Jamani Utotoni kuna vituko..mpaka unakua ni mambo mengi na vituko vingi tumepitia,mojawapo ni majina tuliyokuwa tunatungiana kwa jinsi mtu alivyo au kwa kituko alicho fanya na majina mengine hadi leo yamedumu mimi kwa leo na kuletea baadhi ya majina ya marafiki zangu pamoja na mm enzi za utoto nawe ukipata wasaa tupia lako..
1.Kashiba andazi
2.Sudi nyodo
3.Njino za panya
4.Chogo chuma
5.Bata
6.Makunde
Ha ha haaa mkuu suri
Umenikumbusha mbali sana, huyo jamaa wa mwisho hapo alikuwa anaitwa amisi nyaloo, jamaa alikuwa ana nguvu za mikono ile mbaya.. Akikukamata hautoki mkononi..
Mi Nyumbani nilikuwa naitwa Mbavu mbili, shuleni Nyagagwahase au Babu, nilikuwa naonekana nimekomaa kabra ya wakati. walikuwepo pia Umoja wa vijana, Zee la kisiwa, Jitu la kumsitu, Msagemsage, DJ machacha, Sipika ya kwafau. ISENGA P/SCHOOL MWANZA
Mtoto wa MGANA MSINDAI mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM. Sami Musindai, a.k.a(Samy) tukiwa (std.v) tukisoma somo la Jiografia. akawa anasinzia mwalimu alipo mubaini akamuita we Sami yeye akakurupuka na kusema Bonde la ufa. akawa bondela ufa. ISENGA P/S