Makamba: Bei ya umeme haijapanda

Kelvin X

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,931
2,367
Akijibu swali bungeni hivi leo asubuhi amesema taarifa zinazo zagaa mitandaoni kuhusu kupanda gharama za umeme ni potofu na zina faa kupuuzwa.

====
Serikali imewataka wananchi kupuuza taarifa za kwamba bei ya umeme imepanda nchini.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Juni 9, 2022 na Waziri wa Nishati, Januari Makamba wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nyasa (CCM), Stella Manyanya.

Mbunge huyo alihoji kama ni kweli bei ya umeme imepanda maana katika mitandao ya kijamii kuana taariza inazunguka kuwa bei ya umeme imepanda.

Akijibu swali hilo, Makamba amesema si kweli kwamba bei ya umeme imepanda na kuwa Serikali inasikitishwa na uvumi huo.

Amesema kuwa tayari wameshazitaka mamlaka zichukue hatua kwa watu ambao wanaeneza uvumi huo.

“Mchakato wa kupandisha bei za umeme ni mrefu na unahusisha maoni na wadau ni lazima washirikishwe pale bei inapotaka kupandishwa,”amesema Makamba.
Advertisement

Amesema mchakato huo sio wasiri ni lazima uwashirikishe wadau watoe maoni yao.

Naye Mbunge wa Viti Maalum, Salome Makamba alihoji Serikali inampango gani wa kuhakikisha kuwa maeneo ya viwanda katika jimbo la Shinyanga mjini yanapata umeme.

Akijibu swali hilo Makamba amesema Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limeanzisha programu kwenye maeneo ya uzalishaji ikiwemo kwenye viwanda na migodi.

Amesema katika programu hiyo itawahusu pia maeneo ya Shinyanga Mjini
 
Akijibu swali bungeni hivi leo asubuhi amesema taarifa zinazo zagaa mitandaoni kuhusu kupanda gharama za umeme ni potofu na zina faa kupuuzwa.

Chanzo: TBC
JF kiboko, marope siku zako zinahesabika za UWAZIRI wako, PICHA huku Kanda ya ziwa haisomi Kwa waliokubeba.
 
Hiyo hapo vip?
20220610_112638.jpg
 
sina uhakika na bei kupanda ila wana tabia ya kuhamisha watu kutoka tafiff ya chini kwenda ya juu, mimi wamenifanyia hivo wakati matumizi yangu kwa mwezi ni units 60.
Kama wapo humu wanijibu hawa Tanesco kwanini wamefanya haya
 
Unit 60 ni nyingi
 
Naye Mbunge wa Viti Maalum, Salome Makamba alihoji Serikali inampango gani wa kuhakikisha kuwa maeneo ya viwanda katika jimbo la Shinyanga mjini yanapata umeme.

Akijibu swali hilo Makamba amesema Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limeanzisha programu kwenye maeneo ya uzalishaji ikiwemo kwenye viwanda na migodi.

Amesema katika programu hiyo itawahusu pia maeneo ya Shinyanga Mjini

Huyu Salome Makamba ni Ndugu yake January Makamba?
 
Hapo mwezi wa nne :Malipo yamekamilika.37209837550
9001221011728002566
Units 28.1KWH

Token 0617 5813 0199 3907 1094

Cost 8,196.73
VAT 18% 1,475.40
EWURA 1% 81.97
REA 3% 245.90
TOTAL 10,000.00 11/04/22 17:27 alafu ona mwezi wa sita:

Ndugu mteja, muamala: 35608999318 ulioufanya tarehe 02/06/22 16:02, kiasi: Tsh 10,000 kwenda LUKU GePG ( null ,37209837550
9001221531602319193
Units 25.2KWH

Token 2026 6056 2640 1999 5247

Cost 7,377.05
VAT 18% 1,327.87
EWURA 1% 73.77
REA 3% 221.31
Debt Collected 1,000.00
TOTAL 10,000.00) umekamilika. Salio lako jipya ni TSh 146,071.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom