tukihesabu kuanzia 1964 mpaka 1981, basi ni miaka 17ukereketwa kazi kweli
umeandika " Nijuavyo tuko mbioni kusherehekea miaka 50 ya nchi ya Tanzania ambayo ndio iko kwenye ramani ya dunia"
HII SENTENSI YAKO INA MATATA
HESABU VIZURI,
TANZANIA ILIANZA 26 APRIL1964 ,
ukihesabu 1964 mpaka 1981 ni miaka mingapi???? 50?????
Ndugu yangu uamuzi unao mwenyewe.Ukipenda soma la hupendi acha.Hatutagombana kwa hilo.MohamedIli nisome kitabu chako nihakikishie kwanza kuwa wewe unajua pia upande mwingine wa shilingi jinsi watu wa maeneo ya bara walivyopigania uhuru ili niondokane kwanza na mtazamo kuwa wewe unafahamu mambo ya pale gerezani tu. Halafu ktk uandishi wako usitumie reference ambazo zina mlengo wa kidini i.e Tumaini letu, nyakati, Al huda, An nuur. Tumia neutral sources. Kwangu mie naziamini zaidi habari za Aljazeera, PressTV kuliko taarifa za Al huda na An nuur maana naamini kuwa waandishi ktk magazeti hayo sio waandishi makini.
Unapoteza muda, find some business to do upate japo pesa ya kula, umetumwa na BAKWATA, waislamu wa ukweli they aint enslaved like what you're thinking, kaa hivyo hivyo , huchoki tu kuwa-victimize, wamestuka tayari huoni haya!Wanaukumbi,
Kuanzia leo Jumatano, 28 Septemba
Mwananchi limeanza "series" zangu na
za waandishi wengine kuhusu Miaka
50 ya Uhuru wa Tanganyika.
Tusomeni kwa furaha.
Mohamed Said
========================
UPDATE 29/09/2011
========================
Unashukuru nini sasa, it seems hata wewe huelewi unachoambiwa! Moderator can you block guys like this! kwanza anachafua hali ya hewa tu!Ahsante kwa mchango wako.
Katika gazeti la Mwananchi la leo kuna makala zangu mbili
na kila moja nimeandika kwa staili yake.
Moja nimezungumzia Tanganyika chini ya Udhamini wa Umoja
wa Mataifa.
Makala ya pili nimejieleza mimi mwenyewe kama mtoto mdogo
wakati wa kupigani uhuru.
Nimeanza kwa kuhadithia nyumba kwa nyumba mitaa ya Gerezani
nilikozaliwa na kukulia nikieleza historia za wazee wangu walivyochangia
katika kupigania uhuru.
Sijui hili la Uislam liko sehemu gani. Tafadhali nifahamishe wapi umeliona.
Nimepitia upya makala hizo sikuona popote neno Uislam.
Mohamed
Unashukuru nini sasa, it seems hata wewe huelewi unachoambiwa! Moderator can you block guys like this! kwanza anachafua hali ya hewa tu!
Unapoteza muda, find some business to do upate japo pesa ya kula, umetumwa na BAKWATA, waislamu wa ukweli they aint enslaved like what you're thinking, kaa hivyo hivyo , huchoki tu kuwa-victimize, wamestuka tayari huoni haya!
Mohamed Said,
Bandika vitu mwanzo mpaka mwisho, maswali na majibu mwisho wa bandiko. Achana na hawa wanaosutwa na historia, wanakuta ukweli uliopo ni tofauti na wanavyofundishwa kwenye shule zao za kanisa.
Mohamed Said,
Bandika vitu mwanzo mpaka mwisho, maswali na majibu mwisho wa bandiko. Achana na hawa wanaosutwa na historia, wanakuta ukweli uliopo ni tofauti na wanavyofundishwa kwenye shule zao za kanisa.
Mohamed Said aweke ukweli
ila akileta udini mimi nitamletea udini mara mbili
Dawa ya mdini ni kuwa mdini zaidi yake
Nasaha nzuri sana.Wakuu, hii mada ukiisoma vizuri, ina mafundisho na inatia kiu zaidi kuijua historia ya kweli ya nchi yetu iliyotukuka, nchi ya Tanganyika. Najuwa kuna wanao ujuwa ukweli na hawataki ukweli ujulikane, lakini kupitia hii thread nadhani ni mahala mwafaka kabisa kwa kila Mtanganyika anayejuwa historia ya wapigania uhuru, basi hii ndio fursa kuwaweka hapa, ili kila mtu ajuwe michango yao... Na hao mashujaa wa uhuru si wale wa mikoa ya pwani tu kwa maana ya wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake, la hasha... Watoke mikoa mbali yote ya Tanganyika.
Natarajia wapo wanaojuwa mashujaa kutoka mikoa mingine, kama vile Mwanza, shinyanga, Kigoma, Tabora, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Mara, Kagera, Dodoma, na mikoa mingine ya Tanganyika (Tanzania Bara).
