Makaburi ya Ma-Don na wauza unga wa Mexico

Makaburi ya Ma-Don na wauza unga wa Mexico

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
361,110
Reaction score
831,772
Kwanza lazima utambue kuwa kama kuna kundi hatari duniani kwa ukatili, ubabe na utajiri basi ni makundi ya wauza unga... Hawa ni zaidi ya makundi ya kimafia na kigaidi

Makundi haya huwa na himaya zao na humiliki njia za kupitisha mizigo na huwekeana mipaka. Ole wako ujaribu kuingia kwenye himaya ya mwingine kama huna nguvu hasa.

Makundi haya himaya zao huwa na uongozi kamili na majeshi yake.Yakijumuisha
Walinzi wa mkuu wa himaya
Walinzi wa viongozi wengine
Walinzi wa familia za wanahimaya
Watekaji
Watesaji
Wauaji
Walinda mizigo
Wasafirisha mizigo
Wapokea pesa na wabebaji

Biashara zao hufanyika kwa fedha taslimu na chini ya ulinzi mkali kwa kila upande.

Usipokuwa makini na imara unaweza ukapeleka mzigo na ukaishia kifo ama ukalipa pesa lakini usipewe mzigo... Ni biashara za kibabe na kutoamiana kwa asilimia mia moja.

Wauza unga hawa wana kanuni moja isiyopindishwa na yoyote USALITI NA KUTOA SIRI. Adhabu yake huwa ni moja tuu kifo cha kikatili na mateso makali mno..!!!

Kanuni zao nyingine ni umakini, wepesi wa kutenda, ukamilifu na uthubutu.

Wanaamini katika kupata kila kitu bora kuliko mwingine yoyote
Madon hawa wauza unga wanajifahamu hawana maisha mengi.

Hivyo hupenda kutengeneza pesa ndefu kwa muda mfupi na kuishi maisha ya kifahari kadiri wawezavyo.

Kifo cha risasi moja huwa cha kujivunia zaidi kuliko kukamatwa na makundi pinzani na kuteswa hadi kufa.Huu ni udhalilishaji mkubwa. Hawaogopi kabisa kukamatwa na Serikali

Kwa kuzingatia legacy yao hiyo hupenda hata mazishi yao na makaburi yao kila kitu kiwe cha first class ili wabaki kukumbukwa vizazi na vizazi.

Makaburi yao huwa ya gharama hasa...
Ni makaburi ya nyota tano
Ni makaburi ya ghorofa yenye
Madirisha yasiyopenyeza risasi
Yenye viyoyozi
Yenye satellite TV

Hii yote ni kuonesha nguvu na mamlaka
Kwa sasa anayewika ni mfalme Joacqim Rl-chapo Guzman wa jimbo la Sinaloa..

Nitarejea
Kwenye mji anaotokea huyu bingwa wa sasa ndio kuna makaburi ya kufuru. Ni makaburi yanayojulikana kama makaburi ya nyota tano.

Haya makaburi yana taa automatic zinazowaka masaa 24.. Kama nilivyosema awali security camera hazikosekani masaa yote na hata kama umeme ukikatika kuna backup ya solar.

Baadhi ya makaburi huwa na lounge na makanisa madogo ndani yake. Vyumba maalum ambavyo vyote ni VIP kwa ajili ya wageni. Na mengine huwa na mpaka miti ya Christmas majira yake yanapowadia.

Kitu cha kushangaza kwenye haya makaburi ni kwamba hayaandikwi majina ya marehemu wake. Wala utambulisho wowote. Ni wahudumu wake ndio wenye kufahamu tuu.

Kwahiyo ukienda kichwa kichwa unaweza usirudi.

Asilimia 90 ya wa Mexico ni wakatoliki. Na mmojawapo wa malaika wanaoheshimika na kuabudiwa sana ni Santa mareta ama malaika wa kifo.

Huyu huabudiwa na kuheshimiwa sana mpaka na hawa wazungu wa unga.Wao huamini kuwa malaika huyu wa kifo ana nguvu kuliko malaika wengine wote.

Hii ndio orodha ya top five ya wazungu wa unga waliovuma zaidi.

1. Joaquin Guzman (JO)
2. Pablo Escober 1949- 1993
3. Frank Lucas 1930- 2019
4. Ismai Zambaga Garcia
5. Amado Carrilo Fueten
Halafu kuna mwanamama pekee Griselda Blanco.

*Makala ijayo tutawachambua hawa kwa undani
 
Napenda kutazama channel moja hivi ya CBS REALITY humo utakutana na vipindi kama BORDER SECURITY na kile cha mpakani kati ya Mexico na marekani.

Hawa jamaa wa madawa ni watu wenye akili sana,hasa pale mpakani mwa Mexico jamaa wana kila aina ya technology ila hawaogopi kabisa na jamaa wana ujuzi wa hali ya juu kwenye kusafirisha madawa.Harafu najaribu kuvuta picha na hizi border za kwetu mmmhhhh!!!!
 
