Majukumu ya familia yamekuwa makubwa kuliko kipato chake, mpe ushauri

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
667
1,795
Huyu jamaa yangu amejikuta kwenye dimbwi zito la Mawazo anaomba ushauri.

Ana miaka 37 ameoa ana mke na watoto watatu ,ana watoto wa mdogo wake wa kike watatu.

Mdogo wake wa kike alizalia nyumbani na alikimbia nyumbani na kuwaacha watoto wake ,ili kupunguza shida kwa wazazi akaamua kuwachukua.

Anamlaumu baba yake kwa maisha wanayoishi kwa sababu zifuatazo.

Aliajiriwa kama dreva kwenye makampuni ya usafirishaji,lakini hakuwekeza sehemu yoyote ,hakununua ardhi yoyote,hakujenga nyumba yake ya kudumu,hakuwekeza hata kwenye biashara ,alichoambulia ni pombe na wanawake akaambulia ugonjwa wa kisasa.

Mama yake yeye ndiye alkuwa anajitahidi kuwahudumia wakati baba yao akishindia baa.

Familia sasa ni maskini kweli kweli,kwa juhudi za mama huyo jamaa yangu akajitahidi akasoma akapata kazi serikali za mitaa ingawa mshahara ni mdogo ila anajitahidi kuwahudumia wazazi wote.

Sasa hivi amejikuta katika msongo wa mawazo mazito ambayo yanahitaji tiba haraka sana.

Anasema ndo ameanza kujenga pamoja na mshahara huo mdogo maana familia inakua lakini anajikuta anazidiwa. Pamoja na kuanza kujenga nyumba yake wazazi wanapinga kujenga kwa sababu wazazi wanadai awajengee kwanza kabla hajaanza kujenga nyumba yake.

Anasema kila mwezi alkuwa anawanunulia wazazi wake mahitaji na familia yake,alipoanza kujenga kuna vitu vimepungua hasa kwa wazazi wake (huduma).

Mbaya zaidi mama yake anaumwa ugonjwa wa kuvimba viungo vya mwili,ikabidi akope amtibu mama yake.

Hata mwezi haujaisha baba naye anaumwa hali yake imedhoofika kwa sababu ana ugonjwa mwingine wa kisasa,na mbaya zaidi baba yake ameenda kukaa kwake akimwambia huyo kijana wake ampeleke hospital anajiskia vibaya mnooo.

Na wakati huo huo zimebaki wiki chache mke wake ajifungue.

Mpe jamaa ushauri ,afanyeje na hela hana ...ana familia ya watu watu 7 ina maana watoto watatu na mke wake,watoto wa dada yake wapo watatu na wazazi hao wanamtegemea asilimia mia na wanaumwa tena magonjwa makubwa anafanyaje?
 
Sasa akijinyonga hao watoto itakuwaje?

Apambane tu kuna watu wana shida zaidi yake lakini bado wanapambana tena wana matumaini makubwa.
 
Ila kusema kweli kila mtu ana breaking point yake.

Mwenyewe sometimes nacheki pichaaa naoma kama madrama drama tu
Mkuu ni hali halisi huyu jamaa anayokumbana nayo,kama hapa anawaza baba yake ni kweli ni mgonjwa na hana hela na mbaya Mzee kaja kukaa kwake akimshinikiza ampeleke hospital, ungekuwa wew unafanyaje kwa mfano na huku ukumbuke siku si nyingi ametoka kumuuguza mama yake na mama yake bado hajapona kuna madawa inapaswa awe ananunuliwa dah!!!
 
Mwambie afungue biashara ndogo ndogo kama vile kuuza vitumbua maandazi Na Chai Na chakula itasaidia kupata Hela ndogo ndogo Kwa ajili ya kupunguza ukali WA gharama ZA maisha... Biashara HII isimamiwe Na Hao watoto wa kike anao walea hapo kwake
 
kujinyonga ni udhaifu ni kusalimu pambano,hata jeshini aliyejinyonga hazikwi kwa heshima ya kijeshi maana ni mwoga.

mwambie sifa ya mwanaume ni kukaza,hamna mwanaume mwenye maisha laini,tunacheka sababu tunaamini kuna jua litachomoza tena,hata mashoga wanapata tabu sana.
 
Sasa akijinyonga hao watoto itakuwaje?

Apambane tu kuna watu wana shida zaidi yake lakini bado wanapambana tena wana matumaini makubwa.

ubinafsi unamsumbua anajiangalia yeye tu,wanasema hivi wasemaji.
unazo sababu billioni za kutabasabu,kwa sababu tabasamu lako linaamsha matumaini kwa wengine,huyu jamaa hawazi siku yuko ndani ya jeneza,huo msururu utafarakana kwa style gani!!!
 
Sasa akijinyonga hao watoto itakuwaje?

Apambane tu kuna watu wana shida zaidi yake lakini bado wanapambana tena wana matumaini makubwa.

ubinafsi unamsumbua anajiangalia yeye tu,wanasema hivi wasemaji.
unazo sababu billioni za kutabasabu,kwa sababu tabasamu lako linaamsha matumaini kwa wengine,huyu jamaa hawazi siku yuko ndani ya jeneza,huo msururu utafarakana kwa style gani!!!
 
Mwambie afungue biashara ndogo ndogo kama vile kuuza vitumbua maandazi Na Chai Na chakula itasaidia kupata Hela ndogo ndogo Kwa ajili ya kupunguza ukali WA gharama ZA maisha... Biashara HII isimamiwe Na Hao watoto wa kike anao walea hapo kwake
Mkuu watoto hao wa mdogo wake ndo wa kwanza yupo darasa la pili,na wengine chekechea,hivyo hawawezi kufanya chochote,pia ujue nao wanatakiwa wasome,wale,wavae na watibiwe,si kutoka kwa mtu mwingine wanamungalia uncle yao
 
Haina kukata tamaa, mwanaume ni kupambana hadi tone la mwisho. Afikirie akijinyonga hiyo familia anataka ifanye nini akiiacha?. Ajitahidi kuwa na vyanzo vingine vya mapato vya mtaji mdogo mdogo tu vinatosha. Afu mwambie siye yeye tu mwenye changamoto ni wote tuna changamoto zetu, tena inawezekana tukimsimulia ataona yeye ana nafuu. tunapambana hivo hivo.
 
Hao wazazi watuliee.

Wao waliwajengea wazazi wao???

Badala yakumpa Kongole Kijana wao, wao wanataka kumdidimiza..

Yaan una mke, watoto ,usiwatizame hao,uanzie wazazi kwanza??????.!!!

Maajabu sana !!!... Familia za Kimasikini ni tabu tupu !!!
 
ubinafsi unamsumbua anajiangalia yeye tu,wanasema hivi wasemaji.
unazo sababu billioni za kutabasabu,kwa sababu tabasamu lako linaamsha matumaini kwa wengine,huyu jamaa hawazi siku yuko ndani ya jeneza,huo msururu utafarakana kwa style gani!!!

Kabisa yani kujinyonga ni ubinafsi.

Ana watoto wanamtegemea

Ana wazazi wanamtegemea

Ndugu pia anao apambane tu maisha haya kila mtu ana majanga yake.
 
Kujinyonga ni ujinga na ubinafsi mkubwa kwako na kwa familia hamna asiyepitia changamoto baba, tena huyo wakujinyonga mjinga alipata hela akawekeza kwenye papuchi kavuna ngoma why ajiue Sasa watoto wawe yatima let's be responsible for our mistakes and correct it, sio kutafta solutions zisizo zaa matunda bana.
 
Back
Top Bottom