Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Ndio maana nasema ni udini wa kijinga kwa sababu watu wakipatiwa elimu inayostahili na kujulishwa kile ambacho walikuwa hawakijui juu yao wao wenyewe au vingine wataweza kuona ujinga wao na wataachana nao. Ninaposema ni udini wa kijinga ninamaanisha hilo kwa maana hauna akili. Mtu mwingine kaja kuniambia ati udini wa leo umesababishwa na Nyerere; mwingine anasema udini ni wa Wakristu (kanitolea orodha ndefu ya mambo ambayo wakristu wamefanya) kwa vile rais ni "muislamu"; na wengine wananidokeza jinsi mambo ambayo Rais "muislamu" anayafanya na ambayo wakristu wanaona ni ya kuendeleza "uislamu".
Wote hawa wanaona wako sahihi kwa sababu "udini" kwao ni wa yule aliye tofauti na dini yao lakini hakuna ambaye ameijaribu kuangalia udini wake yeye mwenyewe au wa watu wa dini yake na badala yake anajaribu kutafututia udhuru au kuuhalalisha kwanini watu wake wana "udini".
Yaani, NI UDINI WA KIJINGA!