Ahsante mkuu, ngoja tuone kama ataushughulikia mara nyingi huwa wanapuuza mawazo yetu huku kwenye mitandao.
Huyu Mheshimiwa si kuna kipindi alikuwa kule wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia ? Hapa ndio alitakiwa atuonyeshe huo ujuzi wake kwa kutatua haya matatizo kisayansi na teknolojia na sio tu kinadharia.
Kuna muda huwa nashindwa kuelewa hawa viongozi wetu tena Maprofessa wakubwa wanaokosa ubunifu kabisa, sikuona ulivyoongeza updates anaposema wafanyakazi wa serikalini wote walazimishwe kusafiri na ndege za ATCL.
Kuna maswali najiuliza:
- Je amefanya uchunguzi wa idadi ya wafanyakazi wa serikalini wanaosafiri kwa siku na kuona kama ndege hizo zitajitosheleza na kutoa huduma kwa ufanisi kwa wafanyakazi wote wa serikalini?
- Je kulazimisha huku kutakuwa na unafuu kwa mtumishi wa serikali na serikali bila kuiathiri ATCL.
- Je nini ni chanzo hasa cha kufanya wasafiri wakimbilie mashirika mengine?
- Inamaana hatuwezi kuyashinda hayo mashirika at their game bila kutumia nguvu ya serikali kulazimisha kupata wateja ?
Ni sawa na kusema wafanyakazi wote wa serikalini walazimishwe kutumia TTCL wakati nikifika tu kimara sipati signal yoyote. Tutapata wateja wengi halafu huduma mbovu, tutakuwa tumeenda mbele au kurudi nyuma?
Wafanye hata basic SWOT (Strengths, Weaknesses, Opportunitues, Threats) analysis kabla ya kutoa matamko.
Ikionekana wanakosa kabisa ubunifu waweke hata competition kwa vijana wabunifu waoneyeshe ni maeneo gani wanaweza kuyaboresha kwa ATCL na mshindi apewe fursa ya kutekeleza hilo pendekezo ana usanifu wake, ninaamini kuna vijana wengi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko nchini na wako tu mtaani wanatangatanga.