Prishaz
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 2,855
- 4,894
Haya ni maoni ya Mh H.Kigwangalla.Ndio wabunge waliochaguliwa
kujadili na kupanga mbinu za kunyanyua uchumi wa nchi.mawazo ndo haya. ....kweli tutafika.
Hopeless MP! Yuko kwa ajili ya posho
Haya ni maoni ya Mh H.Kigwangalla.Ndio wabunge waliochaguliwa
kujadili na kupanga mbinu za kunyanyua uchumi wa nchi.mawazo ndo haya. ....kweli tutafika.
Kha! nilikuwa nakuamini kwamba umwana magamba makini kumbe ukipereto (Mpuuzi) namna hii! kweli mvinyo umewalewesha! i seehahahahhahhaaaa the spinning pro., aliwakomesha kweli hao waandishi wa habari!
hahahahhahhaaaa the spinning pro., aliwakomesha kweli hao waandishi wa habari!
Kweli wewe ni MD, MPH, MBA?...........
Yule kibabu aliyepata kuwa katibu mkuu wa CCM Luten Yusuf Makamba ameibuka baada ya kimya cha mda mrefu na kuwaasa watanzania waache kufikiri kwamba wanaishi peponi kwa kulalamika kila siku kuwa maisha ni magumu na badala yake wafanye kazi kwa bidii kwani hata huko peponi nako kuna kazi.
Vilevile amewataka waache kumlalamikia Rais J.M.Kikwete kwamba kashindwa kuyafanya maisha yao kuwa bora,kwani hilo si jukumu la rais Kikwete bali ni jukumu la kila mwananchi kunyanyua maisha yake bila kuitegemea serikali au Rais J.M.Kikwete.Alipoulizwa ni kwa nini wakati wa kampeni rais Kikwete alitoa ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania wakati anafahamu kuwa huo sio wajibu wake.
Makamba alidai kuwa siasa ni mchezo na kila mchezo una mbinu na hiyo ilikuwa mbinu ya rais kikwete na chama chake ili aweze kuchaguliwa kwani hata ahadi alizokuwa anatoa Dk.Slaa ya mfuko wa cement kuwa 5000/=kwa mfuko haiwezekani bali ni mbinu ya mchezo wa siasa.
SOURCE;Gazeti la Jambo Leo ukurasa wa 4.
My take; Mzee umri unamtupa mkono vibaya mno kama kweli haamini kama kazi kubwa aliyonayo rais wa nchi ni kuboresha hali ya maisha ya watu wake.
Makamba alidai kuwa siasa ni mchezo na kila mchezo una mbinu na hiyo ilikuwa mbinu ya rais kikwete na chama chake ili aweze kuchaguliwa
Yeye Makamba ndie mvivu kwa maana binti yake alikuwa anamuombea kaka yake dolari 2 million kwa ajili ya kampeni za ubunge kwa shemejie,sasa hapo inaonyesha Makamba na Co walivyo wavivuKutamka kuwa 'Watanzania waaache kulalamika na kufanya kazi' ni kuwadhalilisha. Je ina maana kuwa Watanzania ni wavivu? Ninaamini kuwa Watanzania ni wachapakazi mno na ndio maana wameweza kustahimili shida zote hizi zinazowakabili kwa miaka yote. Wamelea na kusomesha watoto wao na kujipatia riziki zao kila siku, wamejenga nyumba zao bila mikopo n.k bila msaada wowote.
Kuna siku nilikuwa nasafiri kwenye ndege kuelekea Ulaya, pembeni yangu alikaa Mmarekani. Katika mazungumzo yetu alibainisha kuwa ilikuwa ni safari yake ya kwanza kuja Tanzania. Nilipomuuliza ni kitu gani ambacho atakikumbuka kuhusu Tanzaniai, akasema kuwa kitu alichoona ni kuwa hajaona watu wanaofanya kazi sana kama Watanzania na wanafanya kazi hizo katika mazingira magumu.
Mtu anafanya kazi akiwa na malengo fulani. Kama yale malengo yake hayafanikiwi kutokana na juhudi za kazi zake, inabidi akae chini afikirie kwa nini hafanikiwi. Kuendelea kufanya kazi tu bila kutathmini matokeo ya kazi unayofanya si sahihi. Watanzania wanatathmini juhudi zao, kama wanaona hawayafikii malengo yao 'wanalalamika'. Katika hilo kulalamika ni sahihi. Ni mtumwa tu ndie asiyelalamika akifanyishwa kazi. Lakini hata akichapwa mjeledi, kilio chake cha maumivu ni kulalamika.
Yule kibabu aliyepata kuwa katibu mkuu wa CCM Luten Yusuf Makamba ameibuka baada ya kimya cha mda mrefu na kuwaasa watanzania waache kufikiri kwamba wanaishi peponi kwa kulalamika kila siku kuwa maisha ni magumu na badala yake wafanye kazi kwa bidii kwani hata huko peponi nako kuna kazi.
Vilevile amewataka waache kumlalamikia Rais J.M.Kikwete kwamba kashindwa kuyafanya maisha yao kuwa bora,kwani hilo si jukumu la rais Kikwete bali ni jukumu la kila mwananchi kunyanyua maisha yake bila kuitegemea serikali au Rais J.M.Kikwete.Alipoulizwa ni kwa nini wakati wa kampeni rais Kikwete alitoa ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania wakati anafahamu kuwa huo sio wajibu wake.
Makamba alidai kuwa siasa ni mchezo na kila mchezo una mbinu na hiyo ilikuwa mbinu ya rais kikwete na chama chake ili aweze kuchaguliwa kwani hata ahadi alizokuwa anatoa Dk.Slaa ya mfuko wa cement kuwa 5000/=kwa mfuko haiwezekani bali ni mbinu ya mchezo wa siasa.
