Makachero waendelea kuwahoji maofisa KIA

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linaendelea kuwahoji maofisa kadhaa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuhusiana na tuhuma za kuruhusu usafirishaji wa twiga wanne kwenda Uarabuni bila kibali.
Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Ngh’oboko, aliiambia NIPASHE kuwa uchunguzi huo unaendelea, lakini alisema kuwa twiga hao walitokea mkoani Arusha.
“Maofisa hao wa KIA walikiuka taratibu. Tunachunguza kuona nini kilitokea,” alisema Ngh’oboko. Alisema maofisa wa polisi wako kazini kupitia nyaraka na vibali, ambavyo wanaendelea kuvitafuta.
Kamanda huyo alisema taarifa zikikamilika, polisi watatoa taarifa.
 
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linaendelea kuwahoji maofisa kadhaa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuhusiana na tuhuma za kuruhusu usafirishaji wa twiga wanne kwenda Uarabuni bila kibali.
Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Ngh'oboko, aliiambia NIPASHE kuwa uchunguzi huo unaendelea, lakini alisema kuwa twiga hao walitokea mkoani Arusha.
"Maofisa hao wa KIA walikiuka taratibu. Tunachunguza kuona nini kilitokea," alisema Ngh'oboko. Alisema maofisa wa polisi wako kazini kupitia nyaraka na vibali, ambavyo wanaendelea kuvitafuta.
Kamanda huyo alisema taarifa zikikamilika, polisi watatoa taarifa.

Twiga wanapelekwa kuishi wenye "viyoyozi"
Kama ningeuwa waziri husika ningependekeza hivi

  • No kuuza wanyama wetu. totakuwa tunakodisha kwa mataifa mbali mbali wanaotaka kuwaweka kwenye zoo. So kama twiga toka siku anapochukuliwa serikali inatoza $ 50 per day.
  • Mkataba unasainiwa kuwa hakimiliki ya nyama husika ni yetu na hata akijifungua basi watoto ni mali ya tanzania. teh tehteh

Haya mambo ya kuuza wanyama decison makers wajue wana betray utaliii. Zooo ya UK yenye tembo, twiga sokwe waliotolewa afrika ina watalii na mapato mengi kuliko natinal park ya serengeti. Wanalijua hili

EAC fanyieni kazi hilo hakuna kuuza wanyama nje .
Watetetzi wa haki za wanyama fanyieni kazi hizlo kupinga wanyama pori kupelekwa kwenye habitat isiyokuwa yao.
 
Juzi hapa walikamatwa Cheeter kwenye cages huko huko Arusha na sasa Twiga. Nchi hii tumewapa watu wasiostahili kutuongoza kwa hiyo wanashindwa hata kulinda rasilimali, wako busy kujivua gamba huku wakitengeneza magamba mengine ya wizi wa wanyama. Maskini Tanzania, kama tunashindwa hata kulinda faru ndio iwe twiga. Ifikie siku jamani tuseme basi,,,,
 
viongozi wengi wanachukua chao mapema!sijui kwanini tanzania tumefikia hali hii
 
Marekani hukodisha wanyama aina ya panda kutoka China na kulipa dola milioni moja kwa mwaka. Panda wanapatikana China peke yake.
Sisi tunawaruhusu wale waarabu wa Loliondo kuleta madege ya kubeba mizigo na kuhamisha shehena ya idadi isiyojulikana ya wanyama bila malipo yeyote kwa sababu Mwinyi aliwakabidhi eneo hilo kama himaya yao.
 
kwa vile stakuwa rais lakini ningekuwa rais hao wote waliohusika na sakata hili la kusafirisha hawa wanyama na waliotoa vibali feki wanapigwa risasi hadharani pamoja na wale mafisadi wakubwa wanaotakiwa kujivua gamba na kujiondoa kwenye chama cha magamba.Hebu tuone mwisho wake kama watachukuliwa hatua zozote hawa na wasi wasi kuna mkubwa anahusika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom