Majini & Mapepo 👻🤔

Unamuuliza mwalimu kwanini tukariri Qur’an kwa kiarabu then baadae tuanze kusoma tafsiri kwa kiswahili ni mantiki ipi hapo?

Dini imejaa vitisho kuliko kawaida waumini roho juu alfajiri amkaaaaaaaa swalaaaaaaa hicho kitanda ni kaburi hiyo shuka ni sanda lol 😅😅

Mungu anatuumba mwenyewe anaanza kututisha
Unapohoji udhibitisho wa uwepo wa Mungu ni rahisi kukutana na maneno yafuatayo:
1. Kama una majivuno, ama unajifanya mjuaji.
2. Una kiburi cha uzima. Na vitisho vya aina hiyo.
Unaambiwa Mungu hachunguziki
 
Mkuu ni nani alikukataza kujadili biblia???

Kwenye biblia Kuna kifungu kinasema

Isaya 1:18 – “Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA…”
Isaya 41:21 – “…leteni hoja zenu zenye nguvu, asema Mfalme wa Yakobo.”

Sasa kama Mungu ameruhusu wewe umjudge unaanzaje kusema umekatazwa???

Tatizo mnawasikiliza wachungaji wanaotafuta ulaji kwa kupitia biblia. Achana na wachungaji waongo waongo wewe soma biblia alafu uitafakari.
 
Mimi nilistuka muda mrefu, toka 1992 nikiwa kijana mdogo niligoma kwenda church. Sasa hivi sitaki shobo za dini kabisa. Watoto wangu nimewaambia wanaweza kuamini chochote kama wanaona ni lazima, lakini siwapangii.
 
mkuu hivyo vitabu tunafundishwa na hao viongozi, hivyo tunawatumia wao kama case study. Lakini hata hivyo Bado ukisoma hivyo vitabu ni full contradiction bila hata hao unaosema ni wachungaji maslahi.
 
Mimi nilistuka muda mrefu, toka 1992 nikiwa kijana mdogo niligoma kwenda church. Sasa hivi sitaki shobo za dini kabisa. Watoto wangu nimewaambia wanaweza kuamini chochote kama wanaona ni lazima, lakini siwapangii.
Ulishtuka mapema sana
Na kama umefatilia watu wa dini ndio watu wanaongoza kwa maovu

imani zao hazijawabadilsha
 
mkuu hivyo vitabu tunafundishwa na hao viongozi, hivyo tunawatumia wao kama case study. Lakini hata hivyo Bado ukisoma hivyo vitabu ni full contradiction bila hata hao unaosema ni wachungaji maslahi.
Mkuu, naweza kusema kwamba wote ambao mnamsema Mungu kwa mabaya ni kwamba hamumjui Mungu na wala hamuyajui maisha.

Vijana tokeni nje ya box mlilojiwekea, nendeni migodini huko ndio mtajua kuna Mungu alafu Kuna shetani pia.

Hauwezi kumuona Mungu ukiwa unakula na kushiba, ukitaka kumuona Mungu kwa uhalisia ni pale ambapo utaanza kutafuta vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wako.

Kijana huko migodini watu wanafuga Chatu chini ya maduara, Huyo Chatu watu wanamuona na wanafanya nae kazi. Ninyi mmekaa huko mjini mnaziona dhahabu tuu na hamjui zilipotoka.

Tokeni nje ya mabox hayo. Mmekaa mjini mnaliwa fedha zenu na akina mwamposa kazi yenu kutafuta miujiza, nendeni mapolini huko mtaiona miujiza kwa macho yenu.
 
Ulishtuka mapema sana
Na kama umefatilia watu wa dini ndio watu wanaongoza kwa maovu

imani zao hazijawabadilsha
Hapa ndio upo sahihi. Ukiongelea watu wa dini lakini usimuunganishe Mungu na dini.

Uyahudi ni dini ambayo inafuata mafundisho ya Musa. Hawa wayahudi ndio walimsulubisha YESU kwasababu waliona anafanya mambo tofauti na dini Yao, hivyo hivyo hivi leo Kuna dini inaita watu wa dini nyingine ni makafiri na inaenda mbali kwa kuwachinja hao makafiri. Pia Kuna dini nyingine inawaita watu wa dini nyingine ni wafuga majini, watoto wa bibi mdogo na maneno mengine mengi ya kejeli.

