Majukumu mawili ya kifamilia nisiyoyapenda...

mpasta

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
917
1,997
Wadau nirukie moja kwa moja kwenye mada.

Nina mke na watoto wadogo. Nikiwa Home namsaidia mke wangu kazi mbalimbali, kama kupika, kuogesha watoto, kusimamia Home Work za shule, etc

Lakini mambo mawili siyapendi kabisa.

(1) Kupeleka mtoto hospitalini
Hapo panakuwa pagumu sana kwangu, nitaenda iwapo mke wangu akiwa na dharura lakini kama yupo free basi mie ndio nitatafuta dharura ya uongo na kweli ili miradi nisiende hospitali.

(2) Sipendi kwenda shuleni kwa mtoto kuhudhuria vikao vya shuleni au kupokea ripoti
Nishawahi kuhudhuria siku za nyuma unakuta mnapoteza saa 3 kwa ajili ya kikao kisicho na kichwa wala miguu, porojo kibaoo.Tokea hapo sihudhurii namtuma tu Shemeji yangu aende au mke wangu akiwepo anaenda yeye.

Je, mwenzangu wewe hupendi majukumu gani ya kifamilia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom