Bodaboda ingekuwa ajira CCM ingeiweka kwenye ilani yake

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Wadau nawasabahi,

Nawashangaa sana wanaompinga Lema alivyosema kazi ya bodaboda ni laana. Ukweli lazima usemwe, kazi ya bodaboda ingekuwa ni kazi sahihi naamini CCM ingeweka katika ilani yake ili mwisho wa siku wakati wa uchaguzi waendesha bodaboda waipigie kura CCM.

Hebu jiulize kwanini CCM haijawahi kusema imeandaa ajira milioni 5 za bodaboda? Ni dhahiri hata CCM inajua sio ajira ndio maana inawacha vijana wahangaike wenyewe kutafuta pikipiki za kukodi au mikataba.

Bw. Lema aliposema ni kazi ya laana, ni kutokana na matukio wanayopitia waendesha bodaboda. Matukio kama ajali. Ujambazi kubeba wake za watu, uporaji na ulawiti kwa abiria watoto na wanafunzi. Vitendo hivyo ndio laana yenyewe aliyoisemea Bw. Lema.
 
Ngoja hao chawa,papasi na kunguni wavamie mada.
Wanajiganya kumnanga Lema. Kama bodaboda wanaona ninzuri na salama basi waache ma V-8 yao watumie bodaboda
Hilo litaacha jamii iamini kama usafiri huo nisalama
Pili itachangia kuwaongezea waendesha bodaboda kipato maana misafara ya viongozi inajumuisha watu wengi
 
Back
Top Bottom