Nilichokiona kama shida kwenu ninyi watu mnaomkataa Mungu ni kwamba ninyi mlifuata mafundisho ya dini zenu na sio mafundisho ya vitabu vitakatifu, yaani mlikua mnaangalia/kuwaamini wachungaji/masheikh pasipo kumuangalia/kumuamini Mungu.
 
Huyo nyoka huko mgodini ndio Mungu?!
 
Huyo nyoka huko mgodini ndio Mungu?!
Hapana, anatumika kama mungu kwa wanaomwamini shetani.

Huyo nyoka ni shetani kabisa kwasababu anaingia kwenye shimo la MITA 70 mpaka 100 lakini anaishi vizuri tuu. Huko chini wanapofanya kazi yeye ndio hutoa maelekezo kwamba Leo lipueni jiwe sehemu hii na sehemu hii.

Na pia mkitega baruti na kulipua huyo nyoka mnamuacha huko huko chini lakini mtakuta mawe yamevunjika vunjika lakini nyoka ni mzima na Hana jeraha lolote.

Pia mmiliki wa duara ndio hua anajua huyo nyoka anamlisha Nini? Lakini siku mkiona mwenzenu amefia duarani basi ujue nyoka ameshapata chakula.
 
Mimi nilistuka muda mrefu, toka 1992 nikiwa kijana mdogo niligoma kwenda church. Sasa hivi sitaki shobo za dini kabisa. Watoto wangu nimewaambia wanaweza kuamini chochote kama wanaona ni lazima, lakini siwapangii.
Mkuu wewe ni mtu mzima kunizidi, heshima Yako kwanza.

Pia sorry kuna comment nimekuita kijana lakini haupo kwenye level za vijana.

Lakini hapo kwenye kutomuamini Mungu hapana nakukatalia mkuu. Kuna mambo mengi sana naweza kukuelekeza na ukamuamini Mungu.

Binafsi nimefanya UJINGA mwingi ambao kama asingekua Mungu bhasi nisingekua na maisha au ningepata kilema Cha milele lakini Mungu alijidhihirisha kwangu live.
 
Nitarudi .mkuu
 
Hapa ndio upo sahihi. Ukiongelea watu wa dini lakini usimuunganishe Mungu na dini.
Wewe ulijuaje habari za Mungu bila dini?
Ukijifunza wapi habari za Mungu?
Imagine watu wanaojinasibu na Mungu wana tabia kama hizo
Nilichokiona kama shida kwenu ninyi watu mnaomkataa Mungu ni kwamba ninyi mlifuata mafundisho ya dini zenu na sio mafundisho ya vitabu vitakatifu, yaani mlikua mnaangalia/kuwaamini wachungaji/masheikh pasipo kumuangalia/kumuamini Mungu.
Sasa mkuu vitabu vitakatifu si vimetokana na dini?
 
Wewe ulijuaje habari za Mungu bila dini?
Sio lazima kujua habari za Mungu kupitia dini.

I can tell you about myself. Mimi nimezaliwa kwenye familia ya dini lakini nilikua siamini hizo mambo kabisa.

Imani yangu ilikua ni kupata utajiri kwa njia yoyote ile. Nimekaa miaka saba sijawahi kuingia kanisani.

Nilikua ni mlevi, mvuta bangi na wale vijana wa makundi namimi nilikua ndio kundi lenyewe, thanks God alinipa akili ya kujitambua tuu.

Nikiwa chuo mwaka wa kwanza mimi nimeuza bangi sana, na hiyo ndio ilikua plan ya kuutafuta utajiri. Club zote maarufu Dar kwa miaka ya 2010-2014 ndio vilikua viwanja vyangu. Nimeshinda sana club sansiro, bilcanas na pale sinza africasana pamoja na ambiance.

Mungu aliingilia kati nikajikuta nimeokoka pasipo mtu yoyote kuniambia okoka. Hapa ndipo nilimjua Mungu.

Baada ya kuokoka nilipata amani ambayo sijawahi kuiona maishani mwangu, Yaani amani ambayo siwezi kumsimulia mtu akaelewa. Hicho ndicho kitu pekee Cha tofauti nilikigundua baada ya kuokoka.

Ukijifunza wapi habari za Mungu?

Niliokoka kanisani na hiyo ndio ilikua njia ya kujifunza habari za Mungu.

