Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Arfi) atupa kadi kikaoni, atishia kujiondoa chamani!

Mkulima

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
1,034
1,022
Chanzo: Gazeti la Mwananchi

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezidi kuandamwa na migogoro baada ya jana kuibuka mwingine mkubwa katika kikao chake cha ndani mkoani Katavi kiasi cha kumfanya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Said Arfi, kutupa kadi yake ya uanachama.

Huu ni mgogoro wa pili mkubwa kuripotiwa katika kipindi cha juma moja lililopita baada ya ule wa wilayani Karatu ambako pamoja na mambo mengine uliishia kwa Kamati Kuu kuusimamisha uongozi wote wa chama hicho wilaya.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa Arfi ambaye ni Mbunge wa Mpanda Mjini, alitishia kujitoa Chadema jana, katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya chama hicho Mikoa ya Katavi na Rukwa kilichoketi Namanyere, Nkasi na kufikia uamuzi wa kumsimamisha Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Mkoa wa Rukwa, Laurent Mangweshi.

Katika kikao hicho, Arfi anadaiwa kuichukua kadi yake ya Chadema na kumtupia Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Rukwa, John Mallack akitangaza kuachia nyadhifa zote alizonazo, kisha kuondoka ukumbini, kabla ya kufuatwa na wazee wa chama hicho na kumsihi aichukue kadi yake hiyo.

Alifikia hatua hiyo baada ya kutokea sintofahamu kati ya wajumbe wa kikao hicho katika uamuzi huo uliofikiwa kwa kupiga kura za ndiyo na hapana.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho vilifafanua kuwa Arfi alikerwa na kauli iliyotolewa na Mangweshi kuwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alipokea rushwa kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Vyanzo hivyo vya habari vimeeleza kuwa kutokana na hali hiyo, Arfi alipandwa na hasira na kuamua kumrushia kadi Mallack kisha kutoka nje ya ukumbi.

"Hatua hiyo ilifanya wajumbe wa kikao hicho nao kutoka nje ya ukumbi na kuanza kumbembeleza ili asichukue uamuzi huo na kisha wakamwekea kadi yake ya uanachama katika mfuko wake wa shati," alisema mmoja wa makada hao.

Arfi mwenyewe hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo baada ya simu ya mkononi kuita muda wote bila kupokewa na hata alipotumiwa ujumbe, hakujibu.

Mallack akizungumza na gazeti hili kwa simu alikiri Arfi kurusha kadi mezani kisha kutoka nje ya ukumbi, lakini akasema suala hilo lilishughulikiwa na wazee na kumalizwa.

"Ni kweli unajua huyu ni Makamu Mwenyekiti wetu wa Taifa, sasa inapotokea vijana wadogo wakamtuhumu kwa tuhuma za uongo na ambazo hazipo inatia hasira, ndiyo maana huyo kijana tumemvua uongozi," alisema Mallack.

Tuhuma za Mangweshi
Mangweshi alisimamishwa uongozi baada ya kutuhumiwa kwa mambo mbalimbali ya kiutendaji ndani ya chama hicho ikiwamo kumkashifu Arfi.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Mallack alisema kuwa Magweshi amevuliwa uongozi baada ya chama hicho kujiridhisha kuwa alitenda makosa hayo.

Alisema kamati ya ushauri ilimwita ili kujibu tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimkabili ikiwamo kutoa taarifa zisizo rasmi bila kufuata taratibu za chama.

"Pia amepatikana na hatia ya kuandika barua za kashfa na kuzipeleka makao makuu ya chama kumkashifu Arfi pamoja na viongozi wengine wa chama akiwamo Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa.

Katibu Mwenezi wa Chadema Mikoa ya Rukwa na Katavi, John Matongo alisema kabla ya kupewa adhabu ya kusimamishwa, amewahi kuonywa mara kadhaa lakini ameshindwa kujirekebisha.
 