SOURCE;Gazeti la Jambo Leo ukurasa wa 4.
My take; Mzee umri unamtupa mkono vibaya mno kama kweli haamini kama kazi kubwa aliyonayo rais wa nchi ni kuboresha hali ya maisha ya watu wake.
Sasa hapo Kigwangala unaemtetea katoa hoja gani ya kujadiliwa? Kasome tena alichoandika huyo mbunge wako ili ujilidhishe kama ni hoja au *****!Watanzania bana full of intimidations and all that; hivi kwa ni nini huwa tunakuwa wepesi kuweka hoja pembeni na kuattack mtu hili jukwaa bana linatumiwa tofauti kabisa manake Siasa ni kuvumiliana imagine unamwambia mtu wakati wake unakuja sasa we unazungumzia wakati unakuja ilhali yeye ameshakuwa?? Kwani yeye kasema atakaa hapo maisha yake?? Embu tuwe strict kwenye hoja bana. Niwatake radhi wanajamvi manake na mimi imenipasa nitoke nje ya mada kwa ajili ya kupeana ushauri....
Ishu ni kwamba watanzania tumezidi kulalamika kwamba JK ni tatizo wakati sio kweli!! Mtu ni mfanyakazi wa serikali, shifti yake ni ya mchana, unamkuta saluni saa tano asubuhi siku ya kazi, anafanya scrub huku anamlaumu rais kishenzi!!!! Anamaliza scrub anaenda lunch akiwa huko anapanga mkakati wa jinsi ya kupata cha juu kwenye manunuzi ya computer za idara yake, akitoka huko anaenda kusaini kwa keshia pale kazini kwake alipwe posho ya kukaa kwenye kikao ambacho hakuchangia chochote (wazo lolote). Muda wa kazi umeisha anarudi nyumbani. Sasa anamlaumu raisi wa nini? hiyo hali nzuri anaipataje kwa kulipwa kwa kutofanya kazi? si anaiibia nchi huyo? rais anajengaje uchumi imara kwa watu wake ambao kazi yao ni kuiibia serikali (kujiibia wenyewe)? Tuna tatizo la kiuongozi kwa sababu tu serikali imeshindwa kudhibiti watu wasilipwe bila kuzalisha, full stop. Kila mtu anataka kupata pesa za bure, bila kufanya kazi. na mahali pekee unaweza kuiba kirahisi siku hizi ni serikalini!!! tukitaka maendeleo watanzania wote tubadilike kimtazamo kwanza. bila hivyo hata tukipata rais gani haina maana. Vitu vikuu ambavyo ndiyo msingi wa maendeleo wa taifa lolote na ambavyo vimetumika na mataifa yaliyoendelea zaidi kufika hapo yalipo ni:
1. Maadili.2. Uaminifu.3. Uwajibikaji.4. Kuheshimu sheria.5. Kuheshimu haki zako na watu wengine.
6. Kupenda kufanya kazi.7. Kupenda kuweka akiba na Kuwekeza.8. Kwenda na wakati
Hii imekuwa proved kwenye tafiti mbalimbali za kujaribu kutafuta suluhu ya umaskini uliokithiri huku kwetu. Hizi ni kanuni kuu za maendeleo ambazo hazitekelezwi mojamoja bali zinaenda pamoja. Tunahitaji viongozi wanaoweza kutubadili tukazifuata kwa ukamilifu. Itaendelea.
Wewe inakusaidia nn waandishi wa habari wakikomeshwa? Mtu mzima ovyoo
hahahahhahhaaaa the spinning pro., aliwakomesha kweli hao waandishi wa habari!
hahahahhahhaaaa the spinning pro., aliwakomesha kweli hao waandishi wa habari!
Hivi kuna watu mmetumwa hapa JF kunishughulikia ama basi mnanichukia tu? Mbona hata hoja nyingine hazina maana mnaanza tu kunitukana...acheni hizo, fanyeni bidii kidogo ya kufikiri! Sasa mimi kusema nimefurahishwa na majibu ya kisiasa ya Mzee Makamba ni kosa? Kweli alifanya spinning kwenye maneno yake na alifanya vizuri
Nasema aliwakomesha si kwa nia mbaya, ni kwamba hakuwapa kile walichokitarajia, aliwakwepa...
Ntogwisangu ndg yangu kumbe wewe ni mtu wa MUCHS enzi zile, sasa matusi na kashfa zote unazonirushia ni za nini? Wewe si brother yangu kabisa, hauoni hata aibu unavyonishughulikia hapa jukwaani bila sababu ya msingi? Mimi sikuchukii wala sikumaind bali nakuhurumia na kukuombea upate uelewa...hivi haujawahi hata kuona ni jinsi gani nime-dedicate maisha yangu katika kuikoa fani yetu ya udaktari? Umenisikitisha sana kwa kweli! Kuwa fair, hata kama hutaki kunisifia (ambacho sikuombi ufanye) basi walau usinikashifu, maana mimi hata kama ningekujua nisingekukashfu kwa kuwa wewe ni ndg yangu. By the way, nilikuwaga siendi kuoga Lukuledi, nilikuwa naenda kuoga Kagera, nalala Pangani (kwa mchumba wangu - ambaye leo hii ni mke wangu na mama wa watoto wangu). Nilikuwa nahangaika tu na maisha wala hayo si mambo ya kushabikia kaka, ni umaskini tu wa kwangu binafsi na wa nchi yangu ndiyo maana nilikosa mahala pa kuishi nikalazimika kuishi chuoni kwenye chumba cha mchumba wangu!