Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 34,637
- 37,959
Huwezi maliza shida za watu.. Kwanza, hata zako tu hutaweza zimaliza mpaka siku unaingia kaburini ndo zitaisha..!!Habar Zenu
Mwenzunu nimejikuta kwenye wimbi la mawazo Baada ya kuelemewa na majukum. Baada ya Kupata kibarua nimejikuta napokea simu nyingi kuhusu Matatizo ya kifamilia
Nimejitahid sana kutatua Matatizo Kwa kadri ya uwezo wangu lakini mambo yanazidi kuwa magumu.
Ukiachana na kuhudumia familia Yangu lakini shida za Ndugu zimekuwa haziishi
Zinapokaribia tarehe za mwisho wa mwezi najikuta sina raha Kabisa maana napigiwa simu nyingi za shida na kuombwa pesa tu
Naombeni mbinu ya kukabiliana na changamoto hizi
Fanya haya;
1. Usimpe mtu hela mara tu baada ya kukuomba utawazoesha hivyo, unless otherwise shida hiyo iwe inauwa
2. Usiwe mtu wa kutoa kiasi kamili kilichoombwa, by the way, hakuna anayejua mfuko wako upoje zaidi ya wewe mwenyewe
3. Kumbuka, ndugu hawawasiliani kwamba huyu ameshakuomba, mwingine akupe muda ndo aombe. Kila mmoja anakulilia shida zake kwa namna yake, na wakati mwingine utakutana na watu zaidi ya wawili wote wanakulilia shida
4. SIku moja moja na wewe walilie shida, kila atakayekunyima ndo kakupa tiketi ya wewe nawe kumnyima. Lia shida hata kama huna shida kweli
5. Kumbuka pia humsaidii mtu kwa vile ni nduguyo, BALI KWA VILE ANA SHIDA. Undugu wenu usije ukatumika kukufirisi