Major general Suheil el Hassan, jasiri, mbabe, wanavita, mwanasaikolojia, na Rambo halisi wa kivita vitani Syria

SEHEMU YA TATU
Haya sasa ile siku ndio leo! Mambo vipi wanajf. Binafsi niko poa kama wasemavyo vijana wa kitanzania. Siku zinakimbia sana mwaka ndio huoo! Ni kama unainama siku zitembee. Kifo nacho chaja. Haya bwana huo ni utangulizi tu wa hadithi yetu juu ya Meja jenerali Suheil Al Hassan.

Huyu kamanda Suheil El Hassan akaanza kushangaza wengi kwa mbinu na tabia zake vitani. Tofauti na makamanda wengi wa Kisyria huyu Colonel Suheil El Hassan ( akiwa canali kipindi hicho) akaagiza maiki na speaker kitu cha ajabu vitani. Speaker ? Ya nini sasa? Hizi speaker alizoagiza zilikuwa zenye uwezo wa sauti yake kupenya umbali mrefu sana.

Basi Suheil El Hassan na kikosi chake hiki wakaanza kutembea na speaker hizi katika mission zao . Baadae wakuu wake wakagundua Kwamba speaker zilikuwa maalum kwa ajili ya kuwaimbia maadui zake mashairi ya kutisha sana. Al Hassan huwakanya kwamba wasijaribu kupigana nae kwani wataangamia vibaya.

Pia huwaomba wakumbuke watoto wao na familia zao kwa mara ya mwisho kwani muda wao wao wa kufa umefika Kama hawatasalimu amri. Hii kwa kichaga huitwa Psychological Warfare.

Yaani kuwapiga maadui kwa maneno magumu ya kupukuchua nati za mioyo yao. Na Ni kweli kwa namna hii mara kadhaa waasi walisarenda kwa hofu ya nguvu ya gharika ya mabomu ya kanali Hassan. Mfano kule Allepo na Eastern Ghouta waasi wengi walisarenda kwa wingi kuepuka hasira ya Al Hassan.

Haya sasa katika mwaka 2013 jiji karibu lote la Allepo lilishaangukia mikononi mwa waasi wa Syria. Waasi walikuwa wameteka jiji hilo na hivyo kukata mawasiliano ya barabara ya kijeshi na kiraia kati ya Allepo na eneo la ukanda wa kati wa Syria. Kutokana na jambo hili basi Colonel Suheil El Hassan akapewa jukumu la kuhakikisha kwamba supply line kutoka Allepo na central Syria inarudi mikononi mwa Serikali . Operation dhidi ya waasi hawa ikaitwa Operation Canopus Star. Hii ni moja ya operation ngumu zaidi iliyowahi kutokea katika vita ya Syria.

Waasi waliposikia hili la offensive operation dhidi yao na kamanda ajae wa operation hiyo dhidi yao hofu ikawatawala sana. Wakizungumzia jambo hili dhidi ya kanali Hassan walisema kwamba El Hassan wanamjua na kwa jina la mola hatashinda.

Ilipofika ile siku ya operation,, ndege vita vita za Kisyria zilianza kupiga maeneo yote yaliyosemekana kuwa ngome za waasi. Kwa masaa 48 angani ilikuwa ni makombora yakivurumishwa kutoka ndege Vita za kirusi su 25 frog foot, su 24 fencer . Ndege zikawaminya waasi vilivyo. Wasiopatwa na makombora wakafukiwa na majengo yaliyodondoka. Waswahili wana msemo wao vita havina macho. Ni kweli hata wasio waasi yaani wananchi wakaangamia vibaya.

Unaambiwa kwa siku mbili yalianguka mabom 3000 ndani ya jiji la Allepo. Allepo ya maghorofa ikawa ni magofu ndege zilifanya uasi , si tu dhidi ya wananchi wasio hatia na waasi bali hata kwa maghorofa. Ohh ile Syria nzuri ilikua inaangamia waso huruma walifanya kiitwacho capet bombing yaani kusafisha na kushusha kila kilichosimama.

Siku ya tatu ilikuwa siku ya kanali Hassan. Alipofika tu uwanja wa Vita akawahamasisha vijana kupigana dhidi ya vibaraka wa Ulaya na Marekani. Akaomba kipaza sauti halafu akakiinua juu na akaanza kuimba mashairi mazito akisema..

