Makamu wa Rais ana kazi gani?

Makamu wa Rais ana kazi gani?

Dr. Gharib Bilal... Mtaalam wa Nuclear! Mpambanaji mwenye kuutetea Uzanzibar wake ! Hali ingekuwa mbaya sana kwa CCM kama wasingemteu kuwa makamu wa Rais! ... Jamaa anawafuasi wengi sana Zanzibar...
Kama tunavyojua kuwa Rais wetu yupo nje ya nchi kwa ziara za kikazi sasa je ni nani aliyemwachia kukaimu kiti chake? na kama alimwachia Makamu wake mbona hapaform vile inavyotakiwa?
 
kuanzia sasa mwiteni Prof jakaya kikwete jamanii,bila kumuita hivyo ni kumdharirishaa
 
Hili nalo neno wakuu! ila huyu aliyepo ndio anaepoteza mantiki ya uwepo wa makamu wa Rais, amepooza sana.
 
Anakazi ya kutembea na mikasi ya kukatia utepe kwenye sherehe.
 
Wakati Jairo alipoonekana kukusanya pesa wakati wa bunge la bajeti na kuonekana ni kosa alilopaswa kuwajibishwa, waziri mkuu alisema hana uwezo mpaka rais arudi. Wakati huo rais alikuwa nje kikazi. Sasa hivi rais hayupo tena kwa muda mrefu kidogo na kuna swala la kashfa ya Escrow. Je ikifika wakati wa kuwajibishana ni mpaka rais atakapopona na kurudi? Kwani rais akiwa hayupo huwa hakuna anayemwachia madaraka ya kutenda kwa niaba yake. Nikiangalia walio baki hata sijui ni nani mwenye nguvu baada ya rais. Hivi yule mzee pale magogoni anaweza kufanya lolote kama rais, Pinda naye ana mamlaka yoyote ya kuwajibisha wazembe na mafisadi. Naona kama kuna Ombwe la kiutawala kwa sasa na mambo mazito kama hayo ya Escrow huenda yakasubiri sana na kisha kusahaulika taratibu kama lilivyokuwa suala la Jairo kwani hata mwenye ofisi akirudi anaweza kusubiri mpaka watuhumiwa wastaafu kama alivyofanya kwenye Richmond na au kuwasamehe kama alivyofanya kwa wale wa EPA
 
Salaam Wanajamii, Ni Kweli Kuwa Ofisi Ya Makamu Rais Ipo Kikatiba.Siku Za Nyuma Vice President Alikuwa Rais Wa Zanzibar Pia.Kwa Sasa Sivyo,anawekwaKama Picha Ya Kuwakilisha Zanzibar,hana Maamuzi,anatumwa Kumwakilisha Rais Kwenye Nchi 'cheap'.Waziri Mkuu Anatosha Kuendesha Nchi Kama Rais Hayup😵MR Ni Mzigo Usio Na Faida.Mnaonaje?Tuchangie
 
makamu wa rais ni cheo kimeundwa ili kuwapumbaza wazanzibar waonekane na wao wanafursa ya authority ktk muungano,na ndio maana hana power yeyote zaidi ya kuzindua miradi tu.
 
Kazi ya makamu wa raisi ni kuridhi nafasi raisi akifa.
 
Habari zenu wakuu.

Leo nina dukuduku ambalo nataka kulitoa. Sijui kama wenzangu linawatatiza pia. Hivi jamani makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana kazi gani haswa?

Nauliza hivi kutokana na ninayoyaona kwahiyo kama sipo sahihi nitarekebishwa. Kila nikiona kwenye vyombo vya habari namuona makamu wa rais aidha anazindua kitu au ni mgeni rasmi sehemu au anafanya ziara sehemu. Yani amekuwa "mzee wa kukata utepe". Ninachosema ni hivi huyu mtu tunaemuita makamu wa rais tunamlipa na kumhudumia kwa ajili ya kuhudhuria sherehe tu? Kwa nchi masikini kama yetu why do we need a ceremonial leader?

Najua watu wataanza kusema oh ni kwa ajili ya ku-accomodate muungano. Siamini hiyo ni sababu. Kwa maana tunaweza kabisa kufuta nafasi ya makamo wa rais na tukasema rais akitoka upande mmoja wa muungano basi waziri mkuu atoke upande mwingine. Kwanini tupoteze rasilimali za nchi kwa ajili ya kuwa na mtu asiye na shughuli za maana ambazo hata rais na waziri mkuu wanaweza waka gawana na kufanya?

Sina nia ya kumshushia heshima makamu wa raisi wala nafasi ya umakamu wa rais ila ninachosema sasa ifike wakati aidha tumpe makamu wa rais kazi za maana za kufanya au tukifute hiki cheo. Kwa ufahamu wangu, Makamu wa Rais ni msaidizi wa rais kwa maana rais ndiyo anaamua ampe kazi zipi makamu wake. Sasa ni kwamba rais hamuamini makamu wake kumpa kazi zozote za maana?

Jamani hili ndilo dukuduku langu.

========

Mkata Utepe mkuu
 
makamu wa rais ni cheo kimeundwa ili kuwapumbaza wazanzibar waonekane na wao wanafursa ya authority ktk muungano,na ndio maana hana power yeyote zaidi ya kuzindua miradi tu.

Bila kuingilia porojo zenu za muungano nauzamzibari....makamu wa rais yoyote nafasi ile ipo kwa ajili ya kutwaa madaraka na kuitisha uchaguzi ndani ya siku 90 pindi rais atakaposhindwa kutekeleza majukumu yake kama olivyoainishwa
 
Kama ilivyo kwenye katiba makamu ana kazi ya kumsaidia rais. mfano anweza kwenda hata katika ziara za nje ya nchi kumwakilisha rais. tatizo mkulu ziaara zote anapiga mwenyewe. maana yake hakuna hasa kazi kuuubwa ambayo rais anampa aifaanye kwa niaaba yake. mfano rais angeweza kukaa ofisini kupitia mafaili kusoma taarifa mbalimbali, kusoma vitabu na kujipa fursa ya uelewa mpana zaidilakini mara nyini yuko ziarani.
Pengine makamu husoma na kupitia maandishi na baadae kumsimulia wakati wamekaa ikulu.
kama hupewi kazi kubwa kubwa kazi ndogo ndogo ni za kwako
 
makamu wa rais ni cheo kimeundwa ili kuwapumbaza wazanzibar waonekane na wao wanafursa ya authority ktk muungano,na ndio maana hana power yeyote zaidi ya kuzindua miradi tu.

Kuzinduaa miradi nankusimamia wizara ya mazingira
Na kumuwakilishaa jamaa anapokuwa na udhulu hana tofauti na kiongozi wa mbio za mwengee
 
Back
Top Bottom