sinajinasasa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 2,989
- 4,130
Mwambie akimbie mji aende kuishi peke yake huko na tembo.Huyu jamaa yangu amejikuta kwenye dimbwi zito la Mawazo anaomba ushauri
Ana miaka 37 ameoa ana mke na watoto watatu ,ana watoto wa mdogo wake wa kike watatu
Mdogo wake wa kike alizalia nyumbani na alikimbia nyumbani na kuwaacha watoto wake ,ili kupunguza shida kwa wazazi akaamua kuwachukua
Anamlaumu baba yake kwa maisha wanayoishi kwa sababu zifuatazo
Aliajiriwa kama dreva kwenye makampuni ya usafirishaji,lakini hakuwekeza sehemu yoyote ,hakununua ardhi yoyote,hakujenga nyumba yake ya kudumu,hakuwekeza hata kwenye biashara ,alichoambulia ni pombe na wanawake akaambulia ugonjwa wa kisasa
Mama yake yeye ndiye alkuwa anajitahidi kuwahudumia wakati baba yao akishindia baa
Familia sasa ni maskini kweli kweli,kwa juhudi za mama huyo jamaa yangu akajitahidi akasoma akapata kazi serikali za mitaa ingawa mshahara ni mdogo ila anajitahidi kuwahudumia wazazi wote .
Sasa hivi amejikuta katika msongo wa mawazo mazito ambayo yanahitaji tiba haraka sana
Anasema ndo ameanza kujenga pamoja na mshahara huo mdogo maana familia inakua lakini anajikuta anazidiwa ..Pamoja na kuanza kujenga nyumba yake wazazi wanapinga kujenga kwa sababu wazazi wanadai awajengee kwanza kabla hajaanza kujenga nyumba yake
Anasema kila mwezi alkuwa anawanunulia wazazi wake mahitaji na familia yake,alipoanza kujenga kuna vitu vimepungua hasa kwa wazazi wake (huduma)
Mbaya zaidi mama yake anaumwa ugonjwa wa kuvimba viungo vya mwili,ikabidi akope amtibu mama yake
Hata mwezi haujaisha baba naye anaumwa hali yake imedhoofika kwa sababu ana ugonjwa mwingine wa kisasa,na mbaya zaidi baba yake ameenda kukaa kwake akimwambia huyo kijana wake ampeleke hospital anajiskia vibaya mnooo
Na wakati huo huo zimebaki wiki chache mke wake ajifungue
Mpe jamaa ushauri ,afanyeje na hela hana ...ana familia ya watu watu 7 ina maana watoto watatu na mke wake,watoto wa dada yake wapo watatu na wazazi hao wanamtegemea asilimia mia na wanaumwa tena magonjwa makubwa anafanyaje?
Nawatahadhalisha vijana mnaokwenda kuoa sasa hivi, mjihadhari na kupata watoto...utakuwa na shida hadi kaburini..
Ingekuwa kuna switch ya kuzima via vya uzazi ningevizima ili nisiweze kupata watoto, nyege ndo adui yetu mtamu!!!