Kiongozi anayekimbilia kutupa kadi au kujivua uanachama chama chake kinapokuwa na matatizo si kiongozi kitu bali mzigo. Hivi kila mwanandoa atakimbilia talaka baada ya ndoa kukumbwa na misukosuko ya kawaida si wote tutakuwa wahuni? Arfi atafute sababu nyingine ya kujiondoa chamani na wakati muafaka. Vinginevyo ataonekana sawa na mapandikizi na wachumia tumbo na mapandikizi wengine. Rafiki wa kweli utamjua wakati wa dhiki na si mwisho wa mwezi. Kama Arfi kafanya hivyo basi CDM wamtue haraka kabla hajawaozea.
 
Changamoto za kisiasa...

Hawa vijana maslahi walioikuta CHADEMA imekuwa na inaheshimika wanatumika kama toilet paper kwa kuwadharau waasisi na waliojitolea kuijenga, huyu ni arfi kishafikia hapa kutaka kurudisha kadi, huyu ni mzee mwenye busara na hekima , lakini vijana masalahi wanamtukana na kumdhalilisha, hawa ndio wanashinda humu JF kuizika CHADEMA wakijidai wajuaji , ZZK anasakamwa kule na hutu tuvijana twa ovyo ovyo , wachumia tumbo huu mgogoro hautawaacha salama hata hao kina saaa nane na wenzao, pesa za kuwalipa zimetokana na kura za ubunge za akina arfi , ZZK na wabunge wote CHADEMA, watanzania wakishachoka, mtapata wabunge wawili na katu pesa ya kuwalipa hamtaiona tena.
 
Kiongozi anayekimbilia kutupa kadi au kujivua uanachama chama chake kinapokuwa na matatizo si kiongozi kitu bali mzigo. Hivi kila mwanandoa atakimbilia talaka baada ya ndoa kukumbwa na misukosuko ya kawaida si wote tutakuwa wahuni? Arfi atafute sababu nyingine ya kujiondoa chamani na wakati muafaka. Vinginevyo ataonekana sawa na mapandikizi na wachumia tumbo na mapandikizi wengine. Rafiki wa kweli utamjua wakati wa dhiki na si mwisho wa mwezi. Kama Arfi kafanya hivyo basi CDM wamtue haraka kabla hajawaozea.

hii inaonyesha jinsi gani mikoa mingine inabaki kuwa masikini hata kama watapewa kila kitu kwa kijiko.Hawa jamaa ,ndio makamanda wa ukombozi wa ukanda masikini na uliotoa waziri mkuu ambaye pamoja an kutoka usalama wa taifa bado analialia,na kufanya vituko na si maendeleo mkoani kwake.hayupo aggressive kufanya mambo na kakwama ktk chama kibaya

Arfi na Zitto hawajui wanchokiweka ktk line hapa.Wanaweka ktk lini dini yao, wanaweka ktk line reputation ya maeneo wanayotoka.Wanaweka ktk line makabila yao na ukanda waliotoka kuwa na watu wa hovyo na wasio reliable kabisa hata wakipata nafasi bado hawana cha kujivunia.
 
Mahokaaaaaaaaaa!!!!!!! hahahahaahaha,
Dalili ya mvua ni radi
Kwa elimu uliyokuwa nayo utasubiri radi, kwa wataalam tunapima hali ya hewa. Njaa yako na kutaka umaarufu ndiko kuliko kurudisha CCM. Bora ufanye biashara zako, kuliko kujiingiza katika siasa ambazo sasa unajivunjia heshima yako. Kama kweli umeona mafanikio ya CCM,
1) mbona mpaka leo wazee wetu pamoja na babu yako wa Africa mashariki hawajalipwa mafao yao?
2) Barabara gani ya kujivunia? ajari kila siku, hospitali hakuna dawa, vitanda na chafu
3) Shule hazina vyoo, maabara na walimu hajalipwa mishahara yao kwa miezi. hujui hayo?
Uhuru utaletwa kwa kujitolea na sio vibaraka kama wewe
 
Huku kuabudu watu sio kuzuri kwa afya ya chama,sitaki kuamini kuwa eti mtu anasimamishwa uanachama kwa kuongea jambo kwenye kikao lililomkera Boss wake/au kwa kuandika burua ya malalamiko kwenye makao makuu ya chama chake.Chadema inapaswa ikue katika haya.
 
Back
Top Bottom