Baada ya kuokoka nilikua nakwenda kanisani vizuri tuu na pia nilikua najifunza mahubiri ya mchungaji wangu. Lakini sio Kila alichokuwa anahubiri mchungaji nilikipokea kama kilivyo. Na hapa ndipo ilianza safari nyingine mpya ya Mimi kumjua Mungu zaidi.
Nilianza kusoma biblia Mimi binafsi na pia nilianza kuyachunguza maandiko.

Wachungaji wengi wanafundisha watu habari za mbinguni tuu kitu ambacho sio kweli. Mungu angekua anataka twende mbinguni basi angetuua wote ili twende mbinguni tukapumzike na kukuthibitishia hili wewe nenda kasome biblia Kuna mahali katika kitabu Cha Yohana Mtakatifu YESU anatoa ripoti kwa baba yake ambaye ni Mungu anamwambia "SISEMI KWAMBA UWATOE DUNIANI LAKINI WAPE USAIDIZI" hivyo tunapookoka ni kwamba tunafanyika watoto wa Mungu na kwa hilo tunapewa usaidizi wa kutenda jambo lolote hapa duniani, Sawa sawa na neno katika Wakorinto linasema "NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU".

Kuhitimisha naweza kusema kwamba dini ni msingi wa kumjua Mungu lakini sio lazima ujifunze kupitia dini, wewe soma biblia na Roho Mtakatifu akuongoze bhasi.

Nasema soma biblia kwasababu hapa katika maisha ya kawaida ni Kuna watu wanajua vitu vingi na shule hawajaenda Wala Nini.

Nimalizie kwa kukuuliza swali kwani alieandika mitaala ya shuleni na vitabu yeye alifundishwa na nani? Ukipata jibu hapa bhasi jua kwamba hata Mungu unaweza kumjua pasipo kupitia hiyo njia ya dini.
Imagine watu wanaojinasibu na Mungu wana tabia kama hizo
Mkuu ni lazima uelewe kwamba dini ni Mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu. Lakini pia katika dini yamejaa maslahi ya mwanadamu kwa kutumia jina la Mungu. Nitakupa na mifano yake

Mosi: Wakoloni walitawala Africa pamoja na America kwa kutumia njia ya dini. Kasome historia ya Marekani na ukoloni.

Pili: Dini zinatumika kwa maslahi ya watu ili kuuza silaha, Zingatia wale watu walioaminishwa kwamba wakifa wanapigania dini wataenda peponi.

Tatu: Dini ni chanzo Cha mapato hasa hasa nchi za Africa, angalia wachungaji wanavyomiliki Mali za ajabu huku waumini wao wakikosa nauli na wengine wanalala njaa. Waumini wanajenga shule, mahospitali lakini wanashindwa kusomesha watoto wao wala kutibiwa katika hospital walizozijenga wao wenyewe.

Nne: Dini zinatumika kama chanzo Cha taarifa za kijasusi. Zamani wakati wa utawala wa Roma ilikua ngumu sana kupata taarifa za mauaji na hasa hasa mauaji ya Siri hivyo wakaja na mbinu inaitwa kitubio. Kwamba waumini wa Roman Catholic wanatakiwa kwenda mbele ya padri na kukiri dhambi zake zote na huu utaratibu Hadi Leo unaendelea katika kanisa la Roman. Hii ilikua ni mbinu ya kupata taarifa za uhalifu pasipo watu kujua. Zingatia zamani hizo dini ilikua ni Moja tuu ambayo ndio Roman Catholic church

Tano: Serikali za Dunia nzima zinafaidika sana na uwepo wa dini kwasababu dini zinawapa watu matumaini hivyo kupunguza mzigo wa mashinikizo kwa serikali na pia wanasiasa wanapata unafuu. Ndio maana hapa bongo utaona wanasiasa wetu hawaishi kwenda makanisani na Kuna muda unasikia serikali imewapa kanisa Fulani fedha au Kuna wachungaji Fulani Fulani wamepata milungula. Zingatia fedha za Escrow mpaka wachungaji na mapadri walipata gawio😂😂😂🤗

Yapo mengi sana ya kuandika lakini naomba niishie hapa, huku nilipo mvua inanyesha sana Leo na shughuli zangu zinasuasua.

