Majina ya waliopendekezwa kugombea EAC kutoka CCM

Kwa mtu uliyejijengea jina hapa JF that is too low.
Hii ni ya watoto wa form two.
Kwa mtu mzima haionyeshi ustaarabu.

Mkuu watu waliokulia katika mazingira tatanishi utawajua tu kwa lugha zao.
Fikra tatanishi hazipotei kulingana na makuzi, ndio maana mie nikampa pole tu huyu mkuu Matola.
Ustaarabu wa kugombea uwakilishi hapo ni nongwa.
 
"Babu alikuwa mwalimu; baba na mama walikuwa walimu, mtoto ni mwalimu," hakuna kosa.
"Babu alikuwa daktari; baba na mama walikuwa madaktari, mtoto ni daktari," hakuna kosa.
"Babu alikuwa mwanasiasa, mama na baba walikuwa wanasiasa...," mtoto kuwa mwanasiasa kuna kosa gani?

Wewe unadhani huu mgawanyo unakuja kwa bahati mbaya? Unadhani aliyetoka kwenye background ya familia ya ualimu anafurahia kuwa mwalimu ama analazimika (kwa sababu hana option) kuwa mwalimu na yeye pia kama wazazi wake waliomtangulia? Hii ni social class reproduction: na ipo hapo si kwa bahati mbaya kama unavyotaka kutuaminisha.
 
Huyu Musa Mnyeti anakomaa nao kila nafasi inayojitokeza, kama Shyrose vile hawakubali kupitwa.

Alivyotoswa TUCTA alilalamika sana sijui alikuwa ametumwa na magamba kuingia tucta ili aivuruge!? Hata huko kwenye ubunge wa EAC hana uwezo wa kufaa kuwa muwakilishi wetu lakini kwa akili za wabunge wa ccm lolote laweza kutokea.

Wabunge wa ccm rushwa nje nje kwahiyo mwenye pesa ndio atakayeshinda!! CCM wabunge choka mbaya na mgombea yeyote wakimuona amevaa vizuri akili yao wanafikiri ana pesa basi wanampangia bei!! Siasa za ccm ndio zilivyo kwahiyo hapo Kimbisa atamwaga sana kama alivyomwaga kwenye ubunge wa Dodoma mjini na akashindwa!!
 
Usultani zanzibar unaendelea!watoto wa bilal,mwinyi etc!wanzanzibar wanawanyima nafasi waislam wa tanzania bara

Sio Zanzibar pekee hata bara ni majina yaleyale ya watoto wa vigogo na vigogo wa zamani, hii sio nchi ya kifalme kulisishana nyazifa
 
Ulaya 'kurithi' uongozi is an exception moreover electrol process is free and fair. Hapa kurithi uongozi is the norm tena kwa kutumia utaratibu ulosheheni mizengwe. Usultani mambo leo utatifikisha pabaya.
 
Asiyejulikana ni kuchinjiwa baharini tu, aliyenacho ataongezewa na ambaye hana au ana kidogo hata chenyewe atanyang'anywa labda hawa wanasiasa wanatumia vitabu vitakatifu vibaya au kutimiza maandiko ili Dunia ijengewe chuki na watu wengi dhidi ya watafuna nchi bila huruma.
 
Amazing, naona jina la Fancy, huyu dada nyumba ndogo ya Njaa Kaya, dada alimaliza Tumaini University na kupewa cheo kinyemela cha kuongoza wilaya ya Manyoni baada ya kushindwa tu kapelekwa BOT hah hahh sasa naona mzee ameamua kumpigia chapuo apewe ubunge. this is ccm inside

Shirikisha ubongo pia kabla hujasema kitu
Fancy hajawahi kuwa DC wa manyoni zaidi ya nyie kueneza umbea huu
Hafanyi kazi BOT pia
Simuungi mkono ila siwezi zusha maneno mabaya juu yake
OTIS
 
Hawana uwezo wa kumsaidia mzee sitta labda tusibirie upizani kama mbowe alivyosema cdm 1 sawa na magamba 30,huyo ndo ataweza kutupigania a mashariki vinginevyo wakenya watatuburuza kwa hawa wana cmc
 
Wamebebwa hawa wezi watupu,huoni huko zanzibar kilichofanyika,hapa walalahoi mpaka tupigane na hawa wachumia tumbo watatoa nafasi kwa walalahoi kushiriki kwenye uongozi wa taifa
 
katika majina haya yote sioni kama kuna hata mmoja ambaye amedhamiria kwenda kutetea nchi hii kama ilivyo kwa wanachama wenzetu (ie. Kenya, Uganda, Rwanda nk), sana sana ni kutafuta recognation tu na kuendeleza kujuana kusikoangalia masilahi ya nchi
 
Evans Rweikiza ..... he is good. ni mtendaji na si mwanasiasa.
 
katika majina haya yote sioni kama kuna hata mmoja ambaye amedhamiria kwenda kutetea nchi hii kama ilivyo kwa wanachama wenzetu (ie. Kenya, Uganda, Rwanda nk), sana sana ni kutafuta recognation tu na kuendeleza kujuana kusikoangalia masilahi ya nchi

Katika ile list ya watu 45 ,kulikuwa na watu ambao wangetuwakilisha vizuri tu kama nchi lakini wamechinjiwa baharini ili Vasco apate watu anaowataka yeye ili kukidhi matakwa yake!! Ndio maana ile list yote hawawezi kuiweka hadharani kwani Vasco na cc yake wataumbuka.Kama mtu angeweza kuipata list yote na kuibandika humu tungefumbuka macho na kujua mizengwe ya ccm mafia.
 
kesho wanajieleza Karimejee kwa wabunge wa CCM, tuwaombee wapambanaji wetu, William Malecela na Mrisho Gambo

Balozi.jpg
 
Wewe unadhani huu mgawanyo unakuja kwa bahati mbaya? Unadhani aliyetoka kwenye background ya familia ya ualimu anafurahia kuwa mwalimu ama analazimika (kwa sababu hana option) kuwa mwalimu na yeye pia kama wazazi wake waliomtangulia? Hii ni social class reproduction: na ipo hapo si kwa bahati mbaya kama unavyotaka kutuaminisha.

Hapo kwenye red especial ukiambiwa mchakato wa viti maalum uliofanywa na Kitila ndio utachoka kabisa. Uliyoyasema yote ni kweli kabisa ila tuangalie pia je ni asilimia ngapi ya hao watu ndani ya siasa?
 
Mnapeana tu vijiti? Leo mwinyi sinia, kesho junia, saaafi kabisa.. Cku yenu yaja...., hamtatamani kuitwa Mwinyi, Bilal au malechela!
 
Back
Top Bottom