Makamba ataka mwanae amrithi Shelukindo...

Mkuu,

kisukuma ni kibantu... au sio?

Kisukuma ni lugha iliyotoka kwenye lugha iliyokuwa inaitwa Kibantu.

Neno lolote lile la Kibantu, kama vile Mwanawane, mzizi wake ni Kibantu, sio Kisukuma, au Kihaya au Kifipa.

Wafipa, kwa mfano, asili ya lugha yao ni Kibantu. Kama Wasukuma. Lakini Kifipa sio sawa na Kibantu, na Kisukuma sio sawa na Kibantu, ndio maana Mfipa na Msukuma hawazungumzi lugha moja.

Mwanawane asili yake ni Kibantu.
 
na sie tusiokuwa na watu wa kuwatanguliza majimboni tuna chetu kweli huko? hii hatari sana kwa demokrasia hapa tzania
 
January ana creditials zote kuwa Mbunge, kama ni kweli litakuwa na wazo la mbolea sana. I can see this young man ana excel katika nyadhifa za juu huko mbeleni.

Tatizo watu wana mhukumu January kwa kuangalia utendaji wa baba yake badala ya kumuangalia January kama January, the guy is very intelligent and the future is bright for him.

Hawa ndio calibre ya vijana tunao wataka kule mjengoni go January...

Haya ndiyo mambo mimi kila siku nayakataa kumsifia mtu pasipo kutueleza kawafanyia nini watz achilia mbali wana Bumbuli hadi tumchague/wamchague!

Tufikie hatua tumpe mtu credits kwa kile alichofanya sio tu kwa sababu anaonekana kila siku akihutubia kwenye blog ya michuzi!

Janaury na wenzake ni kama hawa wengine wengi ndani ya CCM,hamna lolote la maana kwenye ubunifu ambalo anaweza akatueleza kuwa kaisha wafanyia wana Bumbuli;sasa hii ya kumsifia kweli kweli kama anafaa kuwa hata Mbunge wa BUMBULI kwa vigezo vipi?

Uwizi mtupu!!,kama tunampigia debe achaguliwe tumpigie tu sio kuingiza sifa ambazo hana!
 
Mkuu Buricheka,

Hata kama Kelly ana mahusiano na JM, je kuna kosa lolote kwa yeye kutoa maoni yake hapa? Ni vizuri kuongea utendaji wa JM lakini pia sioni kama ni vibaya kwa mtu anayemfahamu vizuri JM (kwa mfano - rafiki yake) kutoa maoni yake kumhusu.

Kosa ni kwamba, unapoanza kumuongelea mtu yeyote yule mbele za watu, kutoa uchambuzi wa kazi yake au tabia yake, kama una uhusiano nae wowote ule, mapenzi, ushemeji, urafiki, sema mapema!

Sema mapema.

Inaitwa fair disclosure.

Ili tusije kugundua baadae kwamba kumbe Kelly01 ana uhusiano wa kirafiki na January ndo maana anamfagilia.

Anapalilia mlo?

Sasa leo Kelly01 atatutajia, January Makamba amefanya nini kizuri kazini. Aseme kimoja!
 
kwa hiyo sie ambao hatuna watu wa kuwatanguliza majimboni ndio hatuna chetu?
 
Yanatoka kwenye Kibantu, sio Kisukuma.

Ukirekebisha mtu na maneno makali maKali kama "FOR YOUR INFORMATION", angalau basi jua unachokiongelea.

What are you talking about?nini ukali wa FYI?umesikia tone(sauti) niliotumia?can tone of voice be heard through written communications?au umeweka assumption tu kwamba nimejibu kiukali?maelezo tafadhali?
 
Muulize yeye ambaye yuko big on "kujua unachoongelea" mwanawane maana yake nini?
 
Taji Liundi na Mwamvita Makamba wameowana ama ni mikasi tu!

Huyu eti ndiye ana IQ kubwa JF; hawezi kujua hata hapa watu wanaongelea siasa wala sio wanayofanya watu wazima wakiwa pekee ndani ya vyumba vyao.

Wazee wa Ze Comedy hawa; kuvamia kila topic.
 
kwa hiyo sie ambao hatuna watu wa kuwatanguliza majimboni ndio hatuna chetu?

sisi tusio na wazee wa kutupelekea posa za siasa ndio wenye nafasi kubwa ya kushinda kwakuwa tutakwenda wenyewe na huo ndio ujasiri tulionao ambao utatuongezea credit siku hiyo ya kwenda wenyewe na kusimama kwa miguu yetu miwili na kujieleza,wenzetu watakuwa wapya huko wakati sisi tutakuwa tumeshasikika kabla ya hapo,unajua hii baba kuaza kukupigia ndogondogo ni dalili ya uoga ambayo sio sifa nzuri kwa mtu ambaye anataraji kuongoza watu,sasa anataka kuwaongoza watu ambao hata kuwa-face na kuwaeleza nia yake anaogopa?
 