Tuichukulie hii topic katika hali chanya, na tuijazilie kwa kile tukijuwacho. Wapo wapigania uhuru waliokuwa Waislam, Wakristo na waliokuwa wakiabudu dini za jadi, basi tuwaweke hapa na kila mtu awasome. Mimi nina uhakika kabisa uko mikoani wapo waliojitolea kwa hali na mali katika kadhia hii ya kugombania uhuru, basi tuwape heshima yao japo kwa kuwataja tu majina yao.
Miaka ishirini (20) mpaka therathini (30) nyuma, hatukuweza kupata nafasi kama hii, ya kujimwaga na kujifaragua, sasa ndio wakati mwafaka wa kuelezea kile kilichokuwa kikifichwa hapo zamani...! Chuki zisitawale huu mjadala, kama ndugu yetu Mohamed Saidi yeye anaelezea historia, inayo wagusa Waislam wa mitaa ya Kariakoo na Gerezani, basi aje mwingine aelezee, wapigania uhuru wa mikoa mingine, aidha Wakristo waliojitolea kumtoa mkoloni au walio amini dini za jadi. Maana wote hao ni Watanganyika na wana haki ya kuelezwa hapa na mahala pengine...!
Tusiukatae ukweli, maana ukweli una tabia ya kujilipiza kisasi, leo ukiukataa, kesho ukweli utakuja julikana, basi nyuso zetu tutaziweka wapi? Au mpaka mkoloni arudi tena na kutufundisha historia ya nchi yetu wenyewe?
Jamani shime shime! Wakati ndio huu.
Mohamed Said:Kuanzia leo Jumatano, 28 SeptembaMwananchi limeanza "series" zangu na za waandishi wengine kuhusu Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika
Hadi hapa tunaona mada nzima inajadili miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Fair enough!X-PastersWakuu, hii mada ukiisoma vizuri, ina mafundisho na inatia kiu zaidi kuijua historia ya kweli ya nchi yetu iliyotukuka, nchi ya Tanganyika
Uhuru wa Tanganyika halafu historia ya Kariakoo!! Nadhani tuwe wakweli ili tusiwafanye wana jamvi majuha.Kinachoongelewa hapa ni uhuru wa Tanganyika hili la Kariakoo ni kujaribu kuepusha 'bias'. Tuweni wakweli ni sehemu ya uungwana na uumini.X-Paster: Mohamed Saidi yeye anaelezea historia, inayo wagusa Waislam wa mitaa ya Kariakoo na Gerezani, basi aje mwingine aelezee, wapigania uhuru wa mikoa mingine, aidha Wakristo waliojitolea kumtoa mkoloni au walio amini dini za jadi. Maana wote hao ni Watanganyika na wana haki ya kuelezwa hapa na mahala pengine
Faiza Foxy,
Asante sana kwa hilo ila suala la kanisa ungelipunguza kwani hata sisi tuliosoma shule miaka 1970-1980 tulikuwa tukimeza misumu ya vitabu vya wakoloni. Nilikujaga kusoma historia ya zanzibar nilipokuwa kikazi Zanzibar kutoka kwa wazanzibar wenyewe na baadhi ya wazee waliokuwa wakiishi huko nilitokwa na machozi jinsi wakoloni na serikali ya JKN walivyopindisha mambo mengi. Moja wapo kukataa kuwa utawala wa Sultani ulikuwa ukinufaisha wazanzibar na dhana ya mapinduzi ilikuwa slogan ya kibaguzi na chuki dhidi ya wasiokuwa na asili ya kiarabu. Watu wakati wa Sultani Khalifa mfano walikuwa wakipewa maziwa bure kisiwa kizima, shule bure kisiwa kizima, wanafunzi wanapewa uniform, vitabu na madaftari bure sasa nikajiuliza ubaya wa Sultani uko wapi??? Tanzania ni zaidi ya uijuavyo. Sheikh Mohammed Said endelea kumwaga vitu nimefanya research ya unayosema kuhusu majimaji kwa jamaa zangu wa huko Kilwa na kuconfirm kumbe wale walikuwa watu wa tariqa bwana na wakati mie nilisoma historia ya vita vya majimaji vitabu vikasema ati mganga alikuwa akisoma maji halafu risasi ya mkoloni itageuka kuwa maji (huu ni uongo na nadhani walioandika historia wanatakiwa kuwa sued for intellectual infringment (wamedanganya na kuhadaa)). Maji yalikuwa sio ya mganga bali hawa walikuwa waislamu na walikuwa wakitawadha na kutia udhu na kwenda kupigana vita kama uislamu unavyosema ili wakifa wafe mashahidi. Hiyo dondoo moja Sheikh Mohammad Said ya jitihada zangu binafsi kuufahamu ukweli wa historia ya linchi letu.
