Makaburi yenye kina kifupi - Mauaji ya Familia ya MCStay

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,047
Hiki ni kisa nilichoanza kukifuatilia mwaka 2012, japo familia ilipotea mwaka 2010 na haikujulikana wamekufa au wametoroka hadi mwaka 2013 ambapo mabaki ya miili yao yalipatikana yakiwa yamezikwa jangwani. Baada ya uchunguzi Bw. Charles Merritt ambaye alikuwa rafiki wa Joseph Sr alipatikana na hatia ya kufanya mauaji hayo na kufungwa.

IDx katika kipindi walichokipa jina la Shallow Graves wamepitia upya ushahidi na kesi na hili limeacha mashaka iwapo ni kweli huyu Bwana Charles alitekeleza mauaji hayo. Hata mimi nadhani jamaa hakutekeleza mauaji hayo bali muaji halisi bado anadunda mtaani akitembea kifua mbele kama aliyepigwa ngumi ya mgongo.

mcstay.jpg

Familia ya McStay ilikuwa na maisha kama familia yoyote ile ya Kimarekani wakiishi maisha yta ndoto yao. Joseph Sr ambaye alikuwa kafanikiwa sana kwenye biashara ya kutengeneza water fountains huko California alipenda kutumia muda wake anapokuwa hana kazi akiwa na familia yake aliyeitwa Summer, na watoto wake wawili wa kiume, Gianni (miaka 4) na Joey Jr (miaka 3).

Familia hii ilikuwa imezungukwa na marafiki na ndugu ambao walionekana kuelewana nao vizuri tu. Walipendelea kwenda safari za amtembezi na kufurahia kuona watoto wao wakikua.

Ila ghafla Februari mwaka 2010, familia nzima ikapotea kama moshi unavyopotelea hewani.
Hakuna aliyesikia chochote kutoka kwao au kuwa na dalili zozote za kuonyesha ni wapi walipoenda kwa takribani miaka 4 hadi siku moja mwendesha pikipiki alipokumbana na makaburi yenye kina kifupi katika jangwa la Mojave, ambapo ilikuja kugundulika kwamba makaburi hayo yalikuwa na mabaki ya miili ya wanandoa hao na watoto wao.

Ungunduzi huu ulizidi kuleta matukio ya kushangaza zaidi na kusababisha watu kadhaa kuwa washukiwa ambao wote walikuwa na sababu ya kutaka kuimaliza familia hiyo.

Kulikuwa na watu wengi ambao wangeweza kua na sababu ya kuimaliza familia hiyo na watu wengi wanaamini hili tukio la mauaji halikutekelezwa na mtu mmoja bali zaidi.
Mmoja kati ya washukiwa hao ni Charles Merritt ambaye alishitikiwa na kuhukumiwa mwaka 2019 na hadi sasa anasubiri kunyongwa akiwa gerezani huko California.
Lakini mpaka leo Charles ameshikilia msimamo wake kuwa hakutenda kosa hilo.

How it all started
Siku ya tukio mwaka 2010, Joseph Sr alimpigia simu baba yake na katika mazungumzo alitaja kuwa alikuwa na kikao wakati wa chakula cha mchana. Na hiyo ndio ilikuwa ni mara ya mwisho kuzungumza: hakuna aliyewahi kuwasiliana nao toka tarehe 4 Februari, 2010.

Lakini japo hakuna aliyewasiliana nao, ilichukua muda hadi watu kuanza kuwa na wasiwasi; familia hii mara kadhaa ilikuwa na tabia ya kwenda likizo fupi fupi, hivyo ilichukua zaidi ya wiki kabla ya mdogo wake Joseph Sr, Michael kupita pale nyumbani kwa kaka yake ili kujua kwanini hawapatikani kwenye simu.

Alipoingia ndani alikuta kuna vyakula vinaoza na pia kulikuwa na miwani ya macho ya mke wa Joseph Sr. Hakukuwa na dalili zozote za kuonyesha labda mle ndani kulitokea tukio baya kama kutekwa, mapambano au chochote.

Baada ya kutoa taarifa polisi juu ya kupotea kwa familia hiyo mnamo tarehe 15 Februari, 2010, polisi waligundua kuwa gari la familia hiyo lilivutwa kutoka kwenye maegesho yaliyo jirani na mpaka wa Mexico mnamo tarehe 8 Februari.

Pia waligundua kuwa kwenye kompyuta ya familia hiyo, kulikuwa kuna utafutaji mbalimbali uliofanyika ambao ulihusu jinsi ya kufanya safari kwenda Mexico. Hivyo, mambo hayo yalifanya polisi na watu wenginie kuamini kwamba huenda familia hiyo ilikuwa imesafiri kwenda Mexico. Mkuu wa Idara ya polisi ya San Diego alienda mbali hadi kuweka bango la familia iliyoaminika kuwa ni ya McStay ikivuka mpaka kuingia Mexico. Picha hiyo ilitokana na CCV za mpakani.

