Mzee makamba, shekifu kusimikwa ukamanda leo mkoa wa Tanga.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee makamba, shekifu kusimikwa ukamanda leo mkoa wa Tanga..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MtazamoWangu, Mar 30, 2010.

 1. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Leo CCM itawasimika makamanda wake wa mkoa wa tanga katika mkutano utakaofanyika Mombo, Tanga.

  Wanaotarajiwa kusimikwa ni:

  Mzee makamba (katibu mkuu wa ccm): Kamanda wa mkoa wa Tanga, Mh. Shekifu (mkuu wa mkoa wa Manyara): Kamanda wa wilaya ya Lushoto.

  Wengine watakaosimikwa ni pamoja na makamanda wa kata zote za wilaya ya Lushoto.....

  Wakati hli likiendelea taarifa zilizopo ni kwamba mh. Henry shekifu ametangaza nia ya kurudi tena kugombea ubunge jimbo la lushoto, na hata juzi kwenye mkutano wa wilaya ya lushoto katika baraza la vijana akiwa kama mgeni rasmi alitoa zawadi kwadhaa kwa kata zote za wilaya ya lushoto ikiwa ni mipira na jezi lakini akiwatumia vijana wa arusha na manyara kuwakilisha kwa kudai eti vijana wa arusha na manyara wamewaletea zawadi vijana wenzao wa lushoto.....na hata alipopewa nafasi ya kuongea, alijipamba kwa mazuri aliyowahi kufanya na kusaidia wananchi wa lushoto tu na kusahau kuongelea lilompeleka pale kama kamanda wa vijana....

  Kusimikwa kwake kwa kipindi cha tatu mfululizo kinampa sasa nafasi ya kufanya shughuli zake ndani ya jimbo ikiwa ni pamoja na kutoa misaada kwa tiketi ya ulezi wa vijana.....mh shekifu ni kweli anakubalika bado lushoto lakini gear ccm inazotumia zinawanyonga viongozi wengine...

  Kwa upande wa mzee makamba...kijana wake january makamba ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la bumbuli ndani ya wilaya ya lushoto...na mzee makamba amewaagiza viongozi wa wilaya wahakikishe january ndio mbunge wa bumbuli kwa gharama zote, na hata kanuni zimekuwa zikivunjwa katika kulitimiza hili agizo, mzee makamba anataka kwa gharama zozote zile mh.shelukindo ang'olewe na mwanae....aliwahi kusema kama ukigombana na mtu akikushinda basi unaweza ukawatuma na wanao wakampige...kwani makamba alishawahi kushindwa na shelukindo katika uchaguzi....

  Matusi, ugomvi na kashfa ndio zilizojaa kwenye jimbo la bumbuli....viongozi wa ccm wanalazimisha sio kuomba january awe mbunge, na wale wote wanaompinga wananyanyaswa kwa vitisho;

  1. Makatibu kata kadhaa wamepewa onyo baada ya nia ya kuwafukuza kazi kushindikana baada ya kuonekana hawatoi ushirikiano kwenye kampeni za january ambazo zimeanza toka mwaka jana kinyume na kanuni za CCM.

  2. Makamanda wa kata waliokuwa wameteuliwa na kamati za siasa za kata na kuonekana hawamuungi mkono january pamoja na muhtasi wa uteuzi wao na barua zao kutumwa wamejikuta wakikatwa majina yao dakika za mwisho na viongozi wa ccm vijana.

  3. Mwenyekiti wa ccm vijana (bwana mahanyu) ndio mpiga debe mkuu wa january na amekuwa akiwanyanyasa viongozi wanaoonekana na msimamo toafuti na wa kumuunga mkono january.

  4. Viongozi wa ccm wilaya nao wameonekana kubuluzwa na mzee makamba kwani mzee shelukindo alifikisha malalamiko yake juu za kuvunjwa kwa kanuni za ccm na bwana january lakini hakujibiwa, lakini barua ya kumchafua mzee shelukindo iliyoandaliwa na january na mahanyu na kusainiwa na Leonard Kaoneka ilifikishwa mpaka mkoani na mzee shelukindo kuitwa mbele ya kamati ya siasa na kutishiwa kupelekwa maadili....Bwana Kaoneka alithibitisha kwamba barua ile hakuandika yeye ila aliitwa tu a-sign.

  Kwahiyo sasa mzee Makamba anapewa fimbo nyingine ya kupigia japo hapendwi sana jimboni Bumbuli kwani alishawahi kufukuzwa alipoenda kumuuza kijana wake.

  Je huu ukanda si kweli unahusiana na dalili za kubebana kwenye kinyang'anyiro??? Tazama wote uliowasikia hivi karibuni wanapewa ukamanda......
   
 2. d

  damn JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hawa makamanda kazi zao ni zipi, au ndiyo style ya mafisadi kujificha?
   
 3. O

  Omumura JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tutasikia mengi sana mwaka huu, ni kweli makamba amejiandaa haswa ili Januari amwangushe shelukindo,kwa hali ilivo wapo watu kule bumbuli watatoana roho kwaajili ya vita ya makamba na shelukindo.
   
 4. p

  paison Member

  #4
  Apr 1, 2010
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hata mimi wana nchanganya!hivi ukamanda ni kwa mwanachama yoyote au kuna hatua fulani m/ccm anatakiwa kupitia?

  Paison
   
 5. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Henry Shekifu ni another mwizi aliyebobea ama aliyekomaa. Huyu alishawekwa ndani na Mwalimu Nyerere kwa ajili ya Ulanguzi na wizi wa mali za umma. Leo anakuwa Mh na kamanda wa vijana, sasa atawafundisha nini vijana kama si wizi na uhalifu?.
   
Loading...