Makamba aibuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba aibuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by democratic, Feb 27, 2012.

 1. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yule kibabu aliyepata kuwa katibu mkuu wa CCM Luten Yusuf Makamba ameibuka baada ya kimya cha mda mrefu na kuwaasa watanzania waache kufikiri kwamba wanaishi peponi kwa kulalamika kila siku kuwa maisha ni magumu na badala yake wafanye kazi kwa bidii kwani hata huko peponi nako kuna kazi.

  Vilevile amewataka waache kumlalamikia Rais J.M.Kikwete kwamba kashindwa kuyafanya maisha yao kuwa bora,kwani hilo si jukumu la rais Kikwete bali ni jukumu la kila mwananchi kunyanyua maisha yake bila kuitegemea serikali au Rais J.M.Kikwete.Alipoulizwa ni kwa nini wakati wa kampeni rais Kikwete alitoa ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania wakati anafahamu kuwa huo sio wajibu wake.

  Makamba alidai kuwa siasa ni mchezo na kila mchezo una mbinu na hiyo ilikuwa mbinu ya rais kikwete na chama chake ili aweze kuchaguliwa kwani hata ahadi alizokuwa anatoa Dk.Slaa ya mfuko wa cement kuwa 5000/=kwa mfuko haiwezekani bali ni mbinu ya mchezo wa siasa.

  SOURCE;Gazeti la Jambo Leo ukurasa wa 4.

  My take; Mzee umri unamtupa mkono vibaya mno kama kweli haamini kama kazi kubwa aliyonayo rais wa nchi ni kuboresha hali ya maisha ya watu wake.
   
 2. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  hahahahhahhaaaa the spinning pro., aliwakomesha kweli hao waandishi wa habari!
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Hio signature yako imenikumbusha Mheshimiwa mmoja kwenye kitabu fulani hivi....ngoja waje watakusaidia kutaja hivyo vyeo...........
   
 4. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unategemea huyu babu atasema nini tofauti na hicho! yeye ni mmoja wa ma-engineer wa hii hali ngumu tuliyonayo sasa!!
   
 5. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Huyu mzee akili zake ni kama za JK.
  Sasa kama si jukumu la rais kuakikisha kunakuwa na ustawi mzuri wa kimaisha kwa wananchi wake na nchi kwa ujumla, yeye kama rais jukumu lake hasa ni nini?
  Indirectly Makamba anamaanisha, imekula kwenu wa tz, kwani rais hajui kama anajukumu la kuakikisha good living standard kwa wananchi wake.
  Afu kutokujua majukumu yake ndo kunapelekea awe mzurulaji sana...
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hata kama wananchi watafanya kazi usiku na mchana, lakini iwapo sera za kulinda ajira na masoko ya bidhaa zao, sera za uhamiaji, ulinzi na Usalama wa wananchi zikiwa mbovu ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa!...Ujinga Jazz!
   
 7. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kutamka kuwa 'Watanzania waaache kulalamika na kufanya kazi' ni kuwadhalilisha. Je ina maana kuwa Watanzania ni wavivu? Ninaamini kuwa Watanzania ni wachapakazi mno na ndio maana wameweza kustahimili shida zote hizi zinazowakabili kwa miaka yote. Wamelea na kusomesha watoto wao na kujipatia riziki zao kila siku, wamejenga nyumba zao bila mikopo n.k bila msaada wowote.

  Kuna siku nilikuwa nasafiri kwenye ndege kuelekea Ulaya, pembeni yangu alikaa Mmarekani. Katika mazungumzo yetu alibainisha kuwa ilikuwa ni safari yake ya kwanza kuja Tanzania. Nilipomuuliza ni kitu gani ambacho atakikumbuka kuhusu Tanzaniai, akasema kuwa kitu alichoona ni kuwa hajaona watu wanaofanya kazi sana kama Watanzania na wanafanya kazi hizo katika mazingira magumu.

  Mtu anafanya kazi akiwa na malengo fulani. Kama yale malengo yake hayafanikiwi kutokana na juhudi za kazi zake, inabidi akae chini afikirie kwa nini hafanikiwi. Kuendelea kufanya kazi tu bila kutathmini matokeo ya kazi unayofanya si sahihi. Watanzania wanatathmini juhudi zao, kama wanaona hawayafikii malengo yao 'wanalalamika'. Katika hilo kulalamika ni sahihi. Ni mtumwa tu ndie asiyelalamika akifanyishwa kazi. Lakini hata akichapwa mjeledi, kilio chake cha maumivu ni kulalamika.
   
