Nimepitia majina ya timu za taifa kwa mataifa yote ya Afrika nikahisi kuwa Tanzania, Ghana na Kenya inabidi tubadilishe majina yatu; neno "stars" linakuwa monontonous. Somalia na South Sudan wamelitumia pia lakini kwao wamelitumia taifauti na sis. Hebu angalia halafu utoe maoni yako.
- Algeria - The Greens au Desert Warriors (Wapiganaji wa jangwani)
- Angola - Black Sable Antelopes (Tandala Weusi)
- Benin - The Cheetahs (Duma)
- Botswana - The Zebras (Pundamilia)
- Burkina Faso - The Stallions (Farasi wa kiume)
- Burundi- The Swallows (Mbayuwayu)
- Cameroon - The Indomitable Lions (Simba wasiofugika)
- Cape Verde -Blue Sharks (Papa wa bluu)
- Central African Republic - The Wild Beasts (Wanyama pori wakali)
- Chad - Les Sao (Wazawa wa Sao) - Sao ilikuwa ni himaya ya zamani sana huko Chad
- Comoros - The Coelacanths (Hawa ni samaki wanopatikana Comoros, Tanzania, Madagascar na Mozambiki tu; sikuweza kupata jina lao kwa kiswahili)
- Congo (Republic) - The Red Devils (Shetani wekundu)
- Djibouti -Shoremen of the Red Sea (Watu wa pwani ya bahari nyekunu) - Djibout inapakana na bahari nyekundu.
- Congo (DRC)- The Leopards (Chui)
- Egypt (Misri)- The Pharaohs (Watawala wa Zamani wa Misri)
- Equatorial Guinea - National Thunder (Radi ya taifa)
- Eritrea - Red Sea Camels (Ngamia wa bahari Nyekundu) - Eritrea nayo inapakana na bahari nyekundu.
- Eswatini - King's Shield (Ngao ya Mfalme)
- Ethiopia The Walia Ibex (Mbuzi pori)
- Gambia - The Scorpions (Nge)
- Ghana- Black Stars (Nyota nyeusi) ???? !!! ???? !!!
- Guinea - National Elephants (tembo wa taifa)
- Guinnea Bissau - The Dromedaries (Ngamia wenye nundu moja)
- Ivory Coast -The Elephants (Tembo)
- Kenya - Harambee Stars (Nyota za Harambee) ???? !!! ???? !!!
- Lesotho- Crocodiles (Mamba)
- Liberia - The Lone Stars (Nyota wapwekwe)
- Libya - The Mediterranean Knights (Askari maalum wa Mediteraneae) - Libya inapakana na bahari ya Mediteranean.
- Madagascar - Barea (Ng'ombe mkubwa)- Barea ni aina ya ng'ombe wakubwa wanaopatikana Madgascar tu.
- Malawi- The Flames (Ndimi za moto)
- Mali- The Eagles (Tai - ndege siyo vazi)
- Mauritania- Lions of Chinguetti (Simba wa Chinguetti)- Chinguetti ni kijiji fulani huko jangwani ndani ya Mauritania kilichokuwa maarufu sana kwa biashara enzi za zamani.
- Mauritius - The Dodos (Ndege wa Zamani aliyekuwa anapatika Mauritius tu) - Ndege huyu alishatoweka.
- Mayotte - Seahorses (farasi wa majini)
- Morocco - The Atlas Lions (Simba wa jangwani)
- Mozambique - The Mambas (Nyoka wenye sumu kali)
- Namibia - Namibia Warriors (Wapiganaji wa Namibia)
- Niger - Ménas (Mtakatifu Menas wa Misri)
- Nigeriua - Super Eagles (Tai wakubwa kuliko wote)
- Reunion - Club R (Timu R, wakifupisha jina la Reunion)
- Rwanda - Amavubi (manyigu)
- Sao Tome - Warriors of the Equator (wapiganaji wa ikweta) - Timu hii ina majina matatu lakini hili ndilo linajulikana zaidi kwa wapenzi wake, jingine ni The Elephants (tembo), na Falcons and True Parrots Team (timu ya vipanga na kasuku)
- Senegal - Lions of Teranga (Simba wa Teranga) - teranga ina maana ya uungwana na upole, kwa hiyo timu hiyo ni "Simba wa Unngwana"
- Seyschells - The Pirates (maharamia wa baharini)
- Sierra Leone - Leone Stars (Nyota wa Leone). Jina hili linahitaji maelezo marefu kidogo lakini nitaliacha hivyo hivyo kwani unahitaji kujua maana ya "Sierra Leone" kwanza kabla ya kuvuta neno "Leone."