Waache demokrasia ichukue mkondo wake mi nashangaa wabunge wanao sema wanachezewa rafu wanataka wawe wabunge milele?

Hauelewi mada. Tatiz si kutopata mpinzani bali ni taratibu zifuatwe za muda wa kampeni. Pia makamba kutumia influence yake kumweka mwanae wewe huoni ni tatizo. Ila eande tu aone atakvyogalagazwa kwa aibu
 
Kwa mzee Makamba hii ndiyo staili yake ya kuomba kazi. Hata ajira aliyonayo huyo kijna kwa sasa ni Makamba mwenyewe alimwombea kwa mkuu wa kaya, Yeye mwenyewe pia alivyomwomba JK asimtose kwani bado ana nguvu ya kufanya kazi.
 
Sasa si baba ake kaenda kuongea nao kwanza? We hauoni hata maofisini kabla mtu hajaenda kuonana na mabosi wenyewe kuna kuwa na mtu ana tambus=lisha kabisa kuwa mtu fulani ana kuja na ana nia hii naomba mumsaidie?

That is a wrong approach. Ina maana atakuwa anatawala kwa kuongozwa na baba yake
 
That is a wrong approach. Ina maana atakuwa anatawala kwa kuongozwa na baba yake

Ndo maanake , iwapo baba anampigia debe sasa huyo si anaongozwa na baba ake na kama ni kweli basi kuna kitu ambacho huyo babaake ana interest nacho ktk hili jimbo..........
 
January ana creditials zote kuwa Mbunge, kama ni kweli litakuwa na wazo la mbolea sana. I can see this young man ana excel katika nyadhifa za juu huko mbeleni.

Tatizo watu wana mhukumu January kwa kuangalia utendaji wa baba yake badala ya kumuangalia January kama January, the guy is very intelligent and the future is bright for him.

Hawa ndio calibre ya vijana tunao wataka kule mjengoni go January...

Creditials zipi mkuu tutajie chache na kashawahi kufanya nini kututhibitishia maneno yako? Nafasi aliyonayo ikulu hata wewe ungekuwa nayo kama baba yako angekuwa katibu mkuu wa ccm, yaani kapelekwa. Angekuwa ni mtu kaanza na kupanda taratibu tungesema sawa ila data zake hakuna. Itakuwa ndio hao hao kina nchimbi, masha, mongela mkuu wa wilaya, ridhwani na nk
 
Ndo maanake , iwapo baba anampigia debe sasa huyo si anaongozwa na baba ake na kama ni kweli basi kuna kitu ambacho huyo babaake ana interest nacho ktk hili jimbo..........

Interest kubwa ni kumuondoa mpiganaji Shelu huko. Hii ni kama yale ya bashe na selelii au mwakalinga na mwakyembe. Hayo ni mapandikizi ya ufisadi
 
Creditials zipi mkuu tutajie chache na kashawahi kufanya nini kututhibitishia maneno yako? Nafasi aliyonayo ikulu hata wewe ungekuwa nayo kama baba yako angekuwa katibu mkuu wa ccm, yaani kapelekwa. Angekuwa ni mtu kaanza na kupanda taratibu tungesema sawa ila data zake hakuna. Itakuwa ndio hao hao kina nchimbi, masha, mongela mkuu wa wilaya, ridhwani na nk

Performance yake katika kazi yake ya sasa kwa mujibuwa walio karibu nae jamaa ndio injini pale.

Swali jingine..
 
kwa harakaharaka huyu kijana sio kiongozi na maana hiyo hafai kuwa kiongozi,baba yako ataendaje kukupigia debe?si utaongoza kama anavyotaka yeye?hata alikoajiriwa sasa ni baba yake huyo hyuyo kampigia debe, sasa tz hatutaki viongozi wakubebana,fanya kazi upate uongozi kama unaona unakufaa,wana Lushoto tafadhali sana mwogopeni mtu huyu hata akiletwa na mbwembwe gani, hali kadhalika na majimbo yoote tanzania hii,tusipoteze kumpigia mtu kura kisa mtoto wa fulani,at the end of the day tunaumia wenyewe.tuwapitishe na kuwachagua kutokana na kuwafahamu utndaji from the scratch si kuambiw au kushinikizwa!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom