Nimekuwa nikijaribu kufikiria maisha ya nyuma niliyoyaishi na ya sasa na naona kama kwa sasa nipo kwenye ulimwengu tofauti kabisa. Nimezaliwa na kukulia katika mazingira ya kawaida, ambapo nilikuwa na interactions sana na majirani. Nilikuwa nikicheza, kula na hata siku nyingine kulala kwa majirani.
Miaka hii nashangaa hii hali siioni kabisa. Nimekaa mtaa huu kwa zaidi ya miaka 5, Jirani zangu sifahamiani nao zaidi ya kuona magar yakiingia tu ndani na kutoka. Watoto nao wamekuwa busy na shule na wakitoka ni computer na TV tu, na hawana interactions na wenzao kama ilivyokuwa miaka yetu.
nyie kwenu vp jaman, ni mtaa wetu tu au na hii hali kwenu ipo?
Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
Nashangaa hata kwenye matukia kama misiba, sherehe hata hatuambiani!! uanasikia tu kwa jirani wanasherekea au wanalia, but you are not given any information...halafu tena ukizingatia miaka hii kujipendekeza nayo shidaa!!duh,mie huwa nakutana na majiran kwenye matukio. naifahamu familia iliyo kulia kwangu na kushoto. nyumba ya 2 na 3 hata siwahafamu kwa majina zaidi ya sura. . . zamani tulipokuwa watoto tulikuwa tunacheza kwa kushindana mtaa huu na mtaa wa pîli. afu pia karibu mji mzima tulikuwa tunafahamiana, lakin siku hizi weng tumehamia mji ambayo hatukuzaliwa kwa hiyo hatufahamiani na hata wanetu hawafahamian wapo busy na shule.
Dah! Na kukodi watu wa kulia misibani! Unapatwa na janga, huna jirani wa kukusaidia na kukufariji. Inabidi uingie tu garama za kuwakodi watu!!Ujamaa ulikuwa na raha zake na mojawapo ilikuwa ni hii ya undugu,tofauti na sasa tumefikia mpaka kupeana kadi kwenye misiba...
maisha yamebadilika ni mchakamchaka na kukimbizana na shilingi..... Hapa mtaani majirani ninao wafahamu ni wachache wanaonizunguka na wengine ninaosali nao jumuia maana Kwa sisi wakatoliki angalau jumuia zimesaidia kujuana kutokana na kusali kila jumamosi.......
Ila kwa majirani waliobakia ilinichukua muda kuwajua majina, na kuonana ni mara chache sana..... Hivyo usimlaumu jirani yako asipokualika sherehe, ila msiba hauna mwaliko.....
Hahahahaha....umenifurahisha sana watu8, haya ndio maisha nayotamani kuyaishi!!!Mbona sisi uswazi kwetu mambo ya ujirani yapo sana tu...
Mambo ya kuombana chumvi, moto wa kukolezea mkaa, ungo wa kupepeta mchele, sometimes majirani huwa wanakuja kuchuma matembele home...huku kwetu michezo kama ukuti, kombolela n.k bado ipo kwa sana
Siku hizi hata mtoto hatumwi dukani, achilia mbali mashine!! Wazazi + hg ndio mnafanya shopping ya kila kitu. Nakubaliana na wewe, maisha yale yalikuwa mazuri kuliko haya!!Maisha uliyoishi mtoamada it's same with me .
Tukubali tu global ndiyo imekuja kutofautisha life ile na hii .
Mf. Sisi tulikua tunatumwa kupeleka mahindi kusaga unga mashineni !
Leo hii watoto wetu hawajui kama unga husagwa wapi .
Zamani Mwl alikua ni mtu mwenye kuheshimika kuliko polisi ! Now days kinyume chake.
Bt ukiniambia niseme maisha yale na haya , yepi mazuri ?
Nitasema YALE na si HAYA .
Ujamaa ulikuwa na raha zake na mojawapo ilikuwa ni hii ya undugu,tofauti na sasa tumefikia mpaka kupeana kadi kwenye misiba...
Ndugu wenyewe nao siku hizi wanashikika? Bora hata uanze kujikomba kwa majirani...lol!Siku ambayo nilipishana na jeneza linaingizwa nyumbani kwa jirani yangu ndio nikagundua kweli naishi mjini! Nikajiuliza nisimame, niingie na kujikalisha ama vipi? Mwenye nyumba sijawahi kukutana nae hata sura yake simjui na gari yake siijui. Si ndio mwanzo wa kuitwa mchawi, kutokea msibani kama radi?
Hatua niliyochukua ni kuhakikisha niko karibu na ndugu zangu. Najua hapa nikipata tatizo ni simu tu! Sio utaratibu mzuri kiukweli!