Makamu wa Rais ana kazi gani?

Makamu wa Rais ana kazi gani?

hata mimi naona na cheo cha Makamu wa rais kifutwe kwenye Katiba mpya kwani Waziri Mkuu anaweza kushika madaraka wakati Rais anapokuwa hawezi kuongoza tena.
 
Sasa nani atakuwa anakata utepe kwenye warsha mbalimbali
 
Sarikali moja Tanzania yote ndio jibu la kweli, Enzi zake Dr Bilali aliamuru wafanyakazi wa Tanzania bara waachishwe kazi katika hoteli ya Mawimbini Venta Club Zanzibar
 
Ungejenga hoja yako kivingine lakini sio " ... hana umuhimu ...". Utaona umuhimu wake pale Rais "atakaposhindwa kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na ugonjwa au mapenzi ya Mwenyezi Mungu"; yaani, hapo nchi itakapokosa kamanda mkuu - tutageuka Somalia mara moja.

Hoja yangu hapa sio Makamu wa Rais, bali tupe mbadala mwingine wa nani achukue majukumu ya Rais endapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo. Tunayo mifano ya hivi karibuni kabisa kule Malawi na Ghana tumeona Makamu wa Rais wakichukua madaraka baada ya marais wao kufariki.


Kwa kuwa katiba inatambua waziri mkuu wa jamhuri ya muungano ibara ya 37 (3) (b); Endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano au tashindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu nyingine yoyote, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na mmojawapo wa wafuatao kw kufuata ufuatano
(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake i wazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa; basi;
(b) waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano.
Kwa hiyo ndugu yangu DUDUS kama mbadala mwingine wa nani achukuwe majukumu ya rais ni waziri mkuu na kama naye hawezi au hamudu basi Jaji mkuu ale shavu hilo.
 
Makamo wa Rais yupo pale ili kuziba ombwe la uongozi pindi likitokea. Kumbuka Malawi na Ghana. Malawi ingekuwa kimbembe kama wasingekuwa na Makamo wa Rais.

kimbembe kingetoka wapi wakati kuna waziri mkuu, sipika, jaji mkuu?????????? kwani hapa kwetu ikitokea Rais na makamu wa Rais wako nje ya Jamhuri kwa muda wa zaidi ya masaa 72, kazi na shughuli za Rais zinafanywa na nani?????????????????
 
Swali hili mimi binafsi linanisumbua sana na kwakweli mpaka leo sipati jibu na wala sitarajii kupata jibu la kuridhisha kuhusu umuhimu au ulazima wa kuwepo cheo hiki katika nchi yetu.Kwa kuzingatia mazingira ya kiutendaji na hata ukiangalia kwa kutumia ushahidi wa kimazingira,nafasi ya makamu wa raisi hapa nchin ni mzigo usio wa lazima kwa mlipa kodi na cheo hiki hakina tofauti na waziri asiye na wizara maalum ambae yupo mradi yupo na hata asipokuwepo hakuna athari yoyote itakayojitokeza.

Ushahidi uko mwingi tu.Kwa mfano,linapotokea jambo zitto na labda raisi wa nchi hayupo nchini mara nyingi jukumu hilo hubebwa na waziri mkuu na huwezi kusikia makamu wa raisi kaenda kushugulikia jambo hilo.Tena hapa utakuta watu wanapaza sauti kumtaka hata raisi wa nchi akatize ziara yake huko matokeo yake anatumwa waziri mkuu na makamu wa raisi yupo tu.Mfano mmoja kama sikosei ni yale machafuko ya hivi karibuni mkoani Mtwara.

Hapo ulipo ndugu yangu hebu chukua dakika chache ujihoji wewe mwenyewe, makamu wa raisi mpaka leo hii atakumbukwa kwa jambo lipi katika kulisimamia au kulifanikisha kiutendaji kama makamu wa raisi?Ni maamuzi gani yawe mazito au hata mepesi yamewahi kufanywa na makamu wa raisi ukilinganisha na waziri mkuu?Lowasaa,kwa mfano, atakumbukwa kwa kusimamia shule za kata kama mfano mmoja ingawa zina matatizo.Je aliyekuwa makamu wa raisi,Dr.Shein,anakumbukwa kwa lipi?

Makamu wa raisi akitajwa kwenye vyombo vya habari basi ujue either kaenda nchi za nje kumwakilisha raisi tena na hili ni nadra mno kutokea au kaenda kufungua semina,kongamano,kuzindua ofisi au jengo fulani na hata kuweka jiwe la msingi.

Kwa maoni na mtazamo wangu hiki cheo kipo tu kulinda muungano na si vinginevyo.Ni bora tu cheo cha waziri mkuu na makamu wa rais kirudishwe.

Mwisho wa siku akistaafu anatengewa mafao mazuri kuliko hata waziri mkuu anaeumiza kichwa kiutendaji kulinganisha na makamu wa raisi.

Tuachane na hiki cheo ni mzigo usio wa lazima kwa mlipa kodi!
 
Salaryslip ,Kati ya vyeo vya ovyo kulingana na muundo huu wa serikali ni cha Makamu wa Rais.Kwa katiba mpya hicho cheo ni cha kufuta kabisa.kinaongeza gharama za serikali na ndio maana kazi za Bilal wakati yeye ni kutembea na mikasi tu kwa ajili ya kufungua vyumba vya madarasa na majengo ambayo hata Katibu Tarafa,VEO, WEO,DC,DED anaweza kufanya.
Katika serikali tendaji kama hii ya Tanzania ambayo rais ni Mtendaji, waziri Mkuu mtendaji hakuna haja ya kuwa na MAKAMU RAIS.
 
Last edited by a moderator:
yoyote ambaye hajui kazi za makamo wa rais they need to go back to school .. seriously !? kama watu wazima hawajui no wonder watoto wao wakafeli form 4 alafu wakalaumu serikali :nono:
 
makamu wa rais kazi yake ni kusubiri rais afe ili achukue nafasi yake..hizo mambo za uzinduzi ni kumfanya asiwe idle na asiboreke wakati anasubiria kukaimu
 
yoyote ambaye hajui kazi za makamo wa rais they need to go back to school .. seriJJously !? kama watu wazima hawajui no wonder watoto wao wakafeli form 4 alafu wakalaumu serikali :nono:

Jibu hoja ama lasivyo kaa kimya!Hatutaki majibu ya jumla jumla tupe ufafanuzi!
 
Hana jipya xna anatia umaskin nchin, hana kaz ndo maana anaishia kuzura zurura eti anazindua milad wakat ata mkuu wa wilaya anaweza kuzndua mirad.
 
Jibu hoja ama lasivyo kaa kimya!Hatutaki majibu ya jumla jumla tupe ufafanuzi!


hakuna hoja hapo! mtu mzima hujui kazi za makao wa rais utategemea mwanao anayefanya mtihani wa form 4 afaulu ..??! mambo mengine hayajadiliki kabisa sababu ni viroja ! kesho atakuja kuuliza waziri mkuu ana kazi gani..? mwanaye kapata div 0 anakuja kulaumu serikali .... :nono:
 
Kazi yake kutembea na mkasi.. Kuangaza hukohuko mahala penye utepe
 
Back
Top Bottom