Kwa takribani miaka 4, idara ya polisi na watu wengi waliamini kuwa familia hiyo ilikuwa imekimbilia Mexico.
Hili lilibadilika mnamo Novemba, 2013 pale ambapo miili ya wanafamilia wa McStay ilipogundulika ikiwa imezikwa jangwani huku kukiwa na nyundo ya kupasulia miamba pembeni ambayo iliaminika kuwa ndio silaha iliyotumika kuwaua.

Mwaka uliofuata polisi walimkamata Charles, ambaye aliwahi kufanya kazi na Joseph Sr katika biashara yake ya kuunda water fountains. Charles alikuwa na historia ya uhalifu, na ilibainika kuwa alikuwa akiiba pesa kutoka kwenye biashara hiyo. Uchunguzi ulipoendelea ikaja kugundulika pia kuwa simu ya mwisho iliyopigwa kutoka kwenye simu ya Joseph Sr ilikuwa ni kwenda kwa Charles - ambapo simu ya Charles ilionyesha kuwa kwa wakati huo ilikuwa karibu na mnara wa mawasiliano ya simu ambao uko karibu na yalipogundulika makaburi hayo.

Waendesa mashitaka waliwaambia mahakimu kuwa, Charles aliua ile familia baada ya Joseph Sr kumtaarifu kuwa alikuwa anamwondoa kwenye biashara yake; walidai kwamba Joseph Sr aliwaambia marafiki kuwa Charles alikuwa akifanya kazi mbovu na kumwibia pesa.

Charles anapingana na hili akidai kwamba, kulikuwa kuna dalili zote zilizoonyesha kuwa familia hii ilikua imepotea na kwamba yeye alikuwa atoe taarifa kuwa polisi iwapo kama familia ya Joseph ingechelewa kufanya hivyo. Lakini bado alikutwa na hatia na kuhukumiwa kunyongwa.

Lakini kuna watu wengi ambao wanaonekana kuwa wanaweza kuwa washukiwa kwenye hii kesi.

Kulikuwa na mpenzi wa zamani wa mke wa Joseph Sr ambaye alimtumia barua pepe miezi kadhaa kabla ya familia kupotea akimwambia kwamba kuwa atampenda daima. Alikuwa akiishi karibu na walipokuwa wakiishi na aliwahi kukamatwa kwa kutishia kuwaua majirani zake na binti yake mwenyewe.

Pia kulikuwa na mme mpya wa mke wa zamani wa Jospe Sr, mwanaume ambaye alikuwa na historia ya vurugu ambaye aliwahi kumtishia kumfunga mdomo mke wa Joseph na kumpiga Joseph.

Na pia kulikuwa na mshirika wa Joseph katika biashara zake, mtaalamu wa masuala ya kompyuta ambaye alikuwa nidye anaendesha tovuti ya kampuni ambaye aliwahi kutuma ujumbe kwa familia ya McStay akiwatisha kuharibu eneo walilokuwa wakilifanyia kazi na kuharibu biashara yake.

Pia jamaa huyu aliwahi kuweka tangazo kwenye gazeti kuwa anauza biashara ya water fountain wakati haikuwa ya kwake bali Joseph.

Wanasheria waliokuwa wakimtetea Charles wanaona hawa wanaweza kuwa ndio watu wa kuangalia zaidi ila mahakama iliwazuia kuwajadili wakati wa uendeshaji wa kesi ikiwa hawana ushahidi thabiti wa kuthibitisha uhusika wao kwenye mauaji hayo.

Charles mwenyewe anadai kuwa hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kuthibitisha kuwa alihusika katika mauaji hayo. Hivyo waliamua kutumia ushahidi wa kimazingira mwingi ili kuwahawishi mahakimu kuwa ni mimi niliyeingia nyumbani kwao na kuwaua.

Hata hivyo kamera za CCTV katika nyumba ya McStay ziliwaonyesha wanafamilia hao katikati ya usiku wakitoka wenyewe pasipo kuwa na mtu wakapanda gari na kuondoka. Ila ushahidi wa ndani ya nyumba unaonyesha kuwa waliondoka kwa haraka na kuacha chakula mezani.

Hata baba yake Joseph ambaye naye alifanya upelelezi wake binafsi anaamini kuna mtu wa ziada ambaye alihusika. Anasema kuna ushahidi na kila ishara kuwa hata hao watu wengine kwa yeye anavyoona kuna mmojawapo ambaye alihusika.

Pia kuna wanaodai kuwa aliyewaua ni mdogo wake Joseph Sr na mama yake wa kambo anajua na ndio maana walishirikiana kusafisha nyumba ya McStay kabla ya polisi kufika. Wanadai kuwa mdogo wake ambaye anazaliwa na mama yake wa kambo Jospeh Sr alikuwa akimwonea kijicho kwa mafanikio aliyokuwa nayo.

Na ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika pale na alifanya hivyo baada ya kupigiwa simu mara kadhaa na baba yake akimwambia anashindwa kuwapata wanafamilia hao hivyo anaomba aende nyumbani kwao kuangalia nini kinaendela. Lakini hakufanya hivyo kwa siku kadhaa mpaka hiyo siku alipofika hapo na kudai kuwa hakuwakuta.
 
Back
Top Bottom