Majina ya waliopendekezwa kugombea EAC kutoka CCM

Majina ya waliopendekezwa kugombea EAC kutoka CCM

Mndolwa ninayemfahamu ni very good accountant(ACCA,MBA,PHD) lakini haya mambo ya EA na siasa zake naah bro!! Yule msaliti wa upinzani nafuu kidogo!

Huyu jamaa alichakachua mahesabu ya TTCL halafu matokeo yake tukalipwa kiduchu wakati wa ubinafsafsishaji na balance jamaa wakagoma kulipa kwa sababu eti mahesabu yalikaa vibaya!!
 
Naona mpango wa uislam ndani ya ccm unaendelea kuiva sana! Wanaojua kusimamia kura ni waislam tu?
 
Nawapa pole hawa wanaume wa magamba 17 kwani kwa Kinana na Nape kuwa wasimamizi wa uchaguzi wenu you must be rest asured kuwa kura zenu zitachakachuliwa in favour of Fisadi mwenzie wa RED CROSS pia Nape WILL DO IT IN FAVOUR OF BAHARIA; komaeni nao kuwa mchague wasimamizi wenu wakati kura zinahesabiwa ama sivyo watafix matokeo!!
 
Nimesoma matokeo ya mchujo wa wanaogombea Ubunge wa Africa Mashariki, hasa baada ya kukuta kijana wa nguoni kabisa wa EL, James Millya akiambulia kipigo cha ajabu katika mchujo huo na hasimu wake mkubwa ambaye pia ni hasimu mkubwa wa EL na RA...(itakumbukwa mara kadhaa kwenye vikao mbalimbali amekuwa akiwa attack kwa majina yao kuwa ni mafisadi.)... akirudishwa.

Wakati huohuo kina Benno na Bashe wakiona mbali na kujitoa mapema!

HII NI DALILI YA ANGUKO BAYA LA EDWARD NGOYAYE LOWASSA.
 
Kwa maoni yangu watu kama Mndolwa, Murunya na Rweikiza wanapaswa kujikita ktk shughuli nyingine muhimu kuliko kukimbilia ubunge wa EAC. Wanapoteza muda hawa kwenda huko. Hawa wanapaswa kuwaza kusimamia shughuli kubwa za kiuchumi na biashara badala ya kwenda kusinzia huko Arusha! Kimbisa bado anahangaika kutafuta vyeo tu?
 
Nimesoma matokeo ya mchujo wa wanaogombea Ubunge wa Africa Mashariki, hasa baada ya kukuta kijana wa nguoni kabisa wa EL, James Millya akiambulia kipigo cha ajabu katika mchujo huo na hasimu wake mkubwa ambaye pia ni hasimu mkubwa wa EL na RA...(itakumbukwa mara kadhaa kwenye vikao mbalimbali amekuwa akiwa attack kwa majina yao kuwa ni mafisadi.)... akirudishwa.

Wakati huohuo kina Benno na Bashe wakiona mbali na kujitoa mapema!

HII NI DALILI YA ANGUKO BAYA LA EDWARD NGOYAYE LOWASSA.
Hakuna lolote la maana hapo. Wabunge wa sasa wamesaidia nini Tanzania? Chini ya CCM mpaka sasa sisi kama taifa hatujui tunatafuta na tunataka nini ktk EAC! Tumebaki kulalamika tu!
 
- Jamani heshima yenu sana JF wote niliowakosea nawaomba radhi sana, tulianza na keyboard sasa ni wakati wa vitendo, kaazi!

AHSANTENI!

William.
safari bado ndefu tulioko nje ya uwanja tunakutakia heri na fanaka, hujatukusea ila lanje machekulu mabii mwaha
 
Hiviupinzani nao wanahusika? Tunaomba pia majina Yao au ndio hivyo wote ni wa ccm tu?
 
i love this country, kila mtu ni JOBLESS, hata wenye kazi wanataka kuwa nazo saba
 
Kwa haraka haraka vijana wa mzee mwinyi na bilali wanaendelea kupeta.


Yaani Ndani ya CCM kama wewe siyo mtoto wa KIGOGO, huwezi kupata uongozi, labda Ubalozi wa Nyumba Kumi tu kwa kuwa hawaba POSHO.

HAya NDIO MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA!!!!!!!!!!!!!!!




MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Wanachama kadhaa wa CCM wamesikitishwa na majina ya wanachama waliopitishwa kuwania ubunge wa Afrika Mashariki.Wamesema kwamba kitendo cha chama chao kupitisha idadi kubwa ya majina ya watoto wa vigogo ni ishara tosha kwamba chama chao kimegeuka kuwa cha kisultani.Pia wamesema kitendo hiki kitazidi kuwaweka mbali na wananchi.Baadhi ya watoto wa vigogo waliopitishwa ni mtoto wa Nyerere,mtoto wa Mwinyi,mtoto wa Billali na mtoto wa Malecela.SOURCE:TANZANIA DAIMA.
 
Ndio maana wako tayari kuua kwa risasi ili mradi tu wabaki madarakani,..wanagawana na kurithishana madaraka bila aibu..hii jumuiya nayo imekaa kiposhoposho tu!kwanza hilo bunge lina faida gani hasa?
 
Huyu mkweree anafanya hivyo makusudi ili wakati ukifika aweze kumuingiza zuzu wake nae kwenye nafasi za uongozi bila watu kumyooshea kidole; hopefully he will live to that day!
 
Wanachama kadhaa wa CCM wamesikitishwa na majina ya wanachama waliopitishwa kuwania ubunge wa Afrika Mashariki.Wamesema kwamba kitendo cha chama chao kupitisha idadi kubwa ya majina ya watoto wa vigogo ni ishara tosha kwamba chama chao kimegeuka kuwa cha kisultani.

Hakunaga mwana ccm awezaye kusema maneno haya.
 
Back
Top Bottom