Majirani...

ni hatari na aibu huwa naona pia! simjui hata wa pembeni yangu kulia na kushoto maana ni nyumba za kupanga, wanakuja leo baada ya miezi 6 wameondoka wamekuja wengine! jirani mpangaji alijifungua twins last month, nimetoka job twins wangu nao wananitaarifu kuwa wameona barbies, lakini barbies wao wanalia na kunyonya, nikawauliza wapi, wakanijibu dukani! hiyo familia ina kaduka kwa mbele japo wamepanga. nikatafuta vizawadi same evening tukaenda, cha ajabu waliniambia wako hapo wana mwaka wa 3 wamepanga! na wao hawanijui, basi ukawa ni mwanzo wa kujuliana. ila kwa kweli tunakokwenda, sio kabisaaaaaaaaa! watoto wetu watakuja oana ndugu wallah!
Kwenye nyumba za kupanga tena ndio balaa, mnaweza mkawa mmepanga nyumba moja na hamna mtu mwenye time na mwenzake zaidi ya salam tu!!!!! Wengine hata kufahamiana inakuwa issue.
 
Maisha yamekuwa ya dot.com tu kwa wote mie hata jirani simjui anafananaje........

Zamani mnakwenda kucheza chakula kinapikwa kwa jirani mnakula, mnaoga, mnalala huko siku hizi thubutu utaanzia wapi ukienda kwa jirani watoto wako busy na computer hata kukusalimu mgeni ni issue lakini ndo hivyo maendeleo
Dena Amsi, unaweza kukuta mimi na wewe ni majirani kabisa...but tunafahamiana tu hapa kwenye keyboard!!:ranger::ranger::ranger::ranger::ranger::ranger::ranger:
 
Last edited by a moderator:
Nimekuwa nikijaribu kufikiria maisha ya nyuma niliyoyaishi na ya sasa na naona kama kwa sasa nipo kwenye ulimwengu tofauti kabisa. Nimezaliwa na kukulia katika mazingira ya kawaida, ambapo nilikuwa na interactions sana na majirani. Nilikuwa nikicheza, kula na hata siku nyingine kulala kwa majirani.

Miaka hii nashangaa hii hali siioni kabisa. Nimekaa mtaa huu kwa zaidi ya miaka 5, Jirani zangu sifahamiani nao zaidi ya kuona magar yakiingia tu ndani na kutoka. Watoto nao wamekuwa busy na shule na wakitoka ni computer na TV tu, na hawana interactions na wenzao kama ilivyokuwa miaka yetu.

nyie kwenu vp jaman, ni mtaa wetu tu au na hii hali kwenu ipo?

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums

unachosema ni kweli kabisa...hata mimi nilivyokua mtoto miaka hiyo ilikua majirani wanakuja kwetu na sisi tunaenda kwao, ilikua haipiti siku mbili umeonana au kusalimiana na jirani zenu na wakati huo hawakua tu majirani bali ni marafiki kabisa..siku hizi ukiniuliza nyumba ya pili anakaa nani hata sijui...watoto zetu sasa hivi ni video games, wii na internet..enzi zetu kulikua hakuna cha internet wala play station...na hii inafanya watoto wa generation ya sasa watakua selfish watakua hawajazoea kuongea na watu ukilinganisha na miaka ya nyuma
 
kwa kweli ilikuwa raha sana....

lakini siku hizi uharibifu nao umeongezeka ndio mana watu wanawakaza watoto kwenda nyumba ya pili kula na kucheza!!!!

Nakumbuka hata mkihamia eneo jipya basi haichukui muda tayari mtazoeana na life itaendelea kwa taratibu zilezile!!!!

SWALI nini kifanyike sasa??!!!
 
Back
Top Bottom