Umesema ukweli,sisi yetu machoHawa vijana maslahi walioikuta CHADEMA imekuwa na inaheshimika wanatumika kama toilet paper kwa kuwadharau waasisi na waliojitolea kuijenga, huyu ni arfi kishafikia hapa kutaka kurudisha kadi, huyu ni mzee mwenye busara na hekima , lakini vijana masalahi wanamtukana na kumdhalilisha, hawa ndio wanashinda humu JF kuizika CHADEMA wakijidai wajuaji , ZZK anasakamwa kule na hutu tuvijana twa ovyo ovyo , wachumia tumbo huu mgogoro hautawaacha salama hata hao kina saaa nane na wenzao, pesa za kuwalipa zimetokana na kura za ubunge za akina arfi , ZZK na wabunge wote CHADEMA, watanzania wakishachoka, mtapata wabunge wawili na katu pesa ya kuwalipa hamtaiona tena.
pole sana makamu ,nimeanza kusikia unahujumiwa mda mrefu,nina ushahidi wakutosha kuwa kuna dada mmoja ambaye kajiunga chama mwezi wa tatu mwaka huu ndiye katumwa na kiongozi mtendaji wa juu wa chama kuja kukuhujumu uonekane haufai ili huyo dada ndiyo agombee ubunge mpanda 2015
wanasahau kwamba wewe ndio umekijenga chama mpanda mpaka kimefika hapo.
Makamu sikushauri ususie chama,wewe ni kiongozi na mbunge unapaswa kupambana mpaka mwisho kuhakikisha dhuluma na uonevu wowote kwenye chama unafika kikomo.
Askari bora ni yule asiyekimbia vita.
Okota silaha yako,mapambano yanaendelea.jipe moyo mkuu,yana mwisho.
Kumbe tatizo ni Uislam wao funguka kamanda....
Chanzo: Gazeti la Mwananchi
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezidi kuandamwa na migogoro baada ya jana kuibuka mwingine mkubwa katika kikao chake cha ndani mkoani Katavi kiasi cha kumfanya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Said Arfi, kutupa kadi yake ya uanachama.
Huu ni mgogoro wa pili mkubwa kuripotiwa katika kipindi cha juma moja lililopita baada ya ule wa wilayani Karatu ambako pamoja na mambo mengine uliishia kwa Kamati Kuu kuusimamisha uongozi wote wa chama hicho wilaya.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa Arfi ambaye ni Mbunge wa Mpanda Mjini, alitishia kujitoa Chadema jana, katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya chama hicho Mikoa ya Katavi na Rukwa kilichoketi Namanyere, Nkasi na kufikia uamuzi wa kumsimamisha Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Mkoa wa Rukwa, Laurent Mangweshi.
Katika kikao hicho, Arfi anadaiwa kuichukua kadi yake ya Chadema na kumtupia Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Rukwa, John Mallack akitangaza kuachia nyadhifa zote alizonazo, kisha kuondoka ukumbini, kabla ya kufuatwa na wazee wa chama hicho na kumsihi aichukue kadi yake hiyo.
Alifikia hatua hiyo baada ya kutokea sintofahamu kati ya wajumbe wa kikao hicho katika uamuzi huo uliofikiwa kwa kupiga kura za ndiyo na hapana.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho vilifafanua kuwa Arfi alikerwa na kauli iliyotolewa na Mangweshi kuwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alipokea rushwa kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Vyanzo hivyo vya habari vimeeleza kuwa kutokana na hali hiyo, Arfi alipandwa na hasira na kuamua kumrushia kadi Mallack kisha kutoka nje ya ukumbi.
"Hatua hiyo ilifanya wajumbe wa kikao hicho nao kutoka nje ya ukumbi na kuanza kumbembeleza ili asichukue uamuzi huo na kisha wakamwekea kadi yake ya uanachama katika mfuko wake wa shati," alisema mmoja wa makada hao.
Arfi mwenyewe hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo baada ya simu ya mkononi kuita muda wote bila kupokewa na hata alipotumiwa ujumbe, hakujibu.
Mallack akizungumza na gazeti hili kwa simu alikiri Arfi kurusha kadi mezani kisha kutoka nje ya ukumbi, lakini akasema suala hilo lilishughulikiwa na wazee na kumalizwa.
"Ni kweli unajua huyu ni Makamu Mwenyekiti wetu wa Taifa, sasa inapotokea vijana wadogo wakamtuhumu kwa tuhuma za uongo na ambazo hazipo inatia hasira, ndiyo maana huyo kijana tumemvua uongozi," alisema Mallack.
Tuhuma za Mangweshi
Mangweshi alisimamishwa uongozi baada ya kutuhumiwa kwa mambo mbalimbali ya kiutendaji ndani ya chama hicho ikiwamo kumkashifu Arfi.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Mallack alisema kuwa Magweshi amevuliwa uongozi baada ya chama hicho kujiridhisha kuwa alitenda makosa hayo.
Alisema kamati ya ushauri ilimwita ili kujibu tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimkabili ikiwamo kutoa taarifa zisizo rasmi bila kufuata taratibu za chama.
"Pia amepatikana na hatia ya kuandika barua za kashfa na kuzipeleka makao makuu ya chama kumkashifu Arfi pamoja na viongozi wengine wa chama akiwamo Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa.
Katibu Mwenezi wa Chadema Mikoa ya Rukwa na Katavi, John Matongo alisema kabla ya kupewa adhabu ya kusimamishwa, amewahi kuonywa mara kadhaa lakini ameshindwa kujirekebisha.
pole sana makamu ,nimeanza kusikia unahujumiwa mda mrefu,nina ushahidi wakutosha kuwa kuna dada mmoja ambaye kajiunga chama mwezi wa tatu mwaka huu ndiye katumwa na kiongozi mtendaji wa juu wa chama kuja kukuhujumu uonekane haufai ili huyo dada ndiyo agombee ubunge mpanda 2015
wanasahau kwamba wewe ndio umekijenga chama mpanda mpaka kimefika hapo.
Makamu sikushauri ususie chama,wewe ni kiongozi na mbunge unapaswa kupambana mpaka mwisho kuhakikisha dhuluma na uonevu wowote kwenye chama unafika kikomo.
Askari bora ni yule asiyekimbia vita.
Okota silaha yako,mapambano yanaendelea.jipe moyo mkuu,yana mwisho.
Hahaaaaaaaaa mbona kuna member kanambia ADC ni tawi la CUF
Kama kuna mtu anamdharau Said Arfi huyo ni mshenzi. Hakuna asiyejua mchango wa huyu mzee katika kukijenga chama na hasa maeneno ya Rukwa. Tunahitaji kusimama imara wana-CHADEMA, kuna wahuni wanatafuta namna ya kupambana na CHADEMA.