Sasa mkuu vitabu vitakatifu si vimetokana na dini?
Hapana dini ndio zimetumia vitabu vitakatifu kujianzisha. Binafsi sijawahi kuisoma kuruani ila nikisikiaga baadhi ya mahubiri ya masheikh huwa naona kuruani na biblia tofauti yake ni ndogo sana.

Kwenye biblia anaitwa YESU kwenye kuruani wanamwita Issa bin Mariam.
Manabii wengine wote pia waliopo kwenye biblia wanatambulika katika kuruani pia.

Ukitaka kujua historia ya dini inabidi ukasome historia ya Roma Empire. Roma empire imetawala Dunia muda mrefu sana na Roman Empire ndio chanzo Cha dini na dini ya kwanza kabisa ni Roman Catholic Church.

Achana na Uyahudi, uyahudi ilikua ni tamaduni za watu wa Israel na ndio maana hata Pilato alikataa kumuhukumu Bwana YESU.

Kwa kifupi dini ya kwanza ni Roman Catholic church, ikafuatia dini ya Lutheran, Martin Luther alianzisha Lutheran church baada ya kuona Roman inatumika kukandamiza watu. Yaan Roman ilitumia biblia kuwatumikisha watu na ndio maana waumini wa Roman Catholic hadi Leo hawana utamaduni wa kusoma biblia. Yaani wao biblia anaisoma padri tuu bhasi.

Baada ya Martin Luther dini iliofuatia ni Anglican na hii dini alikuja baada ya Mfalme wa Uingereza kutaka kuoa mke mwingine na Roman Catholic church wakamkatalia hivyo Mfalme wa Uingereza aliamua kuanzisha kanisa lake na kuwaamuru waingereza wote kusali katika kanisa lake. Anglican church ndio kanisa la kwanza duniani kuruhusu ndoa za jinsia moja binafsi hata sikushangazwa kutokana na historia yake.

Hivyo dini hazikuleta vitabu vitakatifu Bali dini zinatumia vitabu vitakatifu.
 
Sijasoma Uzi wako ni mrefu sana ila ninachokumbuka kuna ndugu yetu mmoja wa kike alikuwaga na majini miaka ya 90 yalikuwa yanapanda kabisa ila siku hizi sioni hizo mambo nahisi wale majini waliamua kurudi kwao baada ya kuona hali ngumu hapa Bongo😐
 
Madhara mengi yametutokea sababu ya kuboresha na kuacha nature”
Nafafanua kama utanielewa.

Mapenzi ya Mungu hayakua binadanu aishi kwa kutafuta pesa
Mapenzi ya Mungu hayakua mwanadamu aishi kwenye gholofa
Mapenzi ya Mungu hayakutaka mwanadamu anywe pombe
Mapenzi ya mungu hayakutaka binadam apike chakula
Mapenzi ya Mungu hayakua binadamu awe msomi
N.k

Nina amini.
Mapenzi ya mungu yalikua
Binadanu wazaliane kama wanyama wengine tena kwa kuzingatia racing husika. Mfano Mzungu kwa mzungu ndo maana kuna namna DNA za sasa za mwafrika huenda zisiwe sawa na wale wa karne ya zamani katika ubora.

Binadam ilipaswa kutembea sio kutumia magari na vingine, ndo maana utaona saiv watu wengi wanafanya jogging sababu ni nature tumeiacha.

Binadamu hatukupaswa kutumia dawa za kizungu, ilibidi tutegemee mazingira na vyakula vilivyotuzunguka maana Mungu alie ruhusu ukae equator region ndo alikupa melanin ya kukomaza ngozi yako ila tunatumia sabuni zenye kemikali kuogea na mwisho tunauziwa vipodoz ili kufanya kazi ya kile tulichokiondoa wenyewe kwa ujuaji wetu

Inshort huenda tungekua wenye nguvu zaidi au wenye afya zaidi kama tusingekua na haya tunayiyaita maendeleo tulionayo.

Emu ondoa akili ya kawaida na jaribu kufikiria out of box.
..May be Mungu karuhusu kifo kwa kitu kisichofaa au kilichovuka mipaka yake ndo maana tunakufa kilasiku na tunazaliana tena sababu Dunia inataka kitu pure na fresh kilichokwenye mipaka yake na ili kisurvive inabidi kikutane na yale mazingira ya asiri ambayo yalishakufa sababu ya hiki tunachoita maendeleo ndo maana kila siku life expectancy inazidi kupungua!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…