Tatizo la ATCL ni kubwa sana kuliko vile watu wanavyodhania.
Ni shirika lililoanzishwa kisiasa, Linafanya kazi kisiasa, Lilikufa kisiasa na sasa linafufuliwa kisiasa. Siasa na Biashara ni kama Maji na Mafuta, huwa haviendani kabisa.
Yaani, Waziri Mzima anasema, uwekwe utaratibu ili wafanyakazi wa serikali wanaposafiri kwa Ndege basi Walazimishwe kupanda ndege za ATCL pekee!!
Sijui kama waziri anajua athari za kauli yake kwa makampuni mengine ya ndege, Ubora wa Huduma za ATCL, Wajibu wa mfanyakazi wa serikali nk.
Sijawahi kuona siasa ikifanikisha biashara.
Ni suala la muda tu, ATCL itakufa tena, na tutaendelea kumsaka mchawi milele.
Anayeiloga ATCL ni serikali yenyewe.