" Ile siku mbaya ya kijana mpenda mashairi imefika. Mimi ndio yule mtu hatari mwenye moyo wa chuma. Isitoshe nina fikra pana ya kuwamaliza wote msiposarenda. Lakini pia mimi ni mpole kama bahari tulivu mkinielewa. Mimi kwa jina langu huitwa colonel Suheil Al Hassan. The Tiger"

Baada ya hapo kama hakuna kusarenda Kanali Hassan huingia rasmi kama ambavyo Rambo hufanya vitani. Kushambulia bila kukoma. Kupigana kufa na kupona.

Kwa nguvu yake ya ushawishi na morali kikosi chake kikapigana kufa na kupona mjini Allepo. Wakafanya operation ya nyumba kwa nyumba kuwasaka wabishi. Baada ya wiki moja na siku tatu jeshi la Syria likashinda kwa kishindo na hivyo Alepo ikakombolewa huku operation ikiacha makovu ya raia 248 kufa vitani.

Je ilikuwaje mpaka kanal Hassan akatambulika hadharani? Moja kati ya mambo yaliyopaisha jina la kanali Hassan ilikuwa ni kuwa kamanda kiongozi bora wa kivita ya ardhini kote Syria kuanzia mwaka 2011 hivi na kuendelea. Kutambulika huku kwa El Hassan ilikuwa kwa namna ya jina lake tu na sio picha yake.

Mnamo mwaka 2014 Al Hassan aliletwa Hadharani na watu wakaanza kumjua yeye ni nani historia umri
kwa namna ya picha na video. Ni nani waliofanya hivi na kwanini? Hao walikuwa ni serikali ya Syria waliotaka kuongeza morali ya kivita kwa wapiganaji watiifu wa Assad.

Kupitia SAMA TV, Al Hassan alionekana akiwa mstari wa mbele akiwafariji, na kuongeza morali Vita kwa wapiganaji watiifu wa Assad. Video hiyo ilichukuliwa wakati El Hassan akiwa mjini Ghouta kwenye operation iliyofaulu pia dhidi ya waasi. Kupitia Hassan ardhi nyingine ya Syria ikakombolewa kwani kila kitu kinawezekana. Al Hassan ameweza wao washindwe wana Nini?

Hapo Easten Al Ghouta Al Hassan alikichafua ile mbaya chafu hivyo basi kutokana na nidhamu na ushujaa vitani Rais Dr Assad akampandisha cheo kutoka kanali na kuwa brigedia jenerali mwaka 2015. Hassan alikubali cheo lakini akaamua kupigana mstari wa mbele Kama wapiganaji wengine.

Syria bado iko mikononi mwa waasi. Hivi Bgedia Jenerali El Hassan atafanya nini juu ya Hili?
Pencil
formula2
mbogo mzee
taamu
Spartacus boy
njumu za kosovo
Mamlukii
kawombe
Mr Bundi mtu wa peponi

ITAENDELEA....
 
Huyo Kanali na misipika yake alitumia mbinu ya UMAR IBIN AL KHATAB
"kama mnataka kuwaacha wake zenu wajane
na watoto wenu MAYATIMA endeleeni kunifuata
lah kama mnataka kuishi na wake zenu na watoto zenu mrudi hapo hapo muishie zenu"

NI nani asiyemjua UMAR akinyanyua UPANGA ukirudi chini na DAMU

yeah COMMANDER OF THE FAITHFUL
 
Huyo Kanali na misipika yake alitumia mbinu ya UMAR IBIN AL KHATAB
"kama mnataka kuwaacha wake zenu wajane
na watoto wenu MAYATIMA endeleeni kunifuata
lah kama mnataka kuishi na wake zenu na watoto zenu mrudi hapo hapo muishie zenu"

NI nani asiyemjua UMAR akinyanyua UPANGA ukirudi chini na DAMU

yeah COMMANDER OF THE FAITHFUL
Ni hatari mkuu. Kwa wasoma vitabu wengi hasa mashujaa wengi wa kileo kisayansi, kiutamaduni, na hata kijeshi matendo yao ni mwangwi wa wanafalsafa wa zamani wakiwemo mtume Muhammad, Yes kristo na wengine wengi.
 
