Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
Mungi watu hawataki kwenda Dar es Salaam makao makuu! Huko kila mtu ni mkubwa. Wewe kwa mfano utoke kuwa RPC mwanza (yaani IGP wa Mwanza) halafu uhamishiwe sijui kuwa mkuu wa kitengo makao makuu! Nani anataka hiyo ukiamka IGP huyu hapa, ukigeuka DCI huyu hujakaa sawa Waziri huyu kabla hujajipanga sijui Mkurugenzi gani huyu; nani anataka hiyo?
Ukiwa mkoani wewe na mkuu wa mkoa tu basi hakuna kingine. Budget ya mkoa yako kama mkoa una madini kesi zinaanzia kwako na makandokando mengine kibaaaao.
Mwita Maranya yaani Tossi ameajiriwa tena baada ya kulitumikia Taifa miaka yote hiyo? Ina maana hakuinuliwa mgongo kiasi kwamba akapumzike na kusubiri kukutana na mola wake? Miminilifikiri baada ya kutupatia utumishi uliotukuka basi huyu Kamanda angekuwa anakula pension yake kwa mbwembwe bila tena kutakiwa kutoa report kwa mtu yeyote. Kumbe bado anapambana na majangiri waliomuua George?Venance Tossi amestaafu kazi ya polisi. Sasahivi ameajiriwa kwa mkataba na Tanapa akiongoza kikosi cha Rangers (askari wa wanyamapori).
Zelothe Steven ndiye RPC Dodoma kwa sasa. Naye ni mnoko sana hafai kabisaa kuwa IGP!
Kwa uelewa wangu mdogo cheo cha Mkuu wa Utawala na Rasilomali watu ktk Jeshi letu la Polisi siyo kikubwa kwa madaraka tu bali hata rushwa anayopokea mwenye hiki cheo ni kubwa kulinganisha na RPC wa mikoa! Huyu ni mungu mtu ktk jeshi la polisi! Nadhani amechukua nafasi ya kamishina Mtweve kama sikosei. Acheni mchezo na hiyo nafasi!
.............Pale mkoani alikuwa ndiye mwenye maamuzi na mtendaji mkuu katika mambo ya usalama katika mkoa mzima. Niambieni huko Dar atamwamrisha nani maana ofisi yake imezungukwa na wazito zaidi yake ambao anatakiwa kuwapigia saluti na shikamoo kulinda kitumbua chake.
Pale makao makuu kila anachofanya anatazamwa na kufuatiliwa tofauti na mkoani yeye ndiye yeye, na mkoani ni mmojawapo wa wakuu wa juu mkoani kama Mkuu wa mkoa, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa na RPC. Huko nani atampa nafasi hiyo wakati vizito akina Mwema wapo?
.............. demotion by promotion.......
Kwenye hii thread watu wanaongelea dhuluma za polisi dhidi ya raia na hapo hapo wanaongelea kuwa RPC ni deal kwasababu kuna ulaji.
Hizi contradiction katika fikra zetu ndio zinatishia ile Tanzania bora ambayo wote tunaitaka.
Tatizo la TZ sio mtu mmoja mmoja bali mfumo mzima na culture ya sisi wananchi ya kufikiria deals badala ya kufikiria kazi na uwajibikaji.
Bila kuzingatia hayo tutaondoa Andengenye mmoja na kuleta Andengenye mwingine na tofauti pekee itakuwa sura na utii kwa wanasiasa tofauti.
Ngoja nimsubiri,nitaenda kumpa salamu.Karibu sana.
Hapo kwa ma-analyst wazuri ndipo point ilipo, Mnajua huyu jamaa hana tatizo na mtu na ni mtu wa logic na haki sana niliwahi kukutana ama kushuhudia kashkash zake Moro alipokuwa IGP pale. Anyway nataka kusema kumuhamisha huyu jamaa inaweza ikahusiana na mauaji ya Mwenyekiti wa CDM kwani alikuja na strategy nzuri sana hadi akaahidi 10M sio masihara na inawezekana wauaji walitumwa na WAKUBWA na watu walioko kwenye SYSTEM sasa jamaa (Andengenye) inaonekana angeweza kuwabainisha wahusika wote so ikabidi wamhamishe fasta kufunika kombe mwanaharamu apite wakampa na cheo cha kuzugia. Hebu fikirieni kidogo ni kwanini wamhamishe sasa na kama mnakumbuka maandamano mengine ya CDM Arsh aliyaachia yafanywe freely baada ya yale ya mwanzo sababu yeye kama IGP lazima ashrkshwe, Mi naamini kuna kitu hapo...Heee' zile mil 10 alitoa ahad za kukamatwa kwa waliomuua mwenyekiti wa CDM usa ndo bas tena na hata ufatiliaji wa wahusika wa kifo hicho utakua hafifu sana coz huyo aliyekuja atasema hajui au kakuta file mezani lililoachwa na mtangulizi wake Andengenye so atakuwa hana nguvu ya ufatiliaji wa mauaji hayo.
Mungi,
Taarifa za Andengenye kuandaliwa kuwa IGP zimezagaa sana mitaani hata kabla ya uteuzi huu. Lakini atambue kwamba hata kama atakuwa ameteuliwa kuwa IGP siku tukipandisha juu bendera ya ukombozi kwa mara ya pili basi hapo ni kama alivyofanya Rais Joyce Banda wa Malawi.
Mi kuna kamanda namtafuta anaitwa Venance Tossi..........