Majini: Viumbe vyenye roho hatari na wivu uliopitiliza

Majini: Viumbe vyenye roho hatari na wivu uliopitiliza

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,869
Reaction score
828,403
Msingi wa mada hii ni wanawake ambao wamependwa na 'kuolewa' na majini. Hawa wana bahati mbaya sana kwa kuwa hawaoleki na binadamu

Kwenye ukoo mzima wa majini kuna mazuri na mabaya na kuna haya yanayopenda kufanya mapenzi na binadamu wa kike. Hawa ni tatizo sana

Unapozungumzia wivu wa kiumberoho jini, huwezi kuacha kuzungumzia wivu wa mnyama nyegere, huyu anawakilisha kipimo cha wivu kwenye ulimwengu unaoonekana. Nyegere ana uwezo wa kumfuata mbaya wake hata kilometer 100 kwenda kumdhuru via vya uzazi akikuhisi vibaya na mpenzi wake na pengine pia ana uhusiano na neno nyege.

Ukiachana na jini na nyegere viumbe wenye wivu uliopitiliza kuna kicheche, huyu hana wivu ila kiwango chake cha tamaa ya ngono kiko juu kuliko kiumbe mwingine yeyote. Kicheche ana uwezo wa kufanya ngono mara 18 kwa siku na ndio asili ya binadamu wapenda ngono kuitwa vicheche

Turejee kwenye mada

Kiumbe roho jini hapendi kushare mapenzi na binadamu. Ana wivu mbaya sana hivyo mwanamke anayeshiriki ngono na jini hawezi kupata mpenzi binadamu au kuzaa mtoto

Akipata mpenzi binadamu wataishia kugombana na ikitokea kazaa mtoto atakufa kwa bahati mbaya sana kwakuwa wana hisia kama binadamu wengine wote hili jambo huwaumiza na kuwafadhaisha sana lakini HALINA TIBA, tiba pekee ni jini kuamua kuondoka mwenyewe yaani kutaliki

Na hata jini akiondoka mwanamke huchukua muda mrefu kupata mpenzi wa kutulia naye kutokana na kukosa aina ya mapenzi aliyokuwa anayapata kutoka kwa jini.

Hivyo ndugu yangu kama una mpenzi wa jinsi hii hakuna tiba itakayomfaa zaidi ya kutuliza tu kama asprini
 
ndio jini mahaba? Vipi kwa mwanaume naye akipatwa na huyo jini atapata madhara gani?
 
Tiba ni Yesu ... ukiwa kipofu na kutumia sababu yako kuhalalisha hali yako, nikweli kabisa Roho wachafu watakusumbua tena hasa ukiwa umefanya nao maagano

Ni yesu pekee. Ambaye atakupa ndoa hata ktk miaka 40 yako, atakufanya uzae hata km hospitalin umeambiwa huwezi kuzaa.
 
sikuwahi kujua asili ya kuitwa kicheche mtu mpenda ngono. lakini mkuu hili la majini kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanadamu sidhani kama kuna ukweli wowote nadhani ni hadithi tuu maana jini si kitu kionachoonekana kwa macho wala kushikika sasa kitawezaje kuwa na mahusiani na mtu au mwanadamu
 
sikuwahi kujua asili ya kuitwa kicheche mtu mpenda ngono. lakini mkuu hili la majini kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanadamu sidhani kama kuna ukweli wowote nadhani ni hadithi tuu maana jini si kitu kionachoonekana kwa macho wala kushikika sasa kitawezaje kuwa na mahusiani na mtu au mwanadamu
Hata mahusiano yake ni kwa njia ya ndoto sio live...haya mambo yapo sio uzushi nimeyashuhudia mimi mwenyewe maranyingi sana
 
Back
Top Bottom