Ukirejea mkuu usisahau kunitag
Tayari... Na hizi ni baadhi ya picha... Hapa ni makaburi maarufu ya wazungu wa unga.. Hili eneo linajulikana kama Jardines Del Humaya cemetery... Ukiangalia ni kama Kijiji cha makanisha kumbe ni makaburi... Yaliyofutika wababe na wauaji
NAC1076977ec2c7175_0.jpeg
 
Mshana Jr sijakuelewa hapo uliposema wanaoruhusiwa ni wahudumu, na ukienda kichwa kichwa unaweza usirudi!

Swali, Hao wahudumu wanatoa huduma gani humo? Kuna watu huwa wanatembelea hayo makaburu kama wataliii au ni wahuni wenzao ndio wanaenda kuzuru.?

Vp hali za hizo maiti, zinaharibika au haziharibiki?
 
Kwanza lazima utambue kuwa kama kuna kundi hatari duniani kwa ukatili, ubabe na utajiri basi ni makundi ya wauza unga... Hawa ni zaidi ya makundi ya kimafia na kigaidi
Makundi haya huwa na himaya zao na humiliki njia za kupitisha mizigo na huwekeana mipaka... Ole wako ujaribu kuingia kwenye himaya ya mwingine kama huna nguvu hasa...
Makundi haya himaya zao huwa na uongozi kamili na majeshi yake... Yakijumuisha
Walinzi wa mkuu wa himaya
Walinzi wa viongozi wengine
Walinzi wa familia za wanahimaya
Watekaji
Watesaji
Wauaji
Walinda mizigo
Wasafirisha mizigo
Wapokea pesa na wabebaji
Biashara zao hufanyika kwa fedha taslimu na chini ya ulinzi mkali kwa kila upande... Usipokuwa makini na imara unaweza ukapeleka mzigo na ukaishia kifo ama ukalipa pesa lakini usipewe mzigo... Ni biashara za kibabe na kutoamiana kwa asilimia mia moja...
Wauza unga hawa wana kanuni moja isiyopindishwa na yoyote USALITI NA KUTOA SIRI... Adhabu yake huwa ni moja tuu kifo cha kikatili na mateso makali mno..!!!
Kanuni zao nyingine ni umakini, wepesi wa kutenda, ukamilifu na uthubutu... Wanaamini katika kupata kila kitu bora kuliko mwingine yoyote
Madon hawa wauza unga wanajifahamu hawana maisha mengi... Hivyo hupenda kutengeneza pesa ndefu kwa muda mfupi na kuishi maisha ya kifahari kadiri wawezavyo... Kifo cha risasi moja huwa cha kujivunia zaidi kuliko kukamatwa na makundi pinzani na kuteswa hadi kufa... Huu ni udhalilishaji mkubwa... Hawaogopi kabisa kukamatwa na serikali
Kwa kuzingatia legacy yao hiyo hupenda hata mazishi yao na makaburi yao kila kitu kiwe cha first class ili wabaki kukumbukwa vizazi na vizazi...
Makaburi yao huwa ya gharama hasa...
Ni makaburi ya nyota tano
Ni makaburi ya ghorofa yenye
Madirisha yasiyopenyeza risasi
Yenye viyoyozi
Yenye satellite TV
Hii yote ni kuonesha nguvu na mamlaka
Kwa sasa anayewika ni mfalme Joacqim Rl-chapo Guzman wa jimbo la Sinaloa..

Nitarejea
Kwenye mji anaotokea huyu bingwa wa sasa ndio kuna makaburi ya kufuru... Ni makaburi yanayojulikana kama makaburi ya nyota tano.. Haya makaburi yana taa automatic zinazowaka masaa 24.. Kama nilivyosema awali security camera hazikosekani masaa yote na hata kama umeme ukikatika kuna backup ya solar... Baadhi ya makaburi huwa na lounge na makanisa madogo ndani yake... Vyumba maalum ambavyo vyote ni VIP kwa ajili ya wageni... Na mengine huwa na mpaka miti ya Christmas majira yake yanapowadia....

Kitu cha kushangaza kwenye haya makaburi ni kwamba hayaandikwi majina ya marehemu wake... Wala utambulisho wowote... Ni wahudumu wake ndio wenye kufahamu tuu ... Kwahiyo ukienda kichwa kichwa unaweza usirudi....

Asilimia 90 ya wa Mexico ni wakatoliki.... Na mmojawapo wa malaika wanaoheshimika na kuabudiwa sana ni Santa mareta ama malaika wa kifo... Huyu huabudiwa na kuheshimiwa sana mpaka na hawa wazungu wa unga... Wao huamini kuwa malaika huyu wa kifo ana nguvu kuliko malaika wengine wote....

Hii ndio orodha ya top five ya wazungu wa unga waliovuma zaidi..

1. Joaquin Guzman (JO)
2. Pablo Escober 1949- 1993
3. Frank Lucas 1930- 2019
4. Ismai Zambaga Garcia
5. Amado Carrilo Fueten
Halafu kuna mwanamama pekee Griselda Blanco....

*Makala ijayo tutawachambua hawa kwa undani
Asante sana mkuuu
 
Back
Top Bottom