Makampuni ya Madini wanatulipa, hii pesa inaenda wapi?

Makampuni ya Madini wanatulipa, hii pesa inaenda wapi?

Hizo hela hazilingani hata kidogo na hela alizokwapuwa yule "Nyoka mwenye Makengeza" Kama bakshishi ya udalali wa ununuzi wa Rada. Zaidi ya bilioni mia tatu watu waligawana kama njugu na hakuna walichofanywa. Kivuko cha Dar es salaam ni mfano mwingine kuhusu ufujaji wa fedha zetu, lakini mko kimya.

Kuna watu wanakuona Barbarosa kama vile akili imekurudia lakini ukweli wa mambo ni kwamba huwa mnawatoa kafara watu wasio na madhara kwenu kuhalalisha "Uzalendo" wenu kwa Tanzania. Hizo hela za Kahama unazilinganishe na zile zinazotumika kule chato kufanya uwekezaji ambao hauna tija kwa taifa kwa mwaka huu wala kwa miaka kumi ijayo?


Sijaleta hii Mada kutafuta mchawi, kumshutumu yoyote kwa lolote wala kulinganisha nani kafanya nini na wapi bali nimeleta ili kutataka kufahamu jinsi Wilaya ya Kahama inavyotumia hizo fedha kama kuna mwenye uelewa, ni hivyo tu!
 
Ushasema sio mwanaKahama, alafu unataka kufahamu matumizi ya milioni 700 ungekuwa mwenyeji ningekushauri umfate diwani wako, angekupa maelekezo
 
Ushasema sio mwanaKahama, alafu unataka kufahamu matumizi ya milioni 700 ungekuwa mwenyeji ningekushauri umfate diwani wako, angekupa maelekezo


Kama una ufahamu unaweza kuweka hapa kwa manufaa ya wengi!
 
Sijaleta hii Mada kutafuta mchawi, kumshutumu yoyote kwa lolote wala kulinganisha nani kafanya nini na wapi bali nimeleta ili kutataka kufahamu jinsi Wilaya ya Kahama inavyotumia hizo fedha kama kuna mwenye uelewa, ni hivyo tu!
Ukizungumzia kwamba mvua hainyeshi na mtu akakwambia kwamba kama mvua hainyeshi kuna uwezekano mkubwa sana wa kutokea kwa njaa, wewe unamwambia sizungumzii njaa bali mvua kutokunyesha utakuwa sahihi? Hoja yangu ni kwamba hao wa Kahama wanafanana na wale waliogawana hela za ununuzi wa Rada, kivuko cha Dar es salaam na zile hela za Escrow. Hawa wengine huwa wanatetewa kwa kuwa ni viongozi waandamizi wa "chama"?
 
Ukizungumzia kwamba mvua hainyeshi na mtu akakwambia kwamba kama mvua hainyeshi kuna uwezekano mkubwa sana wa kutokea kwa njaa, wewe unamwambia sizungumzii njaa bali mvua kutokunyesha utakuwa sahihi? Hoja yangu ni kwamba hao wa Kahama wanafanana na wale waliogawana hela za ununuzi wa Rada, kivuko cha Dar es salaam na zile hela za Escrow. Hawa wengine huwa wanatetewa kwa kuwa ni viongozi waandamizi wa "chama"?


Na hoja yangu haikuwa kulinganisha chochote kile, bali ili kuwa ni 100% ufahamu wa matumizi ya fedha wanayolipwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama na mgodi wa Buzwagi, siyo zaidi ya hapo, hivyo kama una fahamu unaweza kuelezea hapa, kama haufahamu basi kaa tu kimya au tafuta Mada zenye kuongelea hayo unayoyataka na hapa JF huwezi kuzikosa!
 
Matumizi ya hizi pesa weekend mjini kubwa bata bajaji na daladala sio issue kipindi kile uchaguzi wa 95 watakua wanafuja mvua zinanyesha watu wakalime, halimashauri viongozi mtaa hauna ajira zikitoka tengua teua mamlaka hyo.
 
