze swaumu yangu bhana, mbona maswli mengi sana? Nimeuliza vitendea kazi tu? unataka kujua na shule yangu ya msingi.....
Umeenda mbali sana mkuu, lengo ilikuwa ni kutaka kujua uwezo wako wa kufikiri kwa manufaa ya jukwaa isijekuwa tunabishana na chekechea humu
 
navitendea kazi vyake vikoje?

kazi kubwa ninayoiona, ni kusafiri na kukata utepe, Makamu ana kazi yenye raha sana.

Mikasi na mafagio.

Kazi za Makamu wa Rais

1. Kupanda Miti

1.jpg

2. Kuzindua Vifaa vya Kilimo


51.jpg

3. Kutembelea waliopata Maafa


download25283325291.jpg

4. Kuangalia Wagonjwa


305236056.jpg

5. Kuhani Misiba


01252812529.jpg

6. Kuhimiza Usafi
7.jpg


_DSC0087.JPG

7. Kugawa Mafagio
DSC01680.jpg

7. Na kubwa kabisa ni Kukata UTEPE
338.jpg
 
Duh hii kali sana ssana, ngoja nikae kimya
Kazi za Makamu wa Rais

1. Kupanda Miti

1.jpg

2. Kuzindua Vifaa vya Kilimo


51.jpg

3. Kutembelea waliopata Maafa


download25283325291.jpg

4. Kuangalia Wagonjwa


305236056.jpg

5. Kuhani Misiba


01252812529.jpg

6. Kuhimiza Usafi
7.jpg


_DSC0087.JPG

7. Kugawa Mafagio
DSC01680.jpg

7. Na kubwa kabisa ni Kukata UTEPE
338.jpg
 
Ok ok nimekusoma Mpwa wangu nina degree mbili zote za UDSM, ya kwanza nimeisoma kwa miaka minne, ya pili kwa miaka miwili na nina Postgraduate Diploma ya Law (PGDL) na sasa najiandaa kufanya kozi ya Investment, vipi nimejibu kidogo ili turudi kwenye swali la msingi?> Ya kwanza nimeipata 2007 baada ya kujoin Mlimani in 2002, ya Pili nimeipata 2011 umeridhika?
Umeenda mbali sana mkuu, lengo ilikuwa ni kutaka kujua uwezo wako wa kufikiri kwa manufaa ya jukwaa isijekuwa tunabishana na chekechea humu
 
OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,



Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,

KAZI ZAKE NI: KUSIMAMIA NA KUDUMISHA MUUNGANO NA MAZINGIRA
​
 
Kipengele cha kwamba "atafanya kazi zote atakazotumwa na Rais" kina mpa uhuru mkubwa wa kufanya almost everything.....
 
Kazi za Makamu wa Rais

1. Kupanda Miti

1.jpg

2. Kuzindua Vifaa vya Kilimo


51.jpg

3. Kutembelea waliopata Maafa


download25283325291.jpg

4. Kuangalia Wagonjwa


305236056.jpg

5. Kuhani Misiba


01252812529.jpg

6. Kuhimiza Usafi
7.jpg


_DSC0087.JPG

7. Kugawa Mafagio
DSC01680.jpg

7. Na kubwa kabisa ni Kukata UTEPE
338.jpg

PR umehakikisha umeweka picha zote muhimu? hahaha no comment kwa sasa
 
2+(1).jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi, Chanagamoto za Maendeleo na ukuaji wa Miji Barani Afrika. Mkutano huo umefunguliwa leo Julai 24, 2013 Jijini Arusha

3+(1).jpg


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Jarida la Sayansi, kutoka kwa Mkurugenzi wa Sayansi 'Physical Sciences' (COSTECH) Prof. Clavery Tungaraza, baada ya Makamu kufungua rasmi mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha leo Julai 24, 2013

2.jpg




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaongoza baadhi ya wananchi wa mkoani Arusha kuchukua futari, wakati wa hafla ya Futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013

1.jpg


Makamu wa Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Makamu na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam

01+(1).jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kuhitimu Kozi maalum ya Kwanza ya Mafunzo, katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) ACP Charles Omari Mkumbo, wakati wa sherehe za kufunga Kozi hiyo zilizofanyika katika Chuo hicho, Kunduchi jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2013.

001+(1).jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akihutubia wakati akifunga rasmi Kozi ya kwanza ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), katika sherehe za maafali ya wahitimu wa mafunzo hayo zilizofanyika chuoni hapo Kunduchi, Jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2013.
 
Back
Top Bottom