Makamba avalia njuga ‘bodaboda’

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225

Imeandikwa tarehe 28 Desemba 2013 By Mwandishi Wetu, MwanzaNAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema Serikali haitavumilia baadhi ya askari Polisi wanaonyanyasa waendesha pikipiki za ‘bodaboda’. Akihutubia mamia ya waendesha bodaboda jana katika uwanja wa Nyamagana jijini hapa, Makamba alisema Serikali ndiye mtetezi wa madereva hao kwa hiyo iko tayari kuchukua hatua za kisheria dhidi ya askari yeyote anayewanyanyasa. “Haiwezekani waendesha pikipiki kunyanyaswa kwani kazi yao inatambuliwa na Serikali na ipo kisheria, ila ninachoomba ni kuzingatia sheria za usalama barabarani,”
alisema Makamba.

Hata hivyo, alikiri kuwapo baadhi ya waendesha pikipiki wahalifu waliojificha katika kazi hiyo na kuendeleza
vitendo viovu ikiwamo unyang’anyi wa fedha kwa abiria na kadhalika.

Alitoa mwito kwa waendesha pikipiki kuepuka ajali za mara kwa mara ambazo zimepoteza maisha yao na ya abiria wao.

Makamba alisema kwa sababu maisha ni kitu muhimu, waendesha bodaboda wanapaswa kujiunga na bima ya
maisha kwani vyombo wanavyoendesha tayari vina bima na kuhoji kwa nini wao wasiwe na bima ya maisha.

Kwa kuanzia alilipia bima ya maisha waendesha pikipiki 100 walioshinda bahati nasibu iliyochezeshwa papo
hapo na alilipa jumla ya Sh 500,000.

Kwa kukatiwa bima hiyo, mwendesha bodaboda atakayepata kilema cha maisha kutokana na ajali atalipwa Sh
milioni 10 na akipata ulemavu wa muda mfupi, kila aliyepata ajali atalipwa kulingana na kiasi alichochanga.

Aliwashauri kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa ili waweke akiba na kujiwekea bima ya afya na akiba ya uzeeni kwani si kila siku watakuwa wanaendesha pikipiki.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Everist Ndikilo alisema suala la akiba uzeeni ni jambo muhimu kwao sawa na la
kuzingatia usalama. Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Dotto Mdoe alisema Polisi
itafanya uchunguzi kubaini wanaojihusisha na unyanyasaji wa waendesha pikipiki na kuchukua hatua.

Hayo yalifikiwa baada ya risala ya Umoja wa Waendesha Pikipiki (UWP) Mwanza iliyosomwa na Katibu Mtendaji wake, Abubakar Juma kuwa waendesha bodaboda wananyanyaswa na Polisi.source; Habari Leo
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
Kuna NINI BODABODA? Viongozi wetu wa CCM wote wanakimbilia huko? Ni Aibu kwa kuuza VIWANDA VYOTE VYA SERIKALI VILIYOKUWA LABOR INTENSIVE???

Sasa Kila KIJANA asiye na ajira anapewa hiyo BODABODA barabara tunazo?
 
ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
Kusaka Urais kwa fedha za Wafadhili plus sehemu ya kodi za makampuni ya Simu kunamtia jeuri Makamba Jr...
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Ndio kampeni za kuelekea 2015 zimeanza rasmi boda boda boda blah blah blah badala ya kuzungumzia kupanda kwa umeme, kuanguka kwa elimu, kupanda kwa gharama za maisha, mishahara midogo n.k.

Kuna NINI BODABODA? Viongozi wetu wa CCM wote wanakimbilia huko? Ni Aibu kwa kuuza VIWANDA VYOTE VYA SERIKALI VILIYOKUWA LABOR INTENSIVE???

Sasa Kila KIJANA asiye na ajira anapewa hiyo BODABODA barabara tunazo?
 
Abdulhalim

Platinum Member
Jul 20, 2007
17,120
2,000
Kuna NINI BODABODA? Viongozi wetu wa CCM wote wanakimbilia huko? Ni Aibu kwa kuuza VIWANDA VYOTE VYA SERIKALI VILIYOKUWA LABOR INTENSIVE???