Narudia Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
'Ukweli unatabia ya kulipa kisasi,leo ukiukataa kesho tutaweka nyuso zetu wapi'? Nami nauliza ukweli ni upi kati ya wanaojadiliana kwa jambo walilosimuliwa au kuhadithiwa? Ukweli unapitakanaje kama haukidhi haja ya majadiliano au malumbano?.Je,ukweli unatokana na kumeza au kutafakari! Hadi hapa tunaona mada nzima inajadili miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Fair enough! Uhuru wa Tanganyika halafu historia ya Kariakoo!! Nadhani tuwe wakweli ili tusiwafanye wana jamvi majuha.Kinachoongelewa hapa ni uhuru wa Tanganyika hili la Kariakoo ni kujaribu kuepusha 'bias'. Tuweni wakweli ni sehemu ya uungwana na uumini.
Mohamed Said ameleta mada hapa (ingawa si mpya) baada ya kuitoa magazetini. Nadhani nia ni kuamsha mjadala wa fikra utakaotusaidia kwenda mbele au vinginevyo kama hajaweka wazi. Taratibu zetu ni kuwa mada inapowekwa inapewa heshima ya kuchangiwa labda kama mwandishi atakuwa amekataa hilo kufanyika, na hiyo itakuwa ajabu kwasababu basi angeiacha huko magazetini wanaomeza wameze tu!
Midhali ameiweka hapa itapata changamoto zinazolingana na kwa viwango kama ilivyowahi kutokea huko nyuma. Katika tafakuri kutakuwa na mitazamo hasi na chanya, na ni wajibu wa mtoa mada kutoa uelekeo. Inapotokea kuwa 'criticized' na kuonekana kama ni 'uasi' au ukorofi ina leta maana kuwa mada imewekwa isomwe tu! na kama hilo ndilo lengo basi litoke tamko na litaheshimiwa.
Vinginevyo hatuna sababu ya kutuhumiana kwa kauli zisizo na ukweli au zenye kuamsha hisia chafu kama zile za 'kusoma makanisani' n.k. Wasomaji na wachangiaji wana mila, kabila na imani zao ikiwa ni pamoja na vyanzo vyao vya elimu, kazi n.k na si vema kuanza kupotosha mada kwa kuchomeka mambo kama hayo yanayojenga hisia za kibaguzi au udini. Lau kama hilo ndilo lengo ahlan wahsalan.
Andiko lolote hapa kwa mujibu wa forum hii lina haki ya kujadiliwa na kuhojiwa, nami nikiwa napenda kusimamia ukweli, kuhoji ili kuelewa na kukemea chembe zozote zinazolenga kuigawa jamii yetu nitahoji bila kuomba radhi au ruhusu kwa kufuata kanuni za forum. Nitakemea ikibidi na kama kufanya hivyo sitampendeza mtu siombi radhi. Nitakachokikwepa ni kejeli,kashfa, tashtiti, munkari,jwazba na ubaradhuli wa namna hiyo.
Mohamed Said,
Ni nini mchango wa AMNUT katika harakati za ukombozi wa Kariakoo, Gerezani au Tanganyika?
Ni kwanini Waislam wa Kariakoo,Gerezani/Tanganyika hawakuiunga mkono?
Ni lini utaratibu wa kutumia namba katika mitihani ulianza kutumika?
Nisaidieni hapa nimekwama na nashindwa kuunganisha dot za mada kwasababu nimekwama. Tafadhali nifahamishe.
Ahsante.
Una mfahamu Mohammed Said au una msikia tu?
Jamaa anatetea msimamo wake wa kidini kama nini vile.
Utabishana naye page na page kwa vile kwake uhuru ni uhuru wa uislamu dhidi ya dini nyingine na si vinginevyo.
Kama humjui mPM.
Bi Faiza,
Mungu akujaze kheri.
Napata faraja ninaposoma fikra kama hizo zako.
Historia ya Majimaji na makumbusho yake Mahenge, Songea
yapo katika mtihani mkubwa.
Hata yale majina ya askari wa Majimaji hayatakiwi kuwapo kwa
kuwa tu jeshi zima lina majina ya Waislam.
Majina ya mashujaa wale yanayoashiria Uislam wao yameondolewa.
Songea Mbano aliyekuwa amiri jeshi dhidi ya Wajerumani jina lake
ni Ali Songea Mbano.
Jina la Ali halitakiwi na ni hivyo hivyo kwa kila askari majina yalowekwa
ni ya Kikristo ati walibatizwa kabla ya kunyongwa.
Hii ni dhulma na upotoshaji mkubwa.
Soma hii kutoka "Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania Mainland":
[1]Maji Maji Museum in Songea which has been greatlydesecrated removing all signs of Muslim symbols during the Maji Maji War withGermans. The Maji Maji Museum at Peramiho under the Catholic Church has closedits doors to young inqusitive Muslims for fear of criticism for distorting history. AllMuslim symbols in Maji Maji War against Germans have been obliterated in theMaji Maji Museum.
[1]In all historical references to Maji Maji War hero and Chief of WangoniAli Songea Mbano, his Muslim name "Ali" would be omitted and he would bereferred to as Songea Mbano.
Mohamed