Elections 2010 Majukumu Makuu ya CHADEMA

Edwin Mtei

Senior Member
Dec 13, 2008
181
342
Nilipofunga kompyuta yangu asubuhi leo ili nishughulikie mambo binafsi yanayoniletea kipato, nilikuwa nimechangia kwa ufupi topic kwamba "Watanzania si Mabwege" any more. Mhe. Kinana alikuwa amenukuliwa au alijieleza kuhusu misimamo ya chama chake cha CCM, kwamba WaTz. si mabwege, na eti Chadema wanadhani hivyo, kwa kuteua mgombea mwenza asiye na degree.

Kama Muasisi wa Chadema, nilisisitiza ni jukumu la Chadema hasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi, kufichua uoza wa CCM na kuonyesha weaknesses za viongozi wao, tukiwataja majina pale tulipo na ushahidi. Hiyo ndio demokrasia. Tunahitaji ujasiri na uzalendo ili wananchi wapate viongozi adilifu.

Nilipofungua kompyuta baadaye nilimkuta Mhe. Kinana akizunguzia Chadema 'Kupotoka' kwa kutaja watu ambao kesi zao za ufisadi ziko mahakamani. Kinana namheshimu sana kwa vile amepata kuongoza wizara nyeti serikalini kama mimi. Lakini serikali wakati wetu, ikimshutumu mtu yeyote, ingeshauri CCM ya wakati huo isimteue Mgombea! Sisi Chadema tunasema "Mafisadi pamoja na Watuhumiwa wa ufisadi Ziiiiii". Watanzania msikubali kupotoshwa na wakina Kinana Oktoba 2010. Hawakubaliki!

Nataka kuongezea kuwa jukumu jingine kuu la Chadema sasa ni kujiandaa kuchunga kura tutakazopigiwa na Watanzania wanaoridhika kwamba sisi ni chama m'badala wa CCM na kwamba Dk. Slaa atafaa zaidi kuliko Kikwete.

Ni lazima kila kituo cha kupigia kura kiwe na wakala wetu shupavu, mkali na jasiri. Ahakikishe ni mpiga kura stahiki tu anapiga kura, na mara moja tu. Ujanja wa CCM kuleta watu wao kurudia kupiga kura, au kununua vitambulisho ili wapenzi wetu washindwe kupiga kura vifichuliwe mapema. Hakuna kulala, mpaka kieleweke.

Namalizia kuwatahadharisha wananchi wenzangu kwamba yaliyotokea pale Jangwani juzi, ambapo wafanyakazi wa TBC walirushiwa mawe na wapenzi wa Chadema wakati TBC walipositisha matangazo 'live' ya mkutano wao, yanaashiria uvumilivu wa WaTz. unafikia kikomo.

Endapo dalili za kutumia vyombo vya umma, kama TBC, ili kuhujumu au kukandamiza upinzani halali zitaendelezwa na serikali, CCM na viongozi wake watabeba lawama kwa lolote litakalotokea. Mimi binafsi nashauri wapenzi wa Chadema wawe watulivu na wapenda amani. Lakini wenye uwezo wa kuepusha vurugu ni wale walio madarakani sasa.

Ahsanteni
 
Nataka kuongezea kuwa jukumu jingine kuu la Chadema sasa ni kujiandaa kuchunga kura tutakazopigiwa na Watanzania wanaoridhika kwamba sisi ni chama m'badala wa CCM na kwamba Dk. Slaa atafaa zaidi kuliko Kikwete.

Ni lazima kila kituo cha kupigia kura kiwe na wakala wetu shupavu, mkali na jasiri. Ahakikishe ni mpiga kura stahiki tu anapiga kura, na mara moja tu. Ujanja wa CCM kuleta watu wao kurudia kupiga kura, au kununua vitambulisho ili wapenzi wetu washindwe kupiga kura vifichuliwe mapema. Hakuna kulala, mpaka kieleweke.

maneno muhimu sana mzee... watu wanachakachua hadi kura!!!
 
Baba! Kumbe uanamapinduzi sio kwa vijana tu! Oneni huyu shujaa! Umenena Baba! Mzee mwenzako Malecela angeweza naye kuthubutu kukemea ufisadi kwa nguvu kama hizi mapambano yangekuwa mbali.
 
Ahsante sana Mzee Mtei,

Ndiyo maana vijana wote wenye akili wanakubali na kutambua kuwa wazee ni tunu inayohitaji kulindwa na kwamba tunawahitaji sana. CHADEMA na watanzania wanaoitakia mema nchi hii bado wanahitaji mchango wako na wenzio. Mungu awalinde na kuwazidishia hekima.

