Makada wa CCM wawe wapole

Makada wa CCM wawe wapole

JOESKY

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
823
Reaction score
2,045
Wasaalam ndugu wanajukwaa!!

Ni muda mrefu kidogo nimezidi kuumizwa na tabia za makada wa Chama Cha Mapinduzi (si wote ni baadhi). Kumekuwa na tabia ambayo wanazidi kuikumbatia na kuiona ni sawa kabisa katika majadiliano kuitumia kama ngao ya kumdhibiti mtu anaehoji uhalali wa kitu fulani au hoja fulani.

Kweli tumezoea na kuona ni kawaida sana kwa sasa hivi Kuona kukosolewa ni kama kushushiwa hadhi au thamani ya kada husika. Kipindi cha mwishilizo wa mwaka jana kipindi cha kampeni Bwana Magoiga SN aliniblock kwa sababu ya kusimamia misimamo yangu yenye misingi ya kidemokrasia.

Leo hii tena bwana Thadei Ole Mushi kaniblock kisa tu eti nimemwambia bwana Tadei huu mwaka kama ukiisha bila kupewa uteuzi achana na siasa fanya mambo yako. Hii imetokana na yeye kupost kuhusu kubadilisha katiba ya JMT ili kumruhusu Yohana kutawala milele.

Si huyo tu kuna huyu Bwana Nape M Nnauye aliniblock twitter kisa tu kumkosoa na kutokubaliana nae kuhusu ile kauli yake ya goli la mkono pamoja na kufungia bunge laivu.

Kwa kifupi ni wengi wameniblock ila sipati majibu ni kwanini wanafikia hatua ya kublock mtu ambaye yuko tofauti nao kimtazamo???
Ningependa kuwashauri waweze kujua kuwa ukishakuwa mwanasiasa unatakiwa uwe na deep spirit ya political torelance. Hiki kitu kwa hawa ndugu zetu kimekuwa kitu ambacho kwao si kipaumbele kabisa.

Nawapa salamu wale wote makada mnaopenda kupost pumba za aina hiyo halafu mnategemea kupata positive respond kutoka kwa watu tunaojitambua mtakuwa mnapoteza nyakati.

Asanteni na karibuni kwa mchango.
 
Shukuru Mungu wanakublock.

Lissu alishambuliwa na risas zaidi ya 30 (hata Nguruwe pori hawezi shambuliwa hivyo).

Ben saanane na Azory hadi leo haonekani.

N.B UKITAKA KUWA RAFIKI WA HAYO MAKADA WEKA AKILI PEMBENI.
KUNA GHARAMA KUBWA YA KULIPA UKITUMIA AKILI YAKO NCHI HII.
 
kuliko kuanza kuchambana nawe, ili wakuongezee atention wanaona bora wakuhifadhi tu.

Ukweli haambiwi mtu mzima.
 
Hilo jambo la block ni kwa wengi hata wanaharakati na baadhi ya wapinzani mkitofautiana tu anakupa tofali
 
Huo uhuni upo twitter kama wote tutaorodhesha walio tublock kazi itakua kubwa mimi Lissu aliniblock kisa tu nilimwambia hatoshinda uraisi na sapoti ya maandamano watu hawatoki!
 
Huo uhuni upo twitter kama wote tutaorodhesha walio tublock kazi itakua kubwa mimi Lissu aliniblock kisa tu nilimwambia hatoshinda uraisi na sapoti ya maandamano watu hawatoki!
Wewe kwa akili ulizonazo huna nafasi ya kumshauri Lissu,
Bora uendelee kuburuzana na chumia tumbo wenzako kina @ wakudadavua
 
Back
Top Bottom