Kahama ni miongoni mwa wilaya chafu, bora wangewekeza kwenye kuboresha miundombinu ya mji mitaro na dustbins.
Ukiacha hiyo service levy wanapokea nyingine nyingi kutoka kwa mgodi wa kakola na migodini mingine midogo.
Niliwahi kufika korogwe tanga na kushangaa kwa nini kule pamepangika na rami hadi mitaani na hakuna chochote ila kahama ilikuwa choka mbaya. Ingekuwa Uwezo wangu migodi ingepewa Uwezo wa kusimamia miradi ya hizo pesa maana hao jamaa wa almashauri sioni kama wanaaminika. Migodi ilipowajengea kahama rami Klm tano hapo mjini kazi ilionekana na kwa wakati.
Iwekwe system ya kufuatilia hizi pesa huwa zinaenda wapi. Uko sahihi kada Barbarosa
 
Nimesoma kwenye blogu ya Michuzi kwamba mgodi wa Buzwagi umeilipa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama shilingi Milioni 700, binafsi siyo mwenyeji wa Kahama na wala sipafamu lkn natambua kwamba hii siyo fedha ndogo, sasa swali ni Je kwa wakazi au watu wanaoifahamu Kahama, kuna mahali hii fedha inaonekana? Kwa maana siyo mara ya kwanza wao kulipwa fedha na mgodi wa Buzwagi, kuna chochote ambacho unaweza kusema ukifika Kahama utaona kwamba hii ni Halmashauri inayopokea Milioni 700 ktk kwa muwekezaji? Ninachomaanisha wanaiwekeza wapi? Ni kwenye Elimu, Miundo mbinu, Maji au hata ustawi wa jamii wa wananchi wa Wilaya ya Kahama?

1.png
Kiutaratibu hayo ni Mapato ambayo huainishwa kwenye budget za halmashauri husika, hukusanywa na kupangiwa matumizi.Chukua mfano wa wilaya ya Ushetu wilaya mpya ambayo zamani ilikuwa sehemu ya Kahama iliripoti kupokea takriban 1500milioni kutokana na mauzo ya Tumbaku 2015, ikiwa ni 80% ya mapato ya Halmashauri huyo. Hata hivyo kuna upigaji mkubwa unafanywa na wakusanyaji wa Halmashauri hizo ambao hupita kwenye Makampuni hayo na kuwashawishi wahasibu walipe kupitia account ambazo sio sahihi ili wachakachue vzr.
Wanasiasa wetu wanapigwa kanzu ndefu bila kujua lakini mwisho wa siku Utasikia CCM au Halmashauri inayoongozwa na Ukawa (Wapinzani) wameshindwa.
LA ajabu kubwa zaidi ni pale Watendaji HAWA wanapochukuliwa hatua utasikia wanasiasa wa upande mwingine wanaibuka na kuwatetea kwa visingizio rahisi ati, ooooh, taratibu, kanuni za utumishi, haki gani sijui...., nakadhalika...
Kuna taarifa ya watumishi wa Halmashauri hiyo ya Kahama kusimamishwa kwa tuhuma mbalimba..., isitoshe inadaiwa wamekutwa na mamia ya Mamilion kwenye accounts zao.
Kwangu Mimi adui wa kwanza wa Watanzania ni Mtumishi wa Umma, kisha ndio afuate msimamizi wake wa kisiasa na chama kilichopo madarakani.
Ndio maana hata Halmashauri zilizoshikwa na Upinzani bado hakuna hatua yoyote ya maana iliyopigwa kwani HAWA mchwa bado wapo, na ukiwagusa wanapata watetezi hasa humu JF.
Bado kwa unafiki mkubwa watumishi hawa hujinasibu na upande wa pili nao wakilalamika eti serikali imeshindwa.. Shame on them..
Kuna haja ya kurebisha sheria za utumishi haraka ili waweze kushughulikiwa mapema kwa harka.
 
Siyo kahama tu , umewahi kujiuliza serikali hii inalipwa bei gani kutokana na madini yake ? Na je hao waliolipa tsh 700 mil wao walipata bei gani ?

Wewe ni kati ya vi...ru..ka njia wa ccm hapa jf nadhani sasa umeanza kupata akili .
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Nimecheka sana. Leo limefunguka macho ndio linaanza kushtuka eee!!!
 
Hilo halina ubishi na niko na wewe kwenye hili, lkn ukweli unabakia kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Kahama inalipwa milioni 700 shilingi, sijui kama ni kwa kila mwaka lkn najua siyo mara ya kwanza, sasa hiyo fedha inatumikaje? Najua siyo nyingi kwa Wilaya kubwa kama Kahama lkn ni lazima ionekane mahali sasa ni wapi, kwa maana kama ni mishahara ya Wafanyakazi bado Serikali KUU inalipia, sasa wanaitumiaje?
Mimi nimetoka Kahama mwezi jana ukifika 10km kabla hujaingia Kahama utaona milima iliyotengenezwa ya kufika mawinguni, inauma sana inavyofukuliwa nchi na hakuna la maana linalotubakia.