- Somalia - The Ocean Stars (Nyota wa baharini)
- South Africa - Bafana Bafana (Wavulana)
- South Sudan - Bright Stars (Nyota zinazong'ara)
- Sudan - Falcons of Jediane ( Vipanga wa Jediane)- Jadiena kwa kisudani ina maana ya ndege ajulikanye kama secretary bird anyatesfrika kwa kiswhali kama ndege kilemba or karani tamba. Muungano wa kipanga na karani tamba sikuweza kutafasri.
- Tanzania - Taifa Stars (Nyota wa Taifa) ???? !!! ???? !!!
- Togo - The Sparrowhawks (Vipanga wadogo wadogo)
- Tunisia - Eagles of Carthage (Tai wa carthage) - cartahge ni mji wa zamani sana nchini Tunisia ulikuwa na maendeleo sana lakini baadaye ulibomolewa na utawala wa warumi baada ya kukataa kutii amri za mtawala wa roma.
- Uganda - The Cranes (Korongo - ndege siyo korongo la ardhi)
- Zambia - Chipolopolo (Risasi za Shaba)
- Zimbabwe - The Warriors (Wapiganaji)
Star maana yake ni nyota, yaani kitu kinachon'gaa angani. Watu maarufu huitwa star kwa maana hiyo hiyo ya nyota kuwa wanag'aa. kama nyotaMeaning of the word star
1. Noun (OBJECT IN SPACE)
very large ball of burning gas in space that is usually seen from the earth as a point of light in sky
2. Noun (FAMOUS/SUCCESSFUL PERSON)
a very famous or successful person, especially a musician, actor, or sports player.
Neno stars kwenye Taifa Stars ina Maana ipi kati ya hizi mbili?
Kiswahili halisi cha indomitable ni "wasiotawalika" au kwa maneno mengine "unsubduable" au "unconquerable." Kutokutawalika ni passive na haina maana sawa na kutoshindwa ambayo ni active. Kutawalika ni sawa na kufugwa. Ni semantics tuIndomitable ni Kiingereza cha kawaida, na wala hakitumiki kwa simba tu, unaweza kusema mtu ana "indomitable courage", hii maana nyingine ya bweni bweni chanzo chake nini?.
KK Eleven ya akina Kalusha Bwallya walikuwa wakali sana lakini baada ya Kaunda kutolewa madarakani, matumizi ya KK nayo yakaisha. Chipolopolo ni jina zuri sana.Kwangu mimi Zambia watakuwa na wataendelea kuwa KK Eleven (Best Zambian Team waliokufa) na baada ya hapo The Mighty Zambia
Ni upuuzi tu.No reforms No election
Ni upumbavu tuNi upuuzi tu.
Leo mchana nilikuwa nawaza majina ya timu za mataifa ya Afrika Mashariki nilipofika kwa Burundi nilikumbuka Intamba tu
Wanajiita mbayuwayu yaani intamba murugamba.Leo mchana nilikuwa nawaza majina ya timu za mataifa ya Afrika Mashariki nilipofika kwa Burundi nilikumbuka Intamba tu
Rwanda ni amavubi au sivyoWanajiita mbayuwayu yaani intamba murugamba.
Yes, amavubi (manyigu).Rwanda ni amavubi au sivyo
😁 No reforms no ELECTIONMkuu huu muda wa kuchambua hayo majina unaupata wapi.
Yeah 😂.Ndiyo mbayuwayu hao.
Wao ama ama tuYes, amavubi (manyigu).
Uwanja wao unaitwa Amahoro yaani uwanja wa amani. (Amahoro -amani).
Ni mambo ya ama ama kwa kwenda mbele 😎.Wao ama ama tu