Makamu Mwenyekiti BAVICHA akamatwa na jeshi la Polisi kwa kutoa kauli za kichochezi

No Comments
Kwa tafsiri ya haraka haraka unaweza kuyaita hayo maneno ya uchochezi. Lakini ukitafakari na kuangalia hali halisisi inayo endelea nchini kwetu,utaona kuwa alichokisema kina ukweli ndani yake. Sehemu yoyote ile iwe kwenye ganzi ya familia, shina, kijiji n.k, haki inapotolewa kwa upendeleo kauli kama hizi huwa haziepukiki. Hata wakati wa ukoloni wapigania uhuru wa nchi yetu waliyasema maneno kama hayo kwa serikali ya kikoloni iliyokuwa ikiwanyima haki. Tumeona akina Nelson Mandela (RIP) na wenzake wameyasema maneno kama hayo kwa serikali ya makabulu. Kwa mtazamo wangu nasema viongozi wetu wajuu wajitafakari sana wakati wanapotoa haki. Wasifiwe biased.
 
Halafu hayo si yaliitwa mahafali ya Wanafunzi kumaliza Chuo Kikuu, hivi kosa la Serikali ni lipi kuyapiga marufuku?

Ndiyo mahafali ya CHASO hayo KUHAMASISHANA KUPIGA POLISI!
CHASO wote waliokuweko kwenye hayo mahafali vyombo vya dola viwafuatilie mmoja baada ya mwingine.
 
Halafu hayo si yaliitwa mahafali ya Wanafunzi kumaliza Chuo Kikuu, hivi kosa la Serikali ni lipi kuyapiga marufuku?
Mkuu, unaongea kama hujaenda shule bwana. Tumeona kuanzia mashule ya sekondary, vyuo, vyuo vikuu n.k kuna vikundi mbali mbali vinavyofanya mahafali kuwapongeza wenzao wanao hitimu. Mfano, vikundi vya dini, wakristo na waislamu wamekuwa wakifanya mahafali kama hayo. Na kinachoongelewa huko pamoja na mambo mengine ni mahubiri. Viongozi wa dini hizo huarikwa kwa ajili ya kutoa nasaa zao kwa wahitimu. Haya yalikuwa mahafasi ya wanachama wa chama cha siasa, je, kwa akili yako ulitegemea nini kiongelewe kama siyo siasa? jaribu kufikiria nje ya box, usiwe confined
 
Kwa tafsiri ya haraka haraka unaweza kuyaita hayo maneno ya uchochezi. Lakini ukitafakari na kuangalia hali halisisi inayo endelea nchini kwetu,utaona kuwa alichokisema kina ukweli ndani yake. Sehemu yoyote ile iwe kwenye ganzi ya familia, shina, kijiji n.k, haki inapotolewa kwa upendeleo kauli kama hizi huwa haziepukiki. Hata wakati wa ukoloni wapigania uhuru wa nchi yetu waliyasema maneno kama hayo kwa serikali ya kikoloni iliyokuwa ikiwanyima haki. Tumeona akina Nelson Mandela (RIP) na wenzake wameyasema maneno kama hayo kwa serikali ya makabulu. Kwa mtazamo wangu nasema viongozi wetu wajuu wajitafakari sana wakati wanapotoa haki. Wasifiwe biased.
Inapendeza akatoe huu utetezi mahakamani.. Kwamba alitaka raia wakaue polisi kwa sababu hizo na mahakama itamwelewa.
 
Siungi mkono vijana kuleta vurugu au kuhujumu familia za polisi huko mitaani, ila pia siungi mkono utendaji wa polisi unaosababisha chuki za kijamii bila sababu za msingi! Viongozi wanaowatumia polisi vibaya ili kufanikisha malengo yao watambue kuwa hao polisi wadogo wanaowatuma hawako wa kutosha, na hawako salama kule mtaani wanakoishi na familia zao! Uvumilivu wa wananchi utakapoisha wajue madhara yatakuwa makubwa sana!
 
Mkuu shida ya jamii yetu ni kwamba tunaangalia upande mmoja tu na kuingiza ushabiki wa kisiasa. Lakini ukweli ni kwamba watu watakapochoka madhara yatakuwa makubwa sana. Mifano ipo mingi tu ambayo watu walivyochoka kuvumilia ilikuwa shida. Tumeona Rwanda, tumeona S.Africa wakati wa utawala wa Makaburu, tumeona Arab spring n.k. Lakini watawala wetu hawataki kujifunza kutokana na makosa yaliyofanywa na watu wengine ili wao wayaepuke.
 
Nimeipenda iyo Kama mbwai na iwe mbwai, duh, vijana kweli wamechoka, ila suluhu ni bora kuliko mapigano na ghasia zingine ambazo zitaleta maafa, haki itendeke kwa vyama vyote ili msije mkatusababishia si tusio na vyama kutembea na miguu hadi nchi za watu
kutafuta ifadhi. Mungu atunusuru tusifikie huko insha"allah
 
Too bad! Vijana uzalendo umekwisha. Mtu anatoaje kauli kali kama hizi? Siasa zisitutenganishe aisee..
 
Back
Top Bottom