Ni kweli kahama ni mji mkubwa na ni kati ya halmashauri zilizo giants
 
Sawa natambua kwamba ni siyo nyingi lkn ni lazima ionekane mahali, yaani ni lazima itumike na ndicho ninachopenda kufahamu, hizo fedha zinatumikaje?
Angalau leo ujinga unaanza kukutoka
 
Na hoja yangu haikuwa kulinganisha chochote kile, bali ili kuwa ni 100% ufahamu wa matumizi ya fedha wanayolipwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama na mgodi wa Buzwagi, siyo zaidi ya hapo,
Wewe kutokutaka kuhususisha na hoja zingine hakuzuii wachangiaji kuhusisha na hoja zingine!!
 
Wewe kutokutaka kuhususisha na hoja zingine hakuzuii wachangiaji kuhusisha na hoja zingine!!


Sawa, lkn usinihusishe mimi na huo uchangiaji wako, sina haja ya kujua/kusikia mambo mengine zaidi ya haya niliyoyauliza!!
 
Hilo swali nin gumu kuliko jiwe...
Lilipaswa kuulizwa na wana Kahama...lakini ukute hawajui hili wala lile...

Kuna almashauri fulani wao walijengea ela yote ukuta wa almashauri....ha ha ha..we acha tu wakati jengo la almashauri lilijengwa wakati wa mjerumani...limechoooka...ukuta wa bei mbaya...
Hii Geita jamaa pale halmashauri na ofisi ya mkoa walikuwa wanajua kuiba tu
 
Mimi sio mwenyeji wa KAHAMA ila nikishawai kukaa kahama mjini kama mwezi mmoja hv..kitu ninachojua kahama ni moja ya almashuri inayokusanya mapato mengi sana...nilidhani we unayeshinda viunga vya Lumumba unalitambua Hili.

Kahama kuna mzunguko mkubwa sana wa hela kwani ipo pia karibu na mgodi wa Bulyhankulu na pia uchimbaji Mdogo Mdogo ni mkubwa sana. Ulimaji wa mpunga ni wa kiwango cha juu sana pia. Kwa hyo kipindi cha msimu Biashara ya mchele huwa inashamiri sana

Kutokana na mzunguko Nzuri wa hela bank nyingi tu zina branch KAHAMA mjini..kwa mfano Crdb, NBC, nmb, backlays, DTB, BOA, Access, Azania bank etc etc

Nilikaa KAHAMA mwaka 2010 ila sikuridhika Kabisa na kuwa eti ni miongoni mwa almashauri zinazikusanyaji mapato makubwa kwani hata Barabara za ndani ya mjini wakati huo zilikuwa ni za Vumbi..nilipita tena mwaka 2013 nikakuta barabara zimewekwa ile lami yetu ya kubabia...kwa sasa siwezi nikasema chochote kwani ni muda sijapita huko.

Tunashukuru Mungu sana mkuu Barbarosa kwani akili zimeanza kukurudi na sasa unahoji vitu vya msingi..tutaendeleza maombi yetu ili usirudi kule ulikokuwa.
 
Barbarosa asante kwa thread ya jana na hii ya leo kwa ujumla, nimefurahi kwamba umeanza kuuona ukweli kwa baadhi ya mambo, hongera kwa kutokufungwa na fikra potofu, umewapoteza na kuwaumiza wengi ila tutayasahau na kuendelea mbele na wewe kama ndugu yetu assadsyria3 na wengineo. Hii nchi haijengwi kwa matamko ya vitisho, ni nchi yetu sote, tusipokemea tutapotea wote. Hakika hongera sana japo umetuumiza kwa mambo ya uongo. I wish Team Lumumba wangekua wanaleta mojadala ya namna hii kila siku mngepata watu wa maana zaidi. Once again, hongera kwa kusema ukweli. Hayo ndio Upinzani wanayoyapigia makelele kwa nguvu zao zote.
 
Hilo halina ubishi na niko na wewe kwenye hili, lkn ukweli unabakia kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Kahama inalipwa milioni 700 shilingi, sijui kama ni kwa kila mwaka lkn najua siyo mara ya kwanza, sasa hiyo fedha inatumikaje? Najua siyo nyingi kwa Wilaya kubwa kama Kahama lkn ni lazima ionekane mahali sasa ni wapi, kwa maana kama ni mishahara ya Wafanyakazi bado Serikali KUU inalipia, sasa wanaitumiaje?
labda vikao vya kamati na ulinzi,,,hahaaa
 
Back
Top Bottom