DC
 
Umenena babu yetu,Ushauri wako ni wa kina na sisi vijana wa taifa hili tunalichukua kama lilivyo kwa utekelezaji wa vitendo.Nina uhakika huna shida na pesa za walalahoi,wewe ni tajiri lakini unapigania maslahi ya watanzania walio wengi walio katika lindi la umaskini wa kutupwa.Sababu tunazo ni hizi hapa:

  1. ELIMU BURE MPAKA CHUO KIKUU
  2. UONGOZI BORA
  3. MIUNDOMBINU YA MAJI,BARABARA
  4. SIASA SAFI ZA KWELI NA SI UONGO UONGO
  5. N.K .. N.K..
 
Tuko pamoja Mzee, mpaka kieleweke. Kinana anatambua wazi kwamba anachokisema sio sahihi lakini yeye ndiye anayedhani kwamba waTz bado wamelala usingizi. Anajidanganya. Subiri tuwaduwaze Oktoba 31.
 
Asante sana Mzee wetu, hapa hakuna la kuongeza, umemaliza kila kona. Binafsi umenigusa sana kwenye jukumu lingine ambalo chama limeona kuwa ni la msingi kufanyiwa kazi. "kulinda kura baada ya kupigwa". Kweli hili lilikuwa ni tatizo sana kwangu. Maana kwa kuchakachua tu, CCM wanajulikana.

Asante sana mzee na MUngu akulinde!
 
mzee umenena....akina malecela chaliiiiiiiiiii......hongera kwa kuamua kukaa pembeni na kuwashauri vijana wako kufikiri namna ya kuwakomboa watz kutoka lindi na tope hili baya la umasikini uliokithili.....TUPO PAMOJA MZEE WETU
 
Asante sana Baba! Hivi najiuliza ingekuwa ni CCM walisema chochote kwa wapinzani au kubeza kama ilivyo desturi yao je hao TBC wangeacha kurusha matangazo hayo? Nilishasema kuwa TBC na redio zake ni kibaraka cha CCM. Sasa Chadema itakapoingia ikulu wao watamtumikia nani? Kwa uelewa wangu TBC ni ya serikali na serikali si chama tawala tu, bali hata wale wananchi ambao wako katika makundi ya vyama na wale ambao hawana vyama. Shameful TBC1.
 
Nataka kuongezea kuwa jukumu jingine kuu la Chadema sasa ni kujiandaa kuchunga kura tutakazopigiwa na Watanzania wanaoridhika kwamba sisi ni chama m'badala wa CCM na kwamba Dk. Slaa atafaa zaidi kuliko Kikwete.

Ahsanteni

Mzee Mtei;

Ni vema kuwa kuanzia Kipindi hiki CHADEMA ikaanza kujijengea "mtandao wa watu" kuanzia mitaani tunamoishi. CCM wana mfumo wa nyumba 10 na wote tunajua kuna mtu anaitwa balozi au mjumbe.

Mitaani kwetu kuna bendera luluki za wajumbe hawa.

CHADEMA ni vema ibuni mfumo sambamba na wa CCM au bora zaidi ili waweze kushinda.

Pili, tumia uzoefu wako na busara yako kuunganisha nguvu na vyama vyenye Nguvu. Chama kama CUF kama mtafanikiwa kitabalance vema.

Najua wasiwasi uliopo wa kutoa kuaminiana na kila chama kukituhumu kingine kuwa ni wakala wa CCM. Propaganda zilizopo kuwa CUF ni chama cha Waislam na wapemba na Chadema ni Chama cha Wakristo na Wachaga zinaweza tu kuepukika kwa nyie kupita vikwazo vyote, kuweka ubinafsi pembeni, maslahi ya taifa mbele na kuungana.

Ninayo imani kuwa kama uliyoyagusia na haya machache yakizingatiwa, come October and 2015 CHADEMA inaweza kuongoza Nchi.

Ieleweke kuwa wengine tunaamini maendeleo yatakuwepo kama kutakuwa na upinzani wa kutosha Bungeni hata kwa level ya 50-50%.
 
Kwenye mkutano mmoja watu waliambiwa wawe na simu za mkono kupiga picha matokeo ya kura yanayobandikwa kwenye vituo vya kura na kutuma sehemu moja kwa njia yamtandao hilo ni moja pili kwa kutumia FOS friends of Slaa - Movement 4 Change kunatakiwa kuwa na wawakilishi tanzania nzima watakaosimamia kufuatilia na kutoa taarifa za zoezi la uchaguzi kuanzia kampeni za slaa mpaka kwenye upigaji kura.http://groups.google.com/group/friendsofslaa?hl=sw&pli=1
 
Akhsante sana mzee wetu, tunakushukuru sana kwa maneno ya busara kama hayo.
 
Asante sana Baba yetu kwa busara zako, ningependa kuongezea kidogo suala la usimamizi wa vituo wakati wa kupiga kura na kuhesabu CHADEMA kama CHADEMA inajua watu wake walio makini ambao hawadanganyiki kuwateuwa kama ndio viongozi wa swala zima la usimamizi wa uhesabuji wa kura na pia mkatoa mafunzo kwa wasimamizi wa CHADEMA kwa kina zaidi (kiundani ) ili wajue ni jinsi gani wataweza kuwamudu hao wanapenda kuchakachua kura zetu.

