Makamu Mwenyekiti BAVICHA akamatwa na jeshi la Polisi kwa kutoa kauli za kichochezi

Ni uonevu tu unaofanywa na huyu dikteta kupitia mgongo wa polisiccm wa kuwaweka Watanzania roho juu wa kushindwa kukemea maovu na utendaji mbovu ndani ya Serikali hii na Serikali zilizopita.
hapana hajaonewa.uongeaji wake ulijaa hasira na akashindwa kutambua mazingira aliyopo na nafasi yake katika chadema na jamii kwa ujumla
 
Oh no! Kuhudhuria mahafali ni uchochezi wa kisiasa??

Basi haitoshangaza nchi kuzalisha wakimbizi wa kisiasa pia...
 
Wanajifanya wahuni. Lazima akanyee ndoo iwefundisho kwa wengine. Halafu mbowe alisema atafanya matukio ya kigaidi.

Na hiyo kesi ya kuhujumu taifa. Lazima mnyooke bado wa kwenye mitandao.

Kama unajipenda kaa mbali weee!!!
 
je leo mahafali ya CHASO yaliruhusiwa huko iringa? tunaomba asije akanyang'anywa siraha yake harakaharaka. pia yote yana mwisho...
 
Tayari Jeshi la Polisi limemkamata Makamu M/kiti wa BAVICHA muda huu hapa Iringa Mjini baada tu ya kumaliza Mahafali ya CHASO.

Kosa ni la uchochezi wa Kisiasa ambalo alilitenda akiwa DSM katika Mahafali ya CHASO ya tarehe 18/06/2016.

Hivyo atasafirishwa kutoka Iringa kwenda DSM kwaajili ya mahojiano na baadae Mahakamani.

Imetolewa June 26

Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa
Ngoja Tuimbe na Kucheza KIMASAI.....HIYAAH HEE HEE! HIYAAH KANYAGA! HIYAAA POA! Achani siasa Fanyeni Kazi!
 
Wakati tunateseka na maradhi we we unaona Ssopi ameleta uchochezi,tunawaza juu ya jinsi tangu Uhuru tukiwa na ccm tumeshindwa kuondoa nyumba za nyasi nchi hii,wewe unawaza vijana Wa chadema wakamatwe,

Tunaishi shule zetu za msingi na sekondari hazina majisafi na salama ,wewe unalishwa matangopori,hakuna dhambi kubwa Duniani kama MTU kupoteza tunu aliyojaliwa na Mwenyezi Mungu" akili" kwa kuwa
Kama Seneta Rahm RAIA Wa USA mwenye asili ya kiisrael anasema" every challenges had its difficults but every choice have difficult decision"

Ccm na nyie vijana Wa Lumumba lazima muwaambie watwezaji wenu kuwa kujenga nchi inahitaji watu makini wasiobebwa na fikra finyu za kichama Bali taswira ya watoto wetu ,wajukuu Wa miaka 50 ijayo watakuta Tanzania IPI?

Hii hii ya wagawana mbao,au itakayokuwa inawika Duniani kwa kukopesha ,kuuza magari nje au ya washabiki Wa muziki Wa Diamond? Tafakari
 
Kwanini asikamatwe siku ile ile aje akamatwe leo? Polisi wa Dar walishindwaje kumkamata? Wameona Mahafali yamefanyika kwa Amani wakakosa cha kufanya hivyo wakaona wamkamate Sosopi ili kuondoa nuksi sio?
Hilo ni kosa la jinai halina expire date acha afundishwe adabu!
 
Back
Top Bottom