Sasa Kila KIJANA asiye na ajira anapewa hiyo BODABODA barabara tunazo?

FYI, huyo ni waziri wa technology! nikikumbuka uzi flani hapa wa mwaka 2010 ya wapambe wa marope na hivi vituko vya sasa, I can only repeat my favorite quote: "Nchi hii imelaaniwa kwa kuchagua wapumbavu watuongoze!"
 
manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
3,536
2,000
Nchi hii limekuwa Shamba la bibi au kichwa cha mwenda wazimu kila mtu anajifunzia kunyoa hapo kupitia umasikini tuliotengenezewa ili tutawaliwe kiulaiiiini kabisa.
 
KOMBAJR

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
5,829
1,195

Imeandikwa tarehe 28 Desemba 2013 By Mwandishi Wetu, MwanzaNAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema Serikali haitavumilia baadhi ya askari Polisi wanaonyanyasa waendesha pikipiki za ‘bodaboda’. Akihutubia mamia ya waendesha bodaboda jana katika uwanja wa Nyamagana jijini hapa, Makamba alisema Serikali ndiye mtetezi wa madereva hao kwa hiyo iko tayari kuchukua hatua za kisheria dhidi ya askari yeyote anayewanyanyasa. “Haiwezekani waendesha pikipiki kunyanyaswa kwani kazi yao inatambuliwa na Serikali na ipo kisheria, ila ninachoomba ni kuzingatia sheria za usalama barabarani,”
alisema Makamba.

Hata hivyo, alikiri kuwapo baadhi ya waendesha pikipiki wahalifu waliojificha katika kazi hiyo na kuendeleza
vitendo viovu ikiwamo unyang’anyi wa fedha kwa abiria na kadhalika.

Alitoa mwito kwa waendesha pikipiki kuepuka ajali za mara kwa mara ambazo zimepoteza maisha yao na ya abiria wao.

Makamba alisema kwa sababu maisha ni kitu muhimu, waendesha bodaboda wanapaswa kujiunga na bima ya
maisha kwani vyombo wanavyoendesha tayari vina bima na kuhoji kwa nini wao wasiwe na bima ya maisha.

Kwa kuanzia alilipia bima ya maisha waendesha pikipiki 100 walioshinda bahati nasibu iliyochezeshwa papo
hapo na alilipa jumla ya Sh 500,000.

Kwa kukatiwa bima hiyo, mwendesha bodaboda atakayepata kilema cha maisha kutokana na ajali atalipwa Sh
milioni 10 na akipata ulemavu wa muda mfupi, kila aliyepata ajali atalipwa kulingana na kiasi alichochanga.

Aliwashauri kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa ili waweke akiba na kujiwekea bima ya afya na akiba ya uzeeni kwani si kila siku watakuwa wanaendesha pikipiki.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Everist Ndikilo alisema suala la akiba uzeeni ni jambo muhimu kwao sawa na la
kuzingatia usalama. Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Dotto Mdoe alisema Polisi
itafanya uchunguzi kubaini wanaojihusisha na unyanyasaji wa waendesha pikipiki na kuchukua hatua.

Hayo yalifikiwa baada ya risala ya Umoja wa Waendesha Pikipiki (UWP) Mwanza iliyosomwa na Katibu Mtendaji wake, Abubakar Juma kuwa waendesha bodaboda wananyanyaswa na Polisi.source; Habari Leo

Baada ya viongozi wa dini next move ilikuwa ni bodaboda. Urais huu utawatoa macho.
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,230
2,000
baada ya kikwete kuongoza kila mtu anahisi anaweza kuongoza hata akihamia uwanja wa ndege kama rubani...january, aliupata ubunge kwa kazi ya ziada ya dada yake ushahidi uliwekwa humu kuwa dada mtu ilibidi achojoe nguo kupata bil 1 ya kampeni, kama ubunge dada aliokoa jahazu kwa namna hiyo urais itakuwaje au anadhani maaskofu ni wapumbavu anaweza kuwa danganya kijinga hivyo kwa kuwapa 50000 na chakula..
 
