Uchaguzi 2020 Makamanda wenzangu tutumie akili, NEC inasimamia uchaguzi ili Watanzania wapate maendeleo

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
3,166
4,581
Nashangaa sana makamanda wenzangu mnamshambulia Wilson Mahera wa NEC kwa kitendo cha kumuita Mgombea wetu kwa kamati ya madili ya taifa.

Je, hamjui kuwa NEC inasimamia uchaguzi ili Watanzania wapate maendeleo? Hamjui aliposema Watanzaia wanahitaji barabara, sekta ya afya iliyoimalika, sekta ya elimu iliyoimalika na miundo mbinu iliyoimalika. Haya ni maendeleo ya wananchi.

Sasa kama mgombea wetu akisimama jukwaani kazi yake ni kutoa tuhuma za JPM kutokuwa na cheti cha kuzaliwa, kupigwa risasi, ufisadi wa uwanja wa ndege Chato, ufisadi wa ununuzi ndege Atcl n.k. Je, hizi ni sera za kuwaletea maendeleo wananchi?

Tuwe wakweli mgombea wetu anatakiwa ajirekebishe sana. Kama anataka urais aseme atatufanyia nini watanzania sio kutuhumu wagombea wenzake.

Je, hizi tuhuma anazozitoa ataweza kuzithibitisha?

Lissu-Mwibara-Mara-1(1).jpg
 
Enyi wakaki, kijani na manjano, mmeona nyekundu ile pale haijaja pale leo.

Ipo tangu kale, msiruhusu iwaguse si kwakua hamna hadhi la hasha, ila ile rangi anaifahamu msimuliaji

Ile rangi ni damu iliyomtoka au kumrukia na mchanganyiko wa damu zote za pande za dunia.

Anajua leo anaijua jana hajaisoma au kuisikia, aliipata wakati akitafuta vya kusimulia

Na ndio hivi anavyotaka kukusimulia leo.

=Dizasta vina=
 
NEC ina tabia mbaya sana, yaani kumgeuza Mkurugenzi wake kuwa mpiga debe wa CCM, hiki kitendo hakikubaliki hata kidogo maana kinakwenda kinyume kabisa na Maadili ya uchaguzi.

Mgombea wa CDM lazima alichukulie hatua jambo hili - Refa kugeuka kuwa kocha hili halikubaliki.
Fuso acha hasira, simamia ukweli.
 
Wewe kweli ni kamanda uliyechoka..... wewe ni kiziwi mpaka sasa hujasikia Tundu Lissu amesema atatufanyia nini????

Wewe hata kujificha umeshindwa kujificha kuwa ni ccm, naomba ujifunze hata kuandika kama unataka kuwa kamanda. ............Pia asilimia kubwa ya wananchi wanaelewa anachokisema Lissu, hayo mnayotaka asema yasemeni ninyi na mgombea wenu pamoja na huyo mkurugenzi wenu wa tume ya ccm
 
Kamanda wenzako ni kina nani?

CCM kwanini mnakuwa na hoja za kijinga hivi ?
 
Wewe hata kujificha umeshindwa kujificha kuwa ni ccm, naomba ujifunze hata kuandika kama unataka kuwa kamanda. ............Pia asilimia kubwa ya wananchi wanaelewa anachokisema Lissu, hayo mnayotaka asema yasemeni ninyi na mgombea wenu pamoja na huyo mkurugenzi wenu wa tume ya ccm

Mkuu bila shaka si mimi unanisema hapa....huyo kamanda asiyechoka
 
Back
Top Bottom