Makampuni Makubwa Yatikisika

Makampuni Makubwa Yatikisika

Kama aliyekua akiishi kama malaika ataishi kama shetani je wewe uliyekua kuishi kama shetaini umewahi jiuliza utaishije?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilitaka kukuonyesha kuwa "this is happening by plan and not by accident" kwani hayo ndio maono ya watawala wetu. Kuhusu maisha yangu, hakika ninapigika kwa kwenda mbele kama zamani.
 
Mabadiriko ya kisiasa na kiuchumi huambatana na athari chanya na hasi.Maboresho ya sera,sheria,usimamiaji sheria,utekelezaji maazimio na usimamiaji.Athari chanya na hasi haziepukiki pindi mapinduzi ya taratibu za kimaisha zinapobinuliwa kwa maslahi tofauti kitaifa na kiuongozi.

Taasisi na makampuni mengi za kibiashara {uwekezaji} zimeyumba hata kupelekea kufunga biashara,kupunguza wafanyakazi,kusimamisha biashara,kuuza hisa na kutafuta wabia mbadala.lakini pia zipo kampuni ambazo zimewekwa chini ya uangalizi wa taasisi za fedha na nyingine kuwa katika mchakato wa kufirisiwa.

Mfano wa taasisi na makampuni tajwa ni Airtel {Redundancy},TBL{Redundancy},Home Shopping {Change Name},GSM Malls {Punguza Wafanyakazi},GSM Media {Imefungwa},Living Room {Kupunguza wafanyakazi},Subway-Diamond Plaza {Fungwa},IPP,SSB,Cocacola,Bravo {redundancy},BMTL {redundancy},Freightworld {redundancy},MTL,DSM Collidor,Quality Group,Abla Properties {...},Spencon {winding up},Acacia {Makinikia},Twiga Bancorp {Supervisory},Gapco {Sold to Total} n.k..

Kama taifa yatupasa kuhakiki faida na hasara za muda mrefu za mabadiriko,marekebisho,maboresho na ufinyangaji wa michakato,sera,usimamizi,utekelezaji wake.Ninayo imani yamkini ipo nia thabiti kabisa ya kila linalofanywa sasa kwa faida za kizazi kilichopo na kijacho hivyo basi tathmini ifanyike ili kulinda biashara halali zilizopo pamoja uwekezaji wa mabilioni na wenye athari mtambuka {ajira,kodi,n.k}.
Vodacom-also redundancy
 
Tuseme haya makampuni yalikuwa hayalipi kodi . Lakini yalitoa ajira , walioajiriwa walilipa kodi , waliweza kumudu gharama za maisha ya kila siku, waliweza kusomesha watoto na ndugu na kuwasaidia wazee wao kwa mishahara waliyopata kutokana na hayo makampuni yasiyolipa kodi, walipokuwa wakienda kazini walikodi tax, au boda boda, au bajaji au walipanda daladala au walitumia magari Yao binafsi. Ina maana hawa waajiriwa walioongeza mzunguko wa pesa na kutoa ajira kutokana na matumizi Yao.

Lakini je Hiyo kodi iliyokuwa inakusanywa miaka ya nyuma au sasa hivi inatumika vile ambavyo sisi walipa kodi tunataka?

Kuyumba kwa kampuni moja kunaathiri kampuni nyengine mmoja kwa Moja kwa kuwa mzunguko wa fedha unakuwa umepungua.
Hela zetu nyingi zinatumika katika matumizi ya anasa ma vx, posho n.k.

Siungi mkono kampuni kutokulipa kodi Lakini ni bora isilipe kodi kuliko kufungwa . Athari ni kubwa .

Ni sahihi kabisa.Extensive effects
 
Back
Top Bottom