Makamba ashindwa kumjibu mama Kilango

Sonara

JF-Expert Member
Oct 2, 2008
726
68
YUOSUF Makamba (TARIK AZIZI)ashindwa kujibu kauli ya mama ANNE KILANGO aliyoitowa hivi karibuni kuhusiana na Mafisadi ndani ya CCM
 
Sonara
Makamba anajua nani gangwe ndani ya chama.
Kwa taarifa yako mama Anne kilango ni mtego mwingine ambao jamii itauvaa mkenge. Nauliza ameongoka lini huyu mama? alikuwa waziri ktk kabinet ya mkapa na sijui kuna nini alifanya mpaka sasa. pia ninachunga na kuunganisha sana dots ktk kauli zake hasa bungeni. kuna orcle imejificha ktk utanashati wake. Anasema sana ila kuna vitu halisi vinamiss ktk kauli zake. kuna missinformations nyingi sana anazopenyeza kupitia speeches zake. Jiulize kwa nini akapewa na wamarekani ile zawadi ya mwanamwali wa shoka kwa nini asipewe TIBAIJUKA au marehemu Chifupa mabaye alitoa hata maisha yake kutumikia UMMA?
Nyie nyie kumbukeni kuna mti unaitwa MKENGE na huwa unaota pembezoni mwa njia. chunga sana baada ya kuchunguza.
 
.............................................................................................
....."Kwa taarifa yako mama Anne kilango ni mtego mwingine ambao jamii itauvaa mkenge". ............

Ni kweli msanii, ila hapo sijakuelewa kabisaa! je anatuhadaa tumuone yeye ni 100% au?
 
Msanii uko sawa..

huyu mama hana lolote uropokaji tuuu na hata wamarekani ni mtego wamemtumia ili aropoke zaidi wapate wanachotaka...hakustahili uhalisia na maana ya hiyo tuzo ila kwa kuwa ni MKENGE wamempaa...mnawajua vema americans kwa politiks zao za kugawa na kusogea then kugeuka (no permanent friends, only permanent interest!!!)

CCM wenyewe wanamsikilizia tuuu ikifika wanamtosaaa kuleeee...
 
Anne Kilango WAZIRI - Mkapa's cabinet???????
toka lini????? Check your facts mkuu.Huyu hajawahi kuwa hata Mkuu wa wilaya.. alipewa ubunge wa kuteuliwa tu na hakupewa uwaziri.
 
Wazee mnapindisha hoja, Anne Kilango anashutumiwa kwa lipi?..... ukiwasikiliza hao wawili Anne Kilango na Makamba, utagundua kuwa mzee wetu Makamba ameachwa mbali mno kiupeo na kiujengaji hoja. Pia Pia Mzee Mkamba ni mmoja kati ya wana CCM wanaotetea mafisadi, ilhali mama Kilango watanzania wengi wakweli wanamuona ni mwiba mkali kwa mafisadi tena na ile tuzo na kupongezwa na JK.....kumefanya watu aina ya mzee Makamba waanze kumuogopa.
 
Anne Kilango WAZIRI - Mkapa's cabinet???????
toka lini????? Check your facts mkuu.Huyu hajawahi kuwa hata Mkuu wa wilaya.. alipewa ubunge wa kuteuliwa tu na hakupewa uwaziri.

unajua niliongea kwa hasira sana pale hata data muhimu zikawa zinaniponyoka.
ila ukiondoa hiyo kasoro mengine niliyoyasema yanabaki vilevile kuwa huu ni mtego mwingine mchangani.
 
unajua niliongea kwa hasira sana pale hata data muhimu zikawa zinaniponyoka.
ila ukiondoa hiyo kasoro mengine niliyoyasema yanabaki vilevile kuwa huu ni mtego mwingine mchangani.
Msaani bana!
Pole lakini. Usi-personalise matatizo ya nchi yetu utapata presha bureee.
 
Changia hoja bana acha blah blah ..Sisi tulichokuwa tinasubiria ni hii kauli ya Comical Ali wetu amwage hiyo anayoona ni hoja kumjibu Kilango..thats it! Matokeo yake tunaona tu kimyaaaa..Hayo mambo ya tuzo yatafutie thread mkuu...
 
