Ni rahisi sana kumshauri mtu waachane na mwenzi wake. Lakini unaweza ukapitia the Same situation kama aliyopitia huyo mwenzako na ukashindwa kumwacha mpenzi wako. Kutoa ushauri ni rahisi sana, ila yakikukuta utashangaa unashindwa hata kujishauri mwenyewe. Ikifika muda wa kufanya maamuzi magumu,
Mshirikishe Mungu na akili yako tu. Wale watu wa muhimu utawapa taarifa tu kuwa imekuwa hivi
Sio kitu kizuri pia kusimulia matatizo yenu kwa watu wengine. Kuna Vitu tunatendewa na wenzi wetu ambavyo tukivisema kwa watu vinatudhalilisha sisi pamoja na wenzi wetu. Au vitafanya wenzi wetu wasiheshimike. As long as Mpo pamoja, basi siri zenu fichianeni