BRELA
Govt Institution
- Dec 14, 2023
- 109
- 84
Watumishi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamepatiwa mafunzo kuhusu magonjwa sugu yasiyoambukiza mahala pa kazi pamoja na afya ya akili, leo tarehe 4 Julai, 2026 katika Ukumbi wa Hazina jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yameambatana na zoezi la upimaji wa afya kwa watumishi, lililofanywa na wataalamu kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI).
Lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia watumishi kupata uelewa kuhusu magonjwa sugu yasiyoambukiza na afya ya akili mahala pa kazi, ili waweze kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza, kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi pamoja na kuzingatia afya zao wakiwa kazini na katika maisha yao ya kila siku.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo kuhusu baadhi ya dalili na visababishi vya msongo wa mawazo, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka MOI, Bi. Stellah Kihombo amesema dalili za msongo wa mawazo hujidhihirisha kupitia mabadiliko ya hisia na tabia.
Amefafanua kuwa baadhi ya visababishi vya msongo wa mawazo ni pamoja na changamoto za mahusiano na matatizo ya kifamilia, hivyo amewashauri watumishi kuchukua hatua za mapema kama vile kuwahi kupata ushauri wa wataalamu wa afya ya akili kabla ya tatizo kuwa kubwa zaidi.
BRELA imekuwa ikiwapatia watumishi wake mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha wanakuwa imara na timamu wakati wote na yale ya kuwajengea uwezo mahala pa kazi.