Makampuni ya usafi na wamiliki wake

sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,204
4,212
Wana JF, Leo Mh samia katoa neno zito dhidi ya makampuni yenye dhamana ya usafi katika mitaa yetu kuwa yamulikwe kama yanatimiza wajibu wao ipasavyo,naomba tuyataje makampuni hayo na wamiliki wao tuyajadili. Mods leave this topic stand alone please.
 
itabidi tupange na siku ya kuwasomesha wanafunzi mashuleni maana kila shirika linaposhindwa kutimiza majukumu yao itabidi wananchi tuwasaidie kama tulivyowasaidia makampuni ya usafi ingawaje tunawalipa kwa kazi hiyo
 
Sherehe za uhuru wanafanyaga 'wao' tena wanalipwa na lunch, wanapasua matofali kwa vichwa, wanaonesha vifaa vya kijeshi, silaha wanazoita ng'ang'anizi,nk, watu baki hatupewi hiyo posho ya siku, leo hii tumelazimishwa woote tufanye usafi, ni vizuri sana.
Mwaka kesho wamesema sherehe itakuwepo ile ya kawaida pale 'uhuru'... waende- wafanye, asipewe mtu hata senti.. na mwenge ukimbizwe bila sent yoyote ya serikali, tujitolee kuukimbiza kavukavu... hela iende kwenye elimu ya form six iwe bure..over!
 
Jerry Silaa anahusika kwa namna moja au nyingine hakwepi hili wamuache tu bado ana machungu ya kupoteza kila kitu kwa wakati mmoja Baba, Umeya ,Udiwani , Ubunge na Office yake inaelekea UKAWA so kila kitu kiaanikwa bado hawajafika Ufukwe wa Coco unaweza kuja ona kijana anazeeka gafla
 
?.... na mwenge ukimbizwe bila sent yoyote ya serikali, tujitolee kuukimbiza kavukavu... !

Hii nimeipenda.........kimyakimya dadeki.......kuuzima hawataki........bora iwe hivi............
 
Back
Top Bottom