Elimu ya kutosha juu ya usimamizi na madhara ya udanganyifu nadhani itakuwa silaha tosha kwetu kujua ni jinsi gani tunakuwa makini na hawa mafisadi wanaopenda kuchakachua kura zetu.
 
Maneno mazito sana haya.......!

Hata na hivyo, huko kwenye kampeni wanakampeni wajitahidi kuwahimiza wale wote waliojiandikisha kupiga kura kufanya hivyo tarehe 31.10.2010! Watu wengi huwa wanashabikia na kupenda mageuzi lakini hufikiri labda mageuzi yanaletwa nje ya box la kupigia kura tena na watu wengine....kumbe kila mmoja anayependa mageuzi na maendeleo ya kweli.....ni kuunganisha nguvu kwa kutumia vema MABOX tarehe 31.10.10!
 


Namalizia kuwatahadharisha wananchi wenzangu kwamba yaliyotokea pale Jangwani juzi, ambapo wafanyakazi wa TBC walirushiwa mawe na wapenzi wa Chadema wakati TBC walipositisha matangazo 'live' ya mkutano wao, yanaashiria uvumilivu wa WaTz. unafikia kikomo.

Endapo dalili za kutumia vyombo vya umma, kama TBC, ili kuhujumu au kukandamiza upinzani halali zitaendelezwa na serikali, CCM na viongozi wake watabeba lawama kwa lolote litakalotokea. Mimi binafsi nashauri wapenzi wa Chadema wawe watulivu na wapenda amani. Lakini wenye uwezo wa kuepusha vurugu ni wale walio madarakani sasa.

Ahsanteni

mzee hapa umesoma alama za nyakati
uvumilivu wa waTZ unafika mwisho
 
Kwenye mkutano mmoja watu waliambiwa wawe na simu za mkono kupiga picha matokeo ya kura yanayobandikwa kwenye vituo vya kura na kutuma sehemu moja kwa njia yamtandao hilo ni moja pili kwa kutumia FOS friends of Slaa - Movement 4 Change kunatakiwa kuwa na wawakilishi tanzania nzima watakaosimamia kufuatilia na kutoa taarifa za zoezi la uchaguzi kuanzia kampeni za slaa mpaka kwenye upigaji kura
Asante sana mzee wetu muasisi wa Chadema,

Kama ulivyosema jukumu mojawapo la Chadema kwa sasa ni pamoja na kulinda kura, kama alivyoshauri Shy hapo juu, FOS ipewe jukumu hilo kwa vile inafika nchi nzima. Nionavyo mimi kwa tanzania tatizo haliko kwa wapiga kura, wapiga kura wamekuwa wakipigia upinzani tangu 1995 lakini kura zao zimekuwa zinaibiwa.

Mnaweza kufanya kampeni kubwa na nzuri lakini matokeo yake kura zikaibiwa. Kama mna bajeti ya kampeni, sehemu kubwa ielekezwe kwenye kulinda kura, kuwapata mawakala wazalendo kwa kila kituo pamoja na kuwawezesha vinginevyo wanaweza kununuliwa na wapinzani wenu.

Maeneo ambayo nina wasiwasi nayo kura nyingi kuibiwa ni ya Kusini kwa vile CCM wanajua Chadema haijafika maeneo hayo basi itatumia hiyo loop hole kuonyesha sehemu hizo wamejitokeza wapigakura wengi kuzidi waliotarajiwa say 120% ili waweze kupata kura zaidi zinazoweza kujaza sehemu itakaposhindwa kuiba.

Kwa hiyo hata kama sehemu fulani Chadema haitaweka mgombea ubunge au hata diwani ni muhimu kuweka wakala wenu. CCM hutumia mbinu ya kuwa na wakala mmoja tu wa CCM kuandika idadi yeyote ya wapiga kura waliojitokeza.

Nimeyataja maeneo hayo kwa vile nakumbuka mwaka 1995 kwa macho yangu kura za mikoa hiyo zilipigiwa Dar es salaam na masanduku yaliyojaa kura yalionekana Uwanja wa ndege wa zamani usiku baada ya kura kupigwa yakipelekwa mikoa hiyo kwa ndege ndogo za kukodi.
 
Asante mkuu wa Kazi, mwaka huu hata sisi ambao hatujawahi kupiga kura hata mara moja TUMO mpaka kieleweke, tushachoka na mfumo butu ulioshidwa kuleta maendeleo ya nchi, kilichobakia kwao CCM ni AHADI kila kukicha, tumeshasikia nyingi sana. Sasa nachosema muda wa ahadi umeshapita sasa tunataka MATENDO na DR. Slaa ndiyo jibu letu.
 
Back
Top Bottom