Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Nimesoma kwenye blogu ya Michuzi kwamba mgodi wa Buzwagi umeilipa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama shilingi Milioni 700, binafsi siyo mwenyeji wa Kahama na wala sipafamu lkn natambua kwamba hii siyo fedha ndogo, sasa swali ni Je kwa wakazi au watu wanaoifahamu Kahama, kuna mahali hii fedha inaonekana? Kwa maana siyo mara ya kwanza wao kulipwa fedha na mgodi wa Buzwagi, kuna chochote ambacho unaweza kusema ukifika Kahama utaona kwamba hii ni Halmashauri inayopokea Milioni 700 ktk kwa muwekezaji? Ninachomaanisha wanaiwekeza wapi? Ni kwenye Elimu, Miundo mbinu, Maji au hata ustawi wa jamii wa wananchi wa Wilaya ya Kahama?