Makachero wa Kagame mbaroni Dodoma

Makachero wa Kagame mbaroni Dodoma

KOLOKOLONI

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
2,476
Reaction score
2,372
Mashushushu wanawake wanne raia wa Rwanda wanaoaminika kutumwa na Rais Paul Kagame wamekamatwa mjini Dodoma. Wamekamatwa wakiwa wameshajenga uhusiano wa karibu na baadhi ya viongozi waandamizi pamoja na wajumbe wa Bunge la Katiba.

Pamoja nao Rwanda inadaiwa kuingiza makachero wengine wengi ili waungane na wakimbizi wa Kitutsi walioingia hapa nchini katika miaka ya 1958/1959 na mwaka 1994. Habari kutoka vyanzo vya uhakika zinasema wapelelezi wengi wamekuwa wakiingia nchini kupitia Karagwe mkoa wa Kagera, ambako kumeanza kuonekana kama sehemu ya Jamhuri ya Rwanda.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Tanzania imethibitisha kukamatwa kwa makachero wanawaeke wanne raia wa Rwanda, wakijifanya ni makahaba, lakini baada ya uchunguzi imebainika pasi na shaka kwamba ni makachero toka Rwanda. Ukahaba unatumika kama moja ya nyezo adhimu katiak shughuli za ukachero.

Duru za uchunguzi zimebaini kuwa wanawake hao ni sehemu ya makachero waliotumwa kuichunguza Tanzania, kwa lengo la kulinda maslahi ya Rwanda. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mathias Chikawe, amethibitisha kukamatwa kwa wanawake hao, lakini amekataa kuingia ktika undani wa suala hilo.

Habari ipo kwa kirefu gazeti la Jamhuri.
 
Dodoma kuna nini hadi kufanyike ukachero!....hao kina Mtikila na Mama Rwakatare?
 
Hujui kuwa serikali ipo huko kwa sasa.
 
Makechero wakakachero nini ktk nch iliyojaa uchuro km hi?au wamekuja kukachero katiba yetu?acheni hzo uchuro kw kagame.
 
Wewe unaobeza kukamatwa kwa makachero hao ni wanyarwanda watutsi. Watanzania hatupati tabu maana wahutu wanatupatia siri zote bila shaka. Habari nyingine ni pale karagwe wamepanga kwenye guest house fulani na wanashirikiana na baadhi ya walinzi wetu nao majina yanaeleweka karibu tutayavujisha jamii forums intelligence itakapomaliza kazi yake.
 
Anayepinga hii ni mtutsi maana mlipoambiwa mnataka kumuua nyamwasa mlipinga lakini mtu wenu kagame akawathibitishia kwa kauli zake.
 
Taarifa ya uwepo wa makachero hao iliwekwa jf i week ago.
 
Ile taarifa niliyoitoa wiki moja iliyopita kuwa kuna uwepo wa mashushu wa kagame wametinga dodoma ambao wanajifanya machangudoa kumbe siyo imeleta majibu chanya hii ni baada ya kuwekewa mtengo na wakadakwa kama kuku wa kuliwa mwaka mpya. ingawa taarifa ile uongozi wa jamiiforums waliifuta kwa sababu za kuwezesha wakamatwe kirahisi sasa wanyarwanda wanne mbaroni mkoani dodoma kwa taarifa zaidi soma gazeti jamhuri.

Halafu leo ni fools day ulileta issue kama hii watu wanachukulia mzaha tu!!! Na mimi nachukulia mzaha pia!! Napita!!
 
Nipo Dodoma tangu wiki iliyopita na hali ya ulinzi
wa chinichini ilikuwa ya hali ya juu.
Hebu nilifuatilie hili nitawaletea majibu sio muda.
 
Ile taarifa niliyoitoa wiki moja iliyopita kuwa kuna uwepo wa mashushu wa kagame wametinga dodoma ambao wanajifanya machangudoa kumbe siyo imeleta majibu chanya hii ni baada ya kuwekewa mtengo na wakadakwa kama kuku wa kuliwa mwaka mpya. ingawa taarifa ile uongozi wa jamiiforums waliifuta kwa sababu za kuwezesha wakamatwe kirahisi sasa wanyarwanda wanne mbaroni mkoani dodoma kwa taarifa zaidi soma gazeti jamhuri.

kumbe ni changudoa...
 
Halafu leo ni fools day ulileta issue kama hii watu wanachukulia mzaha tu!!! Na mimi nachukulia mzaha pia!! Napita!!
angalia muda aliotuma post yake, foolish day inaisha saa 4.00 asubuhi ndg yangu!!!
 
Kolokoloni umeshiba sana mlo wa mchana, hao wapelelezi waje dodoma kufanya kitu gani pale? Pana kitu gani pale? Kama ni machangu doa nao wamekuja kutafuta ridhiki toka kwa mawaziri wa serikali ya mh chikwete.
 
Hao machangu hawajui viongozi wetu wamejiami kwa silaha za kivita hadi AK 47 chezea Malima wewe
 
Nisikuu sikuu yakugawiana uongo nakutiana presha:-x2 let us enjoy a fool day.
 
Back
Top Bottom