Mimi sioni tatizo kama 'anaropoka' vitu vinavyo-make sense na hamwogopi mtu kufanya hivyo. Angalau amejitahidi kusema kile anachotaka kusema bila woga ukimlinganisha na wanasiasa wengine ndani ya sisiem. Nadhani ile tuzo alyopewa anastahili na hata sisiem wenyewe wanalijua hili (at least mwenyekiti wao amempongeza hadharani tena mara mbili!).

Labda mtuambie hayo mabaya aliyoyasema ('ropoka') ambayo wengine hatuyaoni.
 
hakuna kitu pale. yule ni anaandaliwa kuwa MZINDAKAYA wa zama hizi.
Na kwa kuwa uchaguzi ndo huu basi INDOOR PLUMBING ndo imeshika kasi
 
Ukweli utasimama kama ukweli. Kukubali au kutokukubali ni lako binafsi. Huyu mama mimi ninamuona kama mfano bora katika utetezi wa maslahi ya nchi.
 
Samahani mkuu, naweka kumbukumbu sawa; Kilango hajawahi kuwa Waziri kwenye awamu yoyote ya utawala wa nchi hii.
 
Changia hoja bana acha blah blah ..Sisi tulichokuwa tinasubiria ni hii kauli ya Comical Ali wetu amwage hiyo anayoona ni hoja kumjibu Kilango..thats it! Matokeo yake tunaona tu kimyaaaa..Hayo mambo ya tuzo yatafutie thread mkuu...

...Imeandikwa mahala fulani kwamba shetani anaweza kuja kama malaika wa nuru hata watumishi wake wakaja kama watumishi wa haki.... upo hapo?
 
unajua niliongea kwa hasira sana pale hata data muhimu zikawa zinaniponyoka.
ila ukiondoa hiyo kasoro mengine niliyoyasema yanabaki vilevile kuwa huu ni mtego mwingine mchangani.
Ila umejua kujichagulia jina! Maana ni Msanii kweli kweli! Hata hivyo, hongera kwa kukiri kosa. Umeonesha ukomavu.
WoS asante kwa marekebisho, vinginevyo lilishakuwa goli.
I like JF!
 
Ila umejua kujichagulia jina! Maana ni Msanii kweli kweli! Hata hivyo, hongera kwa kukiri kosa. Umeonesha ukomavu.
WoS asante kwa marekebisho, vinginevyo lilishakuwa goli.
I like JF!

..hapo nilipobold nimekuwa curious kufehem ina maana gani??
ninatoa maoni tu wala sipo ktk kuwadunga magoli wanaJF wenzangu. nachangia kwa kuwa nakerwa na ukereketwa wangu juu ya nchi yangu. Naipenda sana ila muda mwingi nalazimishwa kuichukia kutokana na tabia MBAYA zsizo za kimaadili za viongozi.
BTW nashukuru kwa kukubali masahihisho yangu ya waraka wa awali. tusonge mbele tukate kiu ops tukate ishu
 
..Naipenda sana ila muda mwingi nalazimishwa kuichukia kutokana na tabia MBAYA zsizo za kimaadili za viongozi.
Usiichukie nchi yako Mkuu!
SWALI:wazazi wakawa wabaya hawajali, wanajipenda wao tu, nyumbani kukawa kubaya hakuvutii kama kwa jirani , utahamia kwa jirani?
 
Sisi wtz tuna macho, tunaufahamu wetu wa kuweza kupembua mambo bila hata ya kusubiri wa-marekani wamzawadie mama Anna. Waliofuatilia mwenendo wa uchangia hoja kwenye mjadala uliohusu ufisadi mwenye akili zake aliweza kuona nani kachangia nini kuhusu ufisadi. Sasa mnapotuambia eti Anna kilangho ni mropokaji, tueleze nani alikukuna zaidi yake? alichoropoka ambacho hakikuwepo ni kipi? Angalia usiropoke wewe badala yake.
 
Usiichukie nchi yako Mkuu!
SWALI:wazazi wakawa wabaya hawajali, wanajipenda wao tu, nyumbani kukawa kubaya hakuvutii kama kwa jirani , utahamia kwa jirani?

...nitahamia kwangu nikikua.
ila huu si mfano wa kutosheleza mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…