 8. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,464
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Kweli sio jukumu lake! Lingekua jukumu lake angetulia Bongo, ila kwa sababu haimhusu, mwache aendee kuruka Nchi za watu. Makamba upo sahihi kabisa! Endelea kupiga mbiu.
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Kweli wewe ni MD, MPH, MBA?...........
   
 10. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Atueleze bintie pesa alozonunulia lile jumba kama ni za ajira au ujasiriamali.
   
 11. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Kawakomeshaje?
   
 12. t

  taranda Member

  #12
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alaf kama kawakomesha ndo inakuwa vp sasa?
   
 13. t

  taranda Member

  #13
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe inakusaidia nn waandishi wa habari wakikomeshwa? Mtu mzima ovyoo
   
 14. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Bila shaka "alifanya kazi kwa bidii" kama anavyotuasa babaake.
   
 15. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Wananchi wengi sana wameng'ang'ania misingi ya uongozi na kusahau kabisa mahitaji ya uongozi kama inavyowekwa wazi na falsafa za uongozi.

  Unapoona mtu ambaye amewahi kufikia ngazi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi yetu anaongea pumba za namna hii, ujue kwamba wale wanaosema kwamba kuna ombwe la uongozi wanazungumzia Jambo kubwa sana zaidi ya ufisadii na uwajibikaji.

  Katibu mkuu wa chama ambacho kinaongoza serikali iliyopo madarakani ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho hicho ana influence kubwa sana kwenye maamuzi ya nchi yetu, sasa angalia mtazamo wake jinsi ulivyo alafu ndio utajua kwamba serikali yetu imekuwa kwenye auto pilot mode kwa muda gani?

  Anadanganya wananchi kwamba Siasa ni mchezo wa kudanganya danganya, ungekuwa mchezo wa kudanganya danganya wangetumia mabilioni ya fedha kwenye kampeni zao?
  Kama siasa ni mchezo wa kudanganya danganya Lowasa ambaye tunategemea anaujua vizuri sana mchezo huo angekuwa radhi kutapanya mapesa yake kwa ajili ya kujipatia uongozi wa kisiasa.

  Huyu mzee na chama chake wanatapatapa, Watanzania wameishagundua kwamba Mabadiliko ya maisha yao yatatokea pale tu patakapokuwa na mabadiliko katika chama cha siasa ambayo yataambatana na mabadiliko katika mfumo wa kisiasa na uongozi pia.

  Watanzania wa leo wanajua kwamba alichokisema Sumaye kwamba anayetaka utajiri ajiunge na ccm alikuwa ametoa siri kubwa sana iliyokuwa ikizunguka kwenye makorido ya watawala peke yake.

  Siasa ndio mtaji wa maendeleo. Hivyo watanzania tutaendelea kushiriki katika michakato ya kisiasa wakati wote, ije mvua, lije jua, lije giza, uje mwanga, siku saba za kila wiki tutaishiriki siasa, na katika hilo tutaendelea kuwabana ipasavyo watawala wa kisiasa watimize ama ahadi zao ama majukumu yao na sababu tunajua hawawezi kila tutakapopata nafasi tutawalalamikia, kuwasononokea, kuwalaumu, kuwazomea na fursa zikijitokeza kuwaondoa madarakani.
   
 16. Tajy

  Tajy JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimezi'miss sana pumba zake,maana mzee kwa pumba ni kiboko!pepon kuna kazi gani tena!yeye amejuaje?
   
 17. Mnyamwezi wa Urambo

  Mnyamwezi wa Urambo JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hivi huyu mzee hamjamzoea tu?Kauli zake anapozitolea anajua mwenyewe,hapo wangezidi kumbana waandishi wa habari angeanza kunukuu aya za Bible na Quran!!
   
 18. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  wewe naye muda wako unakuja!!!!!!Hamis Andrea kuwa makini!!!tunaokujua tunajua kabisa muda wako unakuja!!!!!!!utalia tu!!!maneno gani hayo bwana andrea!!!!hayo uneongea wakati ule !!!unalala PANGANI,UNAOGA LUKUREDI!
   
 19. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Halafu huwa ana mis interpret mistari ya dini kujustify uovu !!
   
 20. +255

  +255 JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,910
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Kama ndio hivyo kwanini tunapoteza fedha kufanya uchaguzi wa viongozi, kwa nini tuwe na viongozi wakati inatakiwa tujitafutie wenyewe!!?
   
Loading...