Jephta2003
JF-Expert Member
- Feb 27, 2008
- 6,501
- 6,200
Unajua wasafi tv na radio mke wa kusaga ana share kiasi gani?,au unazungumza tu?Wasalaam wanaJF,
Msanii Diamond ambaye ukweli ulio wazi ni msanii nambari moja hapa Tanzania
Msanii Diamond bado anapitia kwenye adhabu isiyo na kikomo ambayo amepewa na wamiliki wa EATV,efm na Clouds fm.
Adhabu hii inalenga kuhakikisha Diamond anapotea kwenye ramani ya Muziki na ikiwezekana asinyanyuke tena.
Lakini adhabu ya kutocheza nyimbo zake ilikwenda mbele zaidi na kuwafata wasanii wake wakina Harmonize,Rich Mavoko,Lavalava na Mboso na Queen Doreen nao wamefungiwa kutochezwa nyimbo zao kwenye vituo vya mabosi hao tajwa.
Lakini pamoja na kutocheza nyimbo za wasanii wote wa WCB bado wasanii hao wamezidi kung'ara kila kona na nyimbo zao zinapigwa kila kona na bila shaka na wao hao maboss wa hivyo vituo wanazisikia kila kona na hilo jambo linawatesa sana maana lengo la kumuangusha Diamond limekuwa gumu sana maana sasa Diamond ameshazaa wakina Diamond wengi kama Harmonize,Mboso na Lavalava.
Sasa Diamond amekuwa kama ni tatizo kubwa zaidi maana ameshazaa vidaimond vingine ambavyo kwakweli kuvizuia itakuwa ngumu sana na watapoteza lengo na ni wazi inakuwa ngumu sana kujua ni wapi sahihi kwa kupiga je ni kwa Diamond au kwa vidaimond.
Rich Mavoko wamemsamehe baada ya kujitoa WCB.
Hawa watanzania wenzetu wana lengo jema sana la kuhakikisha Diamond na vidiamond vyake viaanguka na vinakufa kabisa lakini kila kukicha vinazidi kunawiri moboss wameshindwa kabisa kumuangusha Diamond na wanaendelea kujaribu lakini wanashindwa na ni vyema wakasaidiwa kufanikisha lengo lao hili jema hata la mawazo.
Watumie njia gani mbadala?
Wafanye nini?
Wana kwama wapi?