Makamu Mwenyekiti BAVICHA akamatwa na jeshi la Polisi kwa kutoa kauli za kichochezi

Wakati tunateseka na maradhi we we unaona Ssopi ameleta uchochezi,tunawaza juu ya jinsi tangu Uhuru tukiwa na ccm tumeshindwa kuondoa nyumba za nyasi nchi hii,wewe unawaza vijana Wa chadema wakamatwe,

Tunaishi shule zetu za msingi na sekondari hazina majisafi na salama ,wewe unalishwa matangopori,hakuna dhambi kubwa Duniani kama MTU kupoteza tunu aliyojaliwa na Mwenyezi Mungu" akili" kwa kuwa
Kama Seneta Rahm RAIA Wa USA mwenye asili ya kiisrael anasema" every challenges had its difficults but every choice have difficult decision"

Ccm na nyie vijana Wa Lumumba lazima muwaambie watwezaji wenu kuwa kujenga nchi inahitaji watu makini wasiobebwa na fikra finyu za kichama Bali taswira ya watoto wetu ,wajukuu Wa miaka 50 ijayo watakuta Tanzania IPI?

Hii hii ya wagawana mbao,au itakayokuwa inawika Duniani kwa kukopesha ,kuuza magari nje au ya washabiki Wa muziki Wa Diamond? Tafakari

Rahm Emanuel sio senata Ila Ni meya wa mji wa Chicago huko USA
 
Team buku saba wamechanganyikiwa baada ya kutumika kama TP MAZEMBE au PLASTIC ZA USALAMA Na kumwagwa UDC
 
Aliongea maneno gani? Maana hii nchi kwa sasa ukimtaja tu mkulu unatupwa lumande,tanzania mpya inakuja.
 
Kosa gani alilofanya? ooh ngoja nibashiri.... aliwakosoa viongozi wa serikali!
 
...una chuki binafsi toka siku nyingi,huna lolote!
Kumbe umeona nawe mkuu. Alivyoanza nilidhana ana argument nzuri. Kumbe anafurahi kwa kuwa wana bifu. Roho mbaya hazijengi. Unapowaombea wenzio mabaya nawe ujue iko siku yatakufika.
 
Ila mradi mambo ya ndani ni Mwigulu mwenye historia ya kuandaa vikundi vya mauaji na Raisi ni Magufuli anayeshabikia uvunjanji wa sharia na kuhonga mahakama bilioni 12 ili wawanyamazishe watu basi sosopi ajiandae kwa jela aisee na wananchi tuendelee kukenuwa tuu
 
Hiyo speech yake inapatikana wapi? ili tutafakarina kupima hayo aliyo yasema. Hivi wachangiaji wote kwenye uzi huu wanajua amesema nini au ni kila mtu na upande wake? Bi. Mkubwa anasema tunahojoroka tu.
Nenda swahilitimes.com.. Alikuwa anawaambia vijana wote Tanzania kuvamia polisi kwenye nyumba zao na kuwapiga. Yani kila kijana mtaani kwake anaeishi na polisi amvamie na kumfanyia uhalifu
 


''Sasa kama vijana tuna wajibu mkubwa sana. Nitoe wito nikiwa kama kiongozi wa vijana.

Hili jeshi la polisi, hii salamu iwafikie polisi. Hili jeshi la polisi linaendelea kutumika na Chama Cha Mapinduzi, wakati 90% ya jeshi la polisi tunaishi nao mtaani na hawaishi kwenye makambi yao. Sasa ifike mahali tuseme INATOSHA... Tunaanza na wao kule mtaani (Makofi yanarindima).

If you do me, I do you (shangwe). Hii ndio iwe iwepo ama tukubali km vijana, hili jukumu ni la sisi, sio la akina mzee Lowassa tena.

Ninaomba nitoe wito kwa vijana popote. Na kwa sababu waandishi wa habari mko hapa msichakachue. Tunasema ‘Sasa Inatosha’... Sasa...? (Inatoshaaaaa).

Na kama wanafikiri nafanya uchochezi, maana sasa hivi ikitokea umesifia serikali ya Magufuli unahojiwa, ikitokea umeweza kukosoa unahojiwa.

Vijana wa CHADEMA tunasema, Kama Mbwai na iwe Mbwai – Tunaingia mtaani'' (shangwe).
 
Back
Top Bottom