Itaendelea

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Weka hapo chini hata episodi moja ya kuwazindua mashabiki! Mimi naanza kule juu
JamiiForums-2001443169.gif
 
SEHEMU YA NNE ( MWISHO)

Kwa kweli marafiki zangu wengi wameendelea kunishauri kumaliza stori hii ya kweli ya Jenerali Suheil Al Hassan. Jambo hili limenivutia ya kwamba hadithi hii ni nzuri na hasa kama mwandishi mchanga nina mengi ya kujifunza zaidi.
Ona sasa hadi nasahau kusalimia. Diamond Platinum katika wimbo wake mmoja hivi mtanikumbusha unaitwaje, baada ya kumpigia mkewe anaanza tu kubembeleza bila salam. Wakati akiendelea anagundua hajasalimia hivyo basi anasalimia na kuendelea kushuka mistari. Anyway wazo hili la kusalimia limekuja baada ya kugundua kwamba Wanajf ni siku nyingi sana hatujaonana humu uwanjani kuongea moja mbili. Haya basi ndugu zangu wanajf bila shaka mu wazima wa afya. Naskitika pia tumepata pigo kuwapoteza ndugu zetu kwa ajali. Mola mlezi awape hifadhi bora peponi na ndugu zao awape subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Amyna.

Haya sasa tuendelee.
Alipopandishwa cheo kuwa brigedia jenerali mwaka huo 2015 ni mwaka ambao ISIS ( Islamic State) yaani kundi la kigaidi la Dola la Kiislam lilikuwa linaendelea kutawala na kusimika mipaka yake ya kiutawala. Syria ya makundi ya kiasi ikabadilika ikaingia kwenye wimbi lingine kubwa. Wimbi la kikundi kigumu zaidi chenye nguvu zaidi kijeshi yaani ISIS ama wajiitavyo wao Daesh. Tofauti na mwanzo vikosi vya Syria vikapata adui mpya mwenye nguvu zaidi. Katika mwaka huu 2015 Syria yote pamoja na Iraq zilishaingia kwenye mtafuruku huu dhidi ya Daesh. Yale makundi ya kiasi yanayofadhiliwa na Marekani, Ufaransa, Uingereza na Israel yakaanza kupigana dhidi ya adui mpya anayezidi kumega ardhi yao ya kiutawala yaani ISIS. Wamagharibi wakaongeza misaada juu ya vikundi hivi ili wapigane na ISIS na pia kusimika kambi za kijeshi Kama ile ya Al Tanfu ya Marekani. Lakini Hapa jambo hili la vita dhidi ya ugaidi wala halikua limekuja kwa bahati mbaya. Lilikuwa lengo maalumu la kuiangusha serikali ya Assad kwa namna ya vikundi vingi Sana vinavyotaka kutawala Syria. Vikundi vya kiasi Wamarekani wakaviita vyenye itikadi ya kati vingine Kama ISIS wakaviita vyenye itikadi Kali.
Syria ikaingia vitani pia dhidi ya ISIS wakaangamia mamia ya majeshi ya Assad. Katika hali hii ngumu bado jenerali Hassani aliendelea kupigana dhidi ya vikundi hivi bila kujali hatma yake kivita na kijeshi.
Alishagundua si ISIS wala Alqaeda Wala FSA wenye lengo la kuwa na Syria huru Bali wote lengo lao kuitawala Syria kwa mgongo wa US na vibaraka wake wa Ulaya kama nilivyosema hapo juu.
Sasa basi Syria ikaanza kuwa ya machafuko zaidi hata vikundi vya kiasi vikaanza kuzidiwa nguvu zaidi na ISIS.
Mpaka kufikia mwezi wa pili mwaka ule wa 2015 Syria Hali ilikuwa mbaya zaidi, Syria huru ya kiutamaduni hasa dini na mavazi ikageuka kuwa kaburi la akina mama , watoto na wanaume wasio waislam ama wenye misimamo ya kati. Wote wakalazimishwa kuvaa na kuishi Kama waislamu wenye mrengo mkali zaidi wa kidini.
Wasiotii wakaanza kuuawa kinyama kwanini si waislam? Kwa mfano watu wa kabila la Druze wakaanza kukimbilia Israel kuomba hifadhi ya kibinadam.
Kwa hali hii wairan ambao Ni washirika wa karibu wa jenerali Hassan wakamshauri El Hassan na jopo la uongozi wa juu wa Syria Kwamba waombe usaidizi wa kijeshi kutoka Moscow. Kazi hii ya kuiomba Moscow iwasaidie Syria direct moja kwa moja ikafanywa na jenerali wa ki -Iran Major General Qassem Soleiman. Soleiman alikutana na Putin mjini Moscow kati ya mwezi wa pili au wa tatu mwaka 2015 vyanzo bingine vyasema mwishoni mwaka 2014 hivyo basi majadiliano yakafanyika na mwaka huohuo wa 2015 majeshi ya Urusi yakaingia Syria kuongeza nguvu dhidi ya makundi kadhaa wa kadha ya kiasi na kigaidi .Warusi wakaanzisha kambi mbili za kijeshi yaani jeshi la Wanamaji na jeshi la anga mjini Latakia katika eneo liitwalo Hmeim.
Walipofika huko Syria wakakutana na mwamba ajiitae Al Nimri ama tiger bwa Suheil El Hassan. Walipohadithiwa habari zake wakaamua kushirikiana nae bega kwa bega. Wakaanzisha upya mashambulizi dhidi ya waasi na magaidi na mpaka kufikia nusu ya kwanza ya mwaka 2016 ISIS yenye nguvu ilishadhoofika vilivyo. Sasa ilikuwa imebaki kwa namna ya vikundi vidogovidogo vifanyavyo mashambulizi ya kujitoa mhanga hapa na pale.
Kwa ushujaa huu wa kimapambano brigedia jenerali Al Hassan akapandishwa cheo na Rais Assad na kuwa Meja Jenerali cheo alicho nacho mpaka leo.
Kwa kawaida cheo hiki ni miongoni mwa vyeo vikubwa kabisa kijeshi hivyo basi askari wenye vyeo hivi ni watu wa command and order lakini kwa Al Hassan hali ni tofauti. Hutembea bega kwa bega na vijana kupigana huko frontline.
Kwa Meja Jenerali Al Hassan bila shaka moja ya vitu anavyovipenda sana ni mapigano ya kivita dhidi ya adui ambao yeye huwaita panya. Ni sawa na vile ambavyo pengine wengine hupenda ngono na pombe. Kilevi chake huyu ni vita. Kwa waasi na magaidi ni kama kunywa bia na kulala na akina Kajala Masanja kama zilivyo ndoto za vijana wengi wa kileo akina Harmonize na akina sie.
Je ni shujaa mtu huyu?
Hili ni swali kubwa kwa walimwengu.
Kwa wamagharibi na mashirika yake ya haki za binadam Meja Jenerali Suheil Al Hassan ni butcherman yaani muuaji, mchinjaji wa watoto na akina mama was Syria lakini kwa wafuasi wa Assad jenerali Hassan Ni Shujaa, mzalendo na mkombozi wa taifa lao dhidi ya manyang'gau wa
kimagharibi akina ISIS, Al Nusrah na FSA.
Ni Al Hassan aliyejitokeza kama mwanga gizani kujaribu kuikomboa ardhi ya Syria.
Baada ya kufanya vizuri zaidi vitani Al Hassan amepokea medali kadhaa za kishujaa kutoka kwa Assad na bila kusahau medal of Honor ya Urusi mwaka 2017 aliyokabidhiwa na jenerali wa Kirusi Vitaly Gerasmov kutoka kwa Rais Putin.
Kwa ushujaa na ujasiri wa Suheil El Hassan kupigana akiwa mstari wa mbele inasemekana Suheil Al Hassan aliuawa vitani Kati ya mwaka 2012 na 2013 hivyo basi ili kutoshusha morali ya kijeshi na kivita akatafutwa mfanano wake mwaka huohuo na akaendelea vyema na majukumu yake mpaka leo . Kwenye picha chini unaweza kuona tofauti ya Meja jenerali Hassan katika vipindi tofauti Hali iliyosababisha ije Imani ya kwamba pengine Al Hasan halisi alifariki kweli.
Katika swala zima la familia Al Hassan haijulikani ilipo familia yake mkewe watoto nk.
Mwaka 2018 mpambe wa Jenerali Suheil Al Hassan alipigwa risasi na kupoteza maisha wakiwa pamoja nae mjini Ghouta. Lakini licha ya changamoto hizi Suheil Al Hassan ameendelea na anaendelea kuwa mwiba mkali wa kivita nchini humo kwa vita endelevu ya miaka kumi na moja so dhidi ya waasi na magaidi
Tofauti na makamanda wengi wa ki -Syria ambao ni pro Iran ,Suheil Al Hassan ni pro Russia kindakindaki. Gazeti la Le Monde la Ufaransa linadai Jenerali Al Hassan ni kitisho kwa utawala wa Rais Assad baada ya vita kwisha.
Nashukuru kwa ushirikiano wenu wanajf. Ahsanteni sana. Tutakutana tena katika uzi mwingine.
Mwisho.


Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
View attachment 2414637
 
Back
Top Bottom