Njaa Mbaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2012
666
250
Kama huyu jamaa nae anafikiria kuwa rais basi kazi hii sasa aina tofauti na kunywa gongo hata watu wa hovyo kabisa nao utasikia wanataka urais kweli kikwete ameifanya hii kazi kuonekana ya hovyo
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
13,389
2,000
Hivi ni kweli anautaka uraisi? Mungu wangu! Kiama! Eh? hana hata aibu? Kwa lipi? Shame upon CCM! Mmekosa watu kabisa hadi mmeamua kutuletea hawa?
 
theROOM

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
946
250
Duh, yaani hadi mimi nnaona aibu. Kwamba hadi January anautaka Urais? Hii kazi ya URAIS inaonekana ni rahisi sana...
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
18,482
2,000

Imeandikwa tarehe 28 Desemba 2013 By Mwandishi Wetu, MwanzaNAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema Serikali haitavumilia baadhi ya askari Polisi wanaonyanyasa waendesha pikipiki za ‘bodaboda’. Akihutubia mamia ya waendesha bodaboda jana katika uwanja wa Nyamagana jijini hapa, Makamba alisema Serikali ndiye mtetezi wa madereva hao kwa hiyo iko tayari kuchukua hatua za kisheria dhidi ya askari yeyote anayewanyanyasa. “Haiwezekani waendesha pikipiki kunyanyaswa kwani kazi yao inatambuliwa na Serikali na ipo kisheria, ila ninachoomba ni kuzingatia sheria za usalama barabarani,”
alisema Makamba.

Hata hivyo, alikiri kuwapo baadhi ya waendesha pikipiki wahalifu waliojificha katika kazi hiyo na kuendeleza
vitendo viovu ikiwamo unyang’anyi wa fedha kwa abiria na kadhalika.

Alitoa mwito kwa waendesha pikipiki kuepuka ajali za mara kwa mara ambazo zimepoteza maisha yao na ya abiria wao.

Makamba alisema kwa sababu maisha ni kitu muhimu, waendesha bodaboda wanapaswa kujiunga na bima ya
maisha kwani vyombo wanavyoendesha tayari vina bima na kuhoji kwa nini wao wasiwe na bima ya maisha.

Kwa kuanzia alilipia bima ya maisha waendesha pikipiki 100 walioshinda bahati nasibu iliyochezeshwa papo
hapo na alilipa jumla ya Sh 500,000.

Kwa kukatiwa bima hiyo, mwendesha bodaboda atakayepata kilema cha maisha kutokana na ajali atalipwa Sh
milioni 10 na akipata ulemavu wa muda mfupi, kila aliyepata ajali atalipwa kulingana na kiasi alichochanga.

Aliwashauri kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa ili waweke akiba na kujiwekea bima ya afya na akiba ya uzeeni kwani si kila siku watakuwa wanaendesha pikipiki.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Everist Ndikilo alisema suala la akiba uzeeni ni jambo muhimu kwao sawa na la
kuzingatia usalama. Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Dotto Mdoe alisema Polisi
itafanya uchunguzi kubaini wanaojihusisha na unyanyasaji wa waendesha pikipiki na kuchukua hatua.

Hayo yalifikiwa baada ya risala ya Umoja wa Waendesha Pikipiki (UWP) Mwanza iliyosomwa na Katibu Mtendaji wake, Abubakar Juma kuwa waendesha bodaboda wananyanyaswa na Polisi.source; Habari Leo
Makamba ame out source majukumu yake?

Inakuwaje Makamba anatumia muda mwingi kufanya mambo yasiyo husiana moja kwa moja na wizara yake?

1. Hivi karibuni tumesikia kawakusanya wakulima Songea kuzungumzia changamoto zao

2. Juzi twaambiwa aliwaketisha makasisi

3. Leo kahamia kwa bodaboda ambako pia hakuhusiani na job description yake

Huyu si miongoni mwa mawaziri mizigo? maana haijulikani ni nani anafanya kazi zake ofisini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom