Mzee Mafuchila,
Heshima yako mkuu, na wazee wote wa forum, Hiii habari ni kweli kama ulivyosema sio habari ndogo ni nzito sana kuliko ilivyopokelewa na public kwa ujumla, maana behind it kuna moto unawaka, kama nilivyosema siku chache zilizopita kuwa Mzee JK anajitayarisha kwa kitu kizito behind kuwafuta wajumbe wote wa kamati ya maadili ya CCM, ambayo huyu Mzee Sozigwa alikuwa ni mmoja wao,
INSIDE INFO (Kama ninavyoifahamu):
(1). Ni kwamba moja kati ya makubaliano between Mtandao na BM katika kumpitisha mgombea wao, ilikuwa ni pamoja na kumkabidhi mgombea wao huyo mafaili yote ya maadili yaliyotayarishwa na Mzee Mang'ula, kwa ajili ya wagombea urais wa CCM, na kweli akapewa,
(2). Mafaili mawili kati ya yote ndiyo yaliyokuwa "Mabaya" nayo ni ya JK na JM, na baada ya kuyaona kwa macho yangu, kwanza nimemdharau Mang'ula kumbe the man was a fraud na fake, sivyo kama nilivyokuwa ninamchukulia katika kipindi chake chote cha uongozi, na sio accident kuwa sasa the man is jobless. Baada ya kuyasoma hayo maneno ndio nimegundua kuwa Watanzania tutaendelea kufanyiana fitina na majungu mpaka mwisho wa dunia wakati hatuna jawabu la matatizo yetu, kimaisha, isipokuwa inapokuja kwenye majungu na fitina we are very creative,
(3). Ukweli ni kwamba Mang'ula alifikiri kuwa ili apate nafasi ya kugombea urais yeye mwenyewe, dawa ilikuwa ni kuwapikia majungu wenziwe, na kwamba huenda by luck CCM itaamua kuwa wagombea wote hawafai, na kumuomba yeye Mang'ula, awe mgombea wao, kwa kuitumia kamati ya maadili ya akina Sozigwa, kwa bahati Mtandao walishagundua hivyo wakambana BM, amkataze kuchukua fomu ambayo tayari alikuwa ameichukua kinyemela, na akairudisha kimya kimya,
(4). Katika siku za karibuni, Mzee JK aliamua kuwa wakati umefika wa kuitosa kamati nzima ya maadili, na makatibu wa CCM wa mikoa na wilaya lakini Mzee mmoja wa CCM akamuwahi na kumuomba kwamba awaache makatibu kwa sababu ni hao hao ndio watakao gombea upande wa upinzani, lakini maadili ni ok, sasa kati yaa maadili waliotoswa huyu mzee ni mmoja wao, Halafu sio siri kuwa Mzee JK, ana mpango wa kuwashughulikia viongozi wezi huko mbele ya safari na itaanzia hapa kwenye maadili,
Maoni yangu ni kwamba, Mzee Sozigwa I like your maneno, lakini tatizo ni kwamba yametolewa baada ya kuondolewa hivyo kuifanya hii message iwe suspect, kwa nini usiseme toka siku nyingi au CCM ndio kwanza imeingiwa na wala rushwa? Halafu Mzee kama Sozigwa kusema maneno mazito kama hayo public, ina maana ana ushahidi wa kutosha, hivyo baada ya Makamba kumjibu,
alitakiwa kumwaga ushahidi hadharani, badala ya kuwa kama Kitine kuchokoza na kubana kimya, Mzee Sozigwa has nothing to lose kwa nini asiweke mambo hadharani? Anaogopa kuwa mkono kinywani umekatwa? Ninasema mzee JK kwamba hiyo hatua ya kuwaondoa hao maadili ilikuwa ni nzuri sana maana sasa si unaona watu kama Sozigwa wanasema? Ina maana kisu kimegusa mfupa sasa, kwa hiyo Mzee JK, kwenye silegeze kamba lazima viongozi wezi watinge kwenye sheria hakuna huruma, na kama kuna wanaogopa na wameanza kuwatuma kina Sozigwa kujaribu kuuzima moto, ni lazima wajue kuwa kwenye hili wananchi hatuko na wezi, na kwa Mzee Sozigwa kwa mtu aliyefikia nafasi kama yake kitaifa kwenda kulia public bila kutoa ushahidi kamili ambao nina uhakika kuwa anao, basi ina maana huenda hana ukweli!
Lakini, all in all bado ninampa respect kwa kujikaza na kusema public, sasa ngoja tuone hii issue itaishia wapi,
Hayo